Sheria inasemaje kuhusu mkuu wa nchi kufanya uhaini dhidi ya nchi anayoiongoza ?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
Makosa ya uhaini,
Mara nyingi hutafsiriwa kama nyanja ya mahusiano baina ya Serikali na raia wa nchi husika. Raia wa nchi husika anapofanya vitendo vya hujuma dhidi ya taifa lake huyo huhesabiwa kama mhaini. Vitendo hivyo ni kama Kushirikiana na adui wa Jamhuri, Kutaka kumdhuru Raisi wa nchi yako, Kutaka kupindua serikali na Kuitesa Serikali.


Hapa nchini Tanzania uhaini umetafsiriwa kisheria katika barabara iendayo kumoja tu, ambapo uhaini ni vile vitendo vinavyoweza kufanywa na raia dhidi ya Serikali yao. Hii dhana imejikita katika kuamini kwamba MTAWALA HAWEZI KUKOSEA KAMWE wala hawezi kufanya hujuma dhidi ya Jamhuri anayoingoza. Je, hii dhana ina ukweli wowote ule ndani yake ???

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikosea na wananchi wasiridhike naye Katiba yetu ya mwaka 1977 inasema ataondolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano tu. Mbali na hapo haitawezekana kabisa kumgusa kabisa kwasababu amepewa kinga (Immunity) inayomlinda dhidi ya kuburuzwa mahakamani akiwa madarakani na akistaafu. Kwa kiingereza tunasema Functional Immunity na Personal Immunity, hivyo hawezi kuguswa kabisaaa.

Sasa naomba niulize:
Je, kama imegundulika kwamba mkuu wa nchi amefanya hujuma dhidi ya Jamhuri ya anayoiongoza hapa Sheria ya nchi yetu inasemaje ???? Ataguswa na nani ???
 
Kwa nchi zenye majeshi ya wananchi jeshi likiona rais anaihujumu nchi linaweza kumshauri ajiuzulu, kumuondoa au kumuweka hata kizuizini kama ilivyofanyika Zimbabwe, Misri na Tunisia.
Mimi nimezungumzia Sheria siyo Majeshi mkuu
 
Ikulu ni mahali patakatifu. Mtu aliyewekwa patakatifu petu kupitia uchaguzi huru na wa haki, anakuwa mtakatifu, ndio maana kwa mujibu wa katiba, rais wa JMT hawezi kushitakiwa mahakamani, na urais ana pande mbili,

1. Rais ni taasisi, presidential institution, huyu ni mtakatifu, hawezi kukosea ndio maana ana kinga ya kutokushitakiwa kwa sababu yote ayafanyayo akiwa ikulu, yanakuwa yametakasika, hivyo rais wa JMT, sio tuu hawezi kufanya uhaini, bali hawezi kufanya kosa lolote na anapaswa kuitwa mtukufu rais.

2. Rais as person, huyu ni binadamu kama binadamu wengine wote na anaweza kukosea ambapo Bunge linaweza kumuondosha madarakani andapo atakiuka katiba na kosa la uhaini haliwezi kufanywa na rais wa JMT aliye madarakani.

P
 
Ingawaje mimi si Mwanasheria na kwahiyo sifahamu lolote kuhusu Sheria za Katiba, bado naamini unaweza kuokoteza vifungu na akapatikana na hatia pamoja na Urais wake na kinga yake!

Nitarudi nikishaokoteza na kutumia layman reasoning!

Mkuu Malcom Lumumba, nimerejea... naona hapo chini umesema nirudi na kweli nimerudi!

Anyway, hoja yangu nimeandika kwa haraka haraka na kwahiyo inawezekana ikakosa mpangilio muafaka! Hata hivyo, ni matumaini yangu utanielewa:

Tuanze na the so called Kinga ya Rais kushitakiwa na kwahiyo tutafute namna ya ku-utilize hiyo sheria.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 46 (3) inasema: Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.

Ukiisoma hiyo ibara utaona hiyo kinga hapo ni conditional kwamba, rais akishatoka madarakani itakuwa ni marufuku kumshitaki au kufungua mahakamani shauri lolote... ISIPOKUWA kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46 (10).

Now, Ibara ya 46A(10) inasemaje:

Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.

Kumbe basi, na kila mmoja anafahamu kwamba Bunge linaweza kumtoa Rais madarakani! Na ibara ya 46 (3) inasema Rais akitoka madarakani hawezi kushitakiwa ISIPOKUWA kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46 (10)... yaani hawezi kushitakiwa except kama ametoka madarakani baada ya kuwa impeached kwa mujibu wa Ibara ya 46 (10).

Kupigilia msumari, Ibara ya 46 (11) inasema:

Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

Kumbe basi, Rais anakuwa na privilege zote hizi IF AND ONLY IF utokaji wake madarakani hauhusiani na kuondolewa na Bunge! Akishaondelewa na bunge tu, nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge!

Moja ya hizo nafuu ni KUTOSHITAKIWA mahakamani!

Now, turudi sababu ambazo zinaweza kulipa bunge meno ya kumwondoa Rais madarakani!

Ibara ya 46 (1) & (2) ndiyo zinaelezea suala la Kinga ya Rais kutoshitakiwa huku Ibara ya 46 (3) ikieleza kwamba kutoshitakiwa kwake ni conditional.

Ibara ya 46 A (1) Inasema: Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

Kumbe basi, ingawaje Ibara ya 46 (1), (2) & (3) inazungumzia kinga ya Rais kutoshitakiwa, Ibara ya 46A(1) inaeleza kumbe Bunge linaweza kumuondoa Rais madarakani!

Ibara ya 46A(2) inaorodhozesha makosa ambayo yanaipa mamlaka Bunge kumwondoa Rais madarakani ambapo Ibara ya 46A(2) (a) inasema: Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

NOW, hoja yako ni Rais kufanya Uhaini! Je, kufanya uhuni sio kwamba Rais " ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba..."?

Na Ibara ya 28 (4) ya katiba yetu inasema: Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Hivyo basi, Bunge linaweza kumuondoa madarakani Rais ikiwa itathibitika amtenda kosa la uhaini!

Na kwavile atakuwa ametoka madarakani kwa kuondolewa na Bunge, basi kwa mujibu wa Ibara ya 46 (3) & 46A(10) & 46A(11), Rais anaweza kufunguliwa mashitaka!

Kwa hapo tu, sidhani kama kuna haja ya kwenda kuangalia Sheria ya Uhaini inasemaje!!!
 
Ikulu ni mahali patakatifu. Mtu aliyewekwa patakatifu petu kupitia uchaguzi huru na wa haki, anakuwa mtakatifu, ndio maana kwa mujibu wa katiba, rais wa JMT ana pande mbili,

1. Rais ni taasisi, presidential institution, huyu ni mtakatifu, hawezi kukosea ndio maana ana kinga ya kutokushitakiwa kwa sababu yote ayafanyayo akiwa ikulu, yanakuwa yametakasika, hivyo rais wa JMT, sio tuu hawezi kufanya uhaini, bali hawezi kufanya kosa lolote na anapaswa kuitwa mtukufu rais.

2. Rais as person, huyu ni binadamu kama binadamu wengine wote na anaweza kukosea ambapo Bunge linaweza kumuondosha madarakani andapo atakiuka katiba na kosa la uhaini haliwezi kufanywa na rais wa JMT aliye madarakani.

P

Sasa kama Raisi hafanyi makosa yoyote yale kwanini Katiba inampa Kinga (Immunities) ??
Mkuu Pascal wewe ni mwanasheria mzuri sana labda unirekebishe hapa: Nijuavyo mimi ni kwamba kinga haifuti makosa bali inakuponya dhidi ya mkono wa sheria. Hivyo tukikifuta kipengele kinachompa Raisi kinga dhidi ya kushitakiwa, tutakutana na makosa mengi sana kama ya raia wengine wa kawaida na anaweza kushitakiwa kama raia wengine tu...
 
Back
Top Bottom