Sheria ipite wauza maduka ya madawa wote wavae mask (barakoa)

Ushirombo

JF-Expert Member
Jan 22, 2013
3,557
2,692
Wakuu nimekaa nikatafakari sana, kuwa tabia zetu Watanzania huwa hatuna tabia sana za kwenda hospital hadi mambo yazidi unga, sasa basi ninachokiona hapa maduka ya madawa inaweza kuwa mahali ambapo virus wa corona watakua wanapatikana sana hasa ukizingatia kuwa virusi wenyewe ni airborne, na vile Watanzania wengi anaweza akawa na hao virus akaona anunue tu dawa kwa ajili ya kujitibu kabla ya hospital, sasa wakuu tujilinde sana hasa unapoingia maduka ya madawa na mengi yamefungiwa vioo hayana air circulation.

Mapendekezo yangu
1. Unapoenda duka la madawa jitahidi kutumia muda mfupi, vaa mask na jitahidi usiguse guse vitu vya humo.

2. Wauzaji, kama mama Ummy unasoma hapa tafadhali toa sheria wote wavae mask muda wote kwani ni group ambalo liko vulnerable sawa sawa na wafanyakazi wa hospitali.

3. Maduka ya madawa yawe yanapuliziwa dawa fumigation kila baada ya muda dulani.

Hayo ndo maoni yangu wakuu, karibuni tushee, sababu nimeona angle hii watu wengi hawajaiona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom