Sheria inasemaje mwanamke anapopata ujauzito kutokana na kuwa mhanga wa ubakaji?

Jan 1, 2020
78
89
Napenda kuuliza ili nipate maoni yenu waungwana kuhusu hili:

Je ikitokea mwanamke/msichana amepata ujauzito kutokana na kuwa Mhanga Wa ubakaji na kwa bahati nzuri yule mbakaji akaswekwa ndani yani kutumikia kifungo chake, je sheria inasemaje kuhusu mambo yafuatayo:

1. Matunzo ya huo ujauzito wa mbakaji endapo victim atafanikisha kuthibitisha kuwa ni ujauzito wake.

2.Ni nani atakayekuwa na wajibu Wa kumlea huyo mtoto wa mbakaji atakayezaliwa?

3. Je, sheria zetu zinaruhusu ustawi wa jamii kuwa na wajibu wa moja kwa moja katika kusaidia mtoto anayezaliwa katika mazingira ya namna hii?

4. Je practice ikoje kwa sasa katika case zinazohusisha mazingira ya namna hii?

Angalizo:
Yeyote anayeona kuna gap la sheria katika haya kama ninavyona mimi anaweza nishauri nifanye utafiti zaidi kuhusu haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom