Sheria inasemaje kwa mbunge aliyekutwa nakosa mahakamani na kuhukumiwa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria inasemaje kwa mbunge aliyekutwa nakosa mahakamani na kuhukumiwa??

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KakaKiiza, Dec 30, 2010.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Wakuu naomba kueleweshwa juu ya mwenendo wamakosa yajinai na yasiyokuwa ya jinai,
  Sheria inasemaje kwa mbunge aliyekutwa na kosa mahakamani na kutolewa hukumu na Hakimu wa Mahaka ya Jamuhuri ya muungano Tanzania juu yake??Sheria ina semaje??
  Mfano kesi ya Andrew Chenge kama Mbunge wa Jimbo la Baliadi!Je sheria inazungumza vipi kwa mtu kama huyo je ubunge wake unaendelea au hukumu inakuwa imetengua ubunge wake??:help:
   
 2. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ya chenge ni jinai lakini iko tofauti sana ile tuloizoea, hii iko sana under torts na huwa ina special registry yake tofauti na jinai za kina liyumba /mramba/epa n.k

  chenge yuko salama ktk ubunge wake maana ile charge yake haikuwa kama ya kijana aliyesababisha kifo cha wangwe chacha.

  Pale ni uzembe zaidi ktk management ya gari na blablaaa zingine.
  Mwacheni apumzike vijisenti wa watu. Amechoka sana maana kabla ya jana ni jela ya kutosha alishakuwa +++makashfa yote alokombana nayo na kuukosa u spika !!!
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Au nitatizo la polisi kuwasilisha mashtaka mahakamani??Kuendesha gari bila yakuwa na insurance sikosa lajinai???achilia mabali kugonga!!
   
 4. A

  ALIBAALIO Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani tuwekane sawa na kuelimishana kesi ya Chcha wanwe na chenge zote zilifunguliwa chini ya sheria za makosa ya barabarani hivyo kisheria zina uzito sawa.tofauti iliyopo ni nani na ana nafasi gani katika jamii mtu aliyeusika katika kesi.mfano yule wa chacha mojawapo ya kosa alilohusika nalo ni kuendesha gari bila leseni na kusababisha kifo.yule alihukumiwa kama sikosehi miaka 3 chenge hakuwa na bima nae alisababisha kifo lakini hukumu yake ilikuwa 100000 au kifungo miezi 6 angalia tofauti hapa.lakini utofauti huu unaletwa na discrition waliyonayo mahakimu kwenye kesi za trafic.kuna dereva mmoja wa buffalo alisababisha ajali mwaka 2002 na watu 35 walipoteza maisha lakini dereva alihukumiwa miez 7.yule anayesema kesi ya chenge imekuwa hivyo kwa sababu ni tort sio kweli inafika kuwa tort baada ya hukum ya jinai na hapo ndugu wa marehem wanaweza kufungua kesi ya madhara {tort}kudai fidia
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Je bado an haki ya kuwa na ubunge baada ya huku hii??
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  In reality ni kwamba, sheria za Tanzania zinatekelezwa kwa kuangalia ni nani amefanya kosa gani. Ideally sheria haichagui ni nani amefanya kosa au amefanya kosa. Lakini hapa Tanzania kama watu fulani wakifanya makosa, kuna ile issue inayosemwa kuwa "tutamsaidiaje mwenzetu". Kuna mifano mingi tu ya kesi kama hizi.

  Kwa mfano Ditopile committed a first degree murder, lakini treatment yake ilikuwa tofauti kabisa na wengine wanao-commit first degree murder, walibananga sheria na kuzuga na akaachiwa "huru". Excuse ilikuwa "mazingira" wenye uelewa mzur wa sheria kama Buchanan wanaweza kueleza vizuri. Kuna wengine waliofanya kosa very siilar na Dito lakini matokeo yao ni tofauti kabisa ilivyokuwa Dito, kwa hiyo suala ni nani ni nani na amefanya kosa gani.

  Jaribu kujiulia kamambunge wa Upinzani ndio angekuwa amefanya kosa kama la Chenge. Sijui sheria yetu inapima vipi thamani ya uhai mpaka ikafikia hataua ya kumtoza Chenge laki 7, na sijui hizo laki 7 zilikwenda kwa nani na kwanini, wafiwa? mwenye Bajaji? mfuko wa serikali?

  Sijui makosa mengine kama hayo yaliyotokea huko nyuma yalishughulikiwa vipi, watu walitozwa faini? kigezo gani kilitumika kutoza hiyo faini? au walitumikia adhabu ya kifungo na faini?

  In short, mwenye nguvu ndio mwenye haki, japo tunasema sheria intoa haki sawa.
   
 7. Hiphop

  Hiphop Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 17, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ninaomba nitoe ufafanuzi kutokana na uelewa wangu wa sheria,ni kweli kesi ya chenge imeisha na amekutwa na hatia,katiba ya jamhuri ya muungano imesema kuwa hurusiwi kugombea ubunge ikiwa umekutwa na hatia ya kosa linaloweza kukuweka ndani kuanzia miezi 6,lakini mpaka sasa sijajua sheria inasemaje pale kosa hilo linapofanyika na m2 ambaye tayari amekwisha kuwa mbunge.Kuhusu suala la Ditopile alishtakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia yani 'manslaughter',kosa hili linastahili dhamana,mtazamo wangu ni kwamba kitengo cha prosecution ndio kina uwezo wa kuharibu au kutengeneza kesi nzuri,wao walichagua kumshtaki kwa manslaughter badala ya murder,vivyo hivyo wangeweza kumshtaki chenge kwa reckless driving ili akikutwa na hatia afungwe kuanzia miezi 6 hadi miaka 2,kwa maana faini ya laki 7 si kitu kwake na hairudishi uhai wa wa2 wawili waliofariki.Ndugu wa marehemu wanatakiwa kufungua kesi ya madai ili wapate fidia ya vifo vya ndugu zao.Kuna uozo mkubwa sana kwenye Prosecution section nchi hii.
   
 8. m

  mams JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nadhani kuna vitu havipashwi kubinafsishwa kulingana na sensitivity yake ktk jamii. Hii ni pamoja na legal system na hivi tunaambiwa haturuhusiwi kuongelea jambo lililokwisha tolewa uamuzi na mahakama, mmmh!


  Jaji mstaafu alipokuwa anaaga alisema kuna baadhi ya hukumu alikuwa anazitilia shaka na kuzifuatilia na hii sijui kama angefuatilia!
   
Loading...