Sheria inasemaje Tanesco Inaposema haina meter za luku wakati mteja kaharibikiwa na LUKU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria inasemaje Tanesco Inaposema haina meter za luku wakati mteja kaharibikiwa na LUKU

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by babayah67, Aug 3, 2011.

 1. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanasheria, naomba kueleweshwa sheria inasemaje katika tatizo langu na Tanesco.
  Mimi ni mteja wa Tanesco kwa muda mrefu, na meter ninayotumia ni ya LUKU. Sasa ni Alhamisi iliyopita meter yangu ilikata umeme, yaani umeme ukawa hauingii ndani ya nyumba, wakati unit zinasomeka kwenye meter. Nilienda reporti tatizo hilo Tanesco na jibu walilonipatia ni kuwa meter hiyo imeharibika na hivyo inatakiwa ibadirishwe. Nilipouliza lini watakuja badilisha, walinijibu kuwa kwa sasa hawana akiba ya meter, hadi hapo zitakapokuja ndio nitapatiwa.

  Toka hiyo Alhamisi leo ni siku ya sita sina umeme. SWALI ni Je sheria inasemaje Tanesco inaposhindwa nipatia meter wakati ni jukumu lao la msingi??? Je naweza washitaki ????

  NB: Naomba Tanesco au Serikali wajaribu kutoa ukiritimba katika suala hili la LUKU, wajaribu kuruhusu watu binafsi waingize Luku madukani watuuzie kama TRA walivyofanya kwenye EFD.
   
Loading...