Sheria inayotamka kutaja hadharani makosa ya Rais ni ipi hiyo na ni ya mwaka gani?

Mtu anafananisha kuchunga ng'ombe uko kijijini kwao na kuongoza 50 Million Intelligent people!!Ng'ombe unaweza waswaga tu na wakaenda unapotaka waende,hawawezi kukupinga wala kukususia,lakini kwa sisi wa TZ amabao ni nchi Huru na tumekupa sisi cheo huwezi hata siku moja kujifanya huko juu yetu wala huwezi kutunyamazisha.Wewe una je.shi na hao matakataka mengine lakini sisi tuna Mungu ambaye atatupigania mpaka mwisho.Kwani kufa kitu gani,na hata kama ni kuua utaua wangapi?

Usitubabaishe Bwana,kwanza Kizungu chenyewe hujui.
 
kwann lisu anamsema mheshimiwa hadharani?? mm mwenyewe ningekua (rahisi) nisingekubali
 
Hii habari iliyopa hapa JamiiForums ya kusema kwamba kutaja makosa ya Raisi hadharani ni kosa ni habari ambayo tu si imenishangaza, bali imenishitua sana maan tafsiri yake kwa mtazamo wangu ni kosa kisheria kumkosoa Raisi kwa kutaja makosa yake hadharani.

Sasa wadau,mwenye kuielewa vizuri hiyo sheria naomba atuwekee hapa ili wengi tuifahamu na tuepuka kutenda kosa hilo(kama kweli lipo)

Na kama habari hii imeripotiwa kimakosa basi ni vizuri irekebishwe/ifafanuliwe na wahusika.

Mods nawaomba sana maana leo huyu kesho unaweza kuwa wewe au mimi hivyo nawaomba msihamishe hii mada kwenda jukwaa lingine wala kuiunganisha.

Vyombo vya habari na wamiliki wa mitandao mbalimbali ni wakati wa kila mmoja wenu kutambua hatari iliyopo na kutimiza wajibu wake hasa kwa kuyapa umuhimu wa kipekee mambo ya aina hii katika vyombo vyenu vya habari au mitandao mnayomiliki.

Mnaweza mkadharau lakini kaeni mkijua mtakuja kushituka when it is already too late.
Katika suala hili aliyekuwa mmoja wapo wa pande husika katika kesi ni serikali na baada ya kuzuiliwa kwa ndege huko Canada, serikali ya Tanzania ambayo ndiye sehemu ya kesi hiyo ilijulishwa kwa attachment hiyo (Notification). Hakujulishwa Tundu Lissu. Hivyo, serikali ndiyo ilipashwa kuitisha Press Conference na kuujulisha umma kuwa ndege ambayo ilitarajiwa kuwasili mwezi july haikuja katika muda huo kutokana na kushikiliwa, lakini siyo Tundu Lissu kufanya hivyo. Inasemekana kuwa Tundu Lissu ndiye amekuwa mstari wa mbele kuwashawishi kwa kiwango kikubwa hao jamaa na amewasaidia kwa kuandaa nyaraka ili wakafungue kesi na amewasaidia kuonyesha ni wapi mali ya serikali ya Tanzania ilipo ambayo ni ndenge. Kwa hiyo hapa kuna kitu kimoja tu ambacho ni KUSHAWISHI jamaa wafungue kesi dhidi ya serikali. Kwa mjibu wa sheria ya Uwakili, kumshawishi siyo zuri. Hivyo, kutokana na mambo yanayozidi kumkumba huyu Tundu Lissu hasa ya kiuchochezi, sitashangaa kuona hapo baadaye anafunguliwa kesi ya UHAINI ambayo ni kesi kubwa sana kuliko kesi zote za jinai na ambayo imetamkwa katika katiba ya 1977. Ni suala la kumuombea kwa mungu kuliko kuweka ushabiki mbele.
 
  1. Ndimi Bwana Mungu wako usiabudu miungu mingine.
  2. Usilitaje bure jina la Mungu wako.
  3. Shika kitakatifu siku ya Bwana.
Hizo ndizo amri (maagizo) TATU za kwanza za Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.

Naenda zangu Zimbabweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. nimechoka mie!
 
Katika suala hili aliyekuwa mmoja wapo wa pande husika katika kesi ni serikali na baada ya kuzuiliwa kwa ndege huko Canada, serikali ya Tanzania ambayo ndiye sehemu ya kesi hiyo ilijulishwa kwa attachment hiyo (Notification). Hakujulishwa Tundu Lissu. Hivyo, serikali ndiyo ilipashwa kuitisha Press Conference na kuujulisha umma kuwa ndege ambayo ilitarajiwa kuwasili mwezi july haikuja katika muda huo kutokana na kushikiliwa, lakini siyo Tundu Lissu kufanya hivyo. Inasemekana kuwa Tundu Lissu ndiye amekuwa mstari wa mbele kuwashawishi kwa kiwango kikubwa hao jamaa na amewasaidia kwa kuandaa nyaraka ili wakafungue kesi na amewasaidia kuonyesha ni wapi mali ya serikali ya Tanzania ilipo ambayo ni ndenge. Kwa hiyo hapa kuna kitu kimoja tu ambacho ni KUSHAWISHI jamaa wafungue kesi dhidi ya serikali. Kwa mjibu wa sheria ya Uwakili, kumshawishi siyo zuri. Hivyo, kutokana na mambo yanayozidi kumkumba huyu Tundu Lissu hasa ya kiuchochezi, sitashangaa kuona hapo baadaye anafunguliwa kesi ya UHAINI ambayo ni kesi kubwa sana kuliko kesi zote za jinai na ambayo imetamkwa katika katiba ya 1977. Ni suala la kumuombea kwa mungu kuliko kuweka ushabiki mbele.
Sidhani kama una akili timamu, au HujuI kwa ufasaha hili suala. jaribu kuwaza kwa akili yako badala ya kuwa DODOKI.
 
Sikushangai sana kwa matusi yako hayo na kuropoka. Maana hata huyo aliyelazwa selo, amelazwa huko kutokana na kuwa na tabia ya maneno machafu na uropokaji kama wewe. Matusi na maneno machafu hayatamuondoa mwenziyo selo, ila tu sheria za nchi.
 
Hii habari iliyopa hapa JamiiForums ya kusema kwamba kutaja makosa ya Raisi hadharani ni kosa ni habari ambayo tu si imenishangaza, bali imenishitua sana maan tafsiri yake kwa mtazamo wangu ni kosa kisheria kumkosoa Raisi kwa kutaja makosa yake hadharani.

Sasa wadau,mwenye kuielewa vizuri hiyo sheria naomba atuwekee hapa ili wengi tuifahamu na tuepuka kutenda kosa hilo(kama kweli lipo)

Na kama habari hii imeripotiwa kimakosa basi ni vizuri irekebishwe/ifafanuliwe na wahusika.

Mods nawaomba sana maana leo huyu kesho unaweza kuwa wewe au mimi hivyo nawaomba msihamishe hii mada kwenda jukwaa lingine wala kuiunganisha.

Vyombo vya habari na wamiliki wa mitandao mbalimbali ni wakati wa kila mmoja wenu kutambua hatari iliyopo na kutimiza wajibu wake hasa kwa kuyapa umuhimu wa kipekee mambo ya aina hii katika vyombo vyenu vya habari au mitandao mnayomiliki.

Mnaweza mkadharau lakini kaeni mkijua mtakuja kushituka when it is already too late.
Usipotoshe
Unapomkosoa raisi hata mtu yeyote huwe na vigezo vya kufanya hivyo.
Siwezi kukushutumu mwenye hospital kwa kifo cha mgonjwa ambacho either limefanywa na Doctor mhusika, nesi au yule aliyemleta mgonjwa.

Hili ndilo anguko la Tundu,
Hanyanyuki tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina maana rais wa Tanzania yuko above reproach?

Huu utawala wa Magufuli umezidi sasa.
Ukitaka kujua jinsi ya hiyo aproach jaribu kutumia mwenendo wa lisu, mkosoe bosi wako. Usitoke nje wala kuita waandishi wa habari. Toa shutuma humo humo ofisini kisha hakikisha zimemfikia boss.
Alafu tupe marejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kosa la Lissu ni kumwambia mfalme kwamba mtukufu mfalme haujavaa Nguo. Wasaidizi wote wa mfalme wanamwona mfalme yupo uchi ila wanamwambia mheshimiwa mfalme umevaa vazi la thamani kubwa limepambwa kwa johari.
 
Unajiuliza ni kwanini hata tulidai uhuru!!
Mi naona bora mwingereza angebakibaki kidogo,sijui tulukuwa tuna haraka gani wakati kujitawala wenyewe hatuwezi,miaka 50 ya uhuru alafu hata madawati darasani bdo ni changamoto,tulipaswa tupate uhuru kwenye miaka ya tisini.
 
Nafikiri sasa Mh. Rais anatakiwa aingilie kati. Mapolisi na wakuu wa wilaya/mikoa wanamfanya anaonekana vibaya mbele ya jamii anayoingoza.
Rais kukosolewa sio dhambi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeye ndie anayewatuma.unadhani wanakurupuka tu,kwani awamu ya kikwete hakuku na ma RC,DC na polisi?,mbona huu ujinga haukuwepo?.
 
Katika suala hili aliyekuwa mmoja wapo wa pande husika katika kesi ni serikali na baada ya kuzuiliwa kwa ndege huko Canada, serikali ya Tanzania ambayo ndiye sehemu ya kesi hiyo ilijulishwa kwa attachment hiyo (Notification). Hakujulishwa Tundu Lissu. Hivyo, serikali ndiyo ilipashwa kuitisha Press Conference na kuujulisha umma kuwa ndege ambayo ilitarajiwa kuwasili mwezi july haikuja katika muda huo kutokana na kushikiliwa, lakini siyo Tundu Lissu kufanya hivyo. Inasemekana kuwa Tundu Lissu ndiye amekuwa mstari wa mbele kuwashawishi kwa kiwango kikubwa hao jamaa na amewasaidia kwa kuandaa nyaraka ili wakafungue kesi na amewasaidia kuonyesha ni wapi mali ya serikali ya Tanzania ilipo ambayo ni ndenge. Kwa hiyo hapa kuna kitu kimoja tu ambacho ni KUSHAWISHI jamaa wafungue kesi dhidi ya serikali. Kwa mjibu wa sheria ya Uwakili, kumshawishi siyo zuri. Hivyo, kutokana na mambo yanayozidi kumkumba huyu Tundu Lissu hasa ya kiuchochezi, sitashangaa kuona hapo baadaye anafunguliwa kesi ya UHAINI ambayo ni kesi kubwa sana kuliko kesi zote za jinai na ambayo imetamkwa katika katiba ya 1977. Ni suala la kumuombea kwa mungu kuliko kuweka ushabiki mbele.
Tafuta maana ya neno Kimeo halafu ujitathmini upo upande gani wa vimeo!
 
Back
Top Bottom