Sheria inasemaje kuhusu kesi ya madai? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria inasemaje kuhusu kesi ya madai?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ruhazwe JR, Aug 16, 2011.

1. Ruhazwe JR

Ruhazwe JR JF-Expert Member

#1
Aug 16, 2011
Joined: Jan 31, 2011
Messages: 3,412
Likes Received: 15
Trophy Points: 135
Ndugu zangu wana jamii forums ninaomba kufahamishwa juu ya kesi za madai kuanzia procedure za kufungua kes.ninadaiwa milion 3 ambazo niliazimwa na rafiki yangu wa karibu,wakti tunakopeshana tulienda kuandikiana kwa wakili wa kujitegemea,tulipofka pale wakili alidai hata kama tunapeana kindugu lazima tuweke kiwango cha riba endapo siku itazidi kwa siku ya marejesho.badaye mambo yakaeniendea vibaya ambapo hadi sasa sijaweza kurejesha mkopo na nipo namuuguza mke wangu ambaye anamtoto wa miez tisa.napigiwa simu na mtu ambaye simjui anadai yeye ni ndugu wa anaye nidai ananitafuta akiwa na RB ya kunikamata.naomb kujua haki zangu ni zp ingawaje nadaiwa ktk hl.nielimishen sina ufahamu wowote juu ya elimu ya sheria na nifanye nin maana nipo mbali na natafutwa kwa RB ukizingatia itakua ni mara ya kwanza kwenda pors na mahakam

2. B

Bongemzito Senior Member

#2
Aug 17, 2011
Joined: Nov 5, 2010
Messages: 163
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
ukishashitakiwa kwa kuwa tayari unao mkataba wa kimaandishi na ambao umepitishwa na mwanasheria hapo huna ujanja lazima utiwe hatiani na masharti utayopewa na mahakama utatakiwa udiclare pato lako ili uweze kulipa kwa awamu mpaka umalize deni la watu.....

3. Ruhazwe JR

Ruhazwe JR JF-Expert Member

#3
Aug 17, 2011
Joined: Jan 31, 2011
Messages: 3,412
Likes Received: 15
Trophy Points: 135

4. Ruhazwe JR

Ruhazwe JR JF-Expert Member

#4
Aug 17, 2011
Joined: Jan 31, 2011
Messages: 3,412
Likes Received: 15
Trophy Points: 135
Nashukuru kaka,je watazingatia sana uwiano wa den na kipato?mfan naweza kupata lak2 kwa mwezi watanikadiliaje

5. Nyani Ngabu

Nyani Ngabu Platinum Member

#5
Aug 17, 2011
Joined: May 15, 2006
Messages: 70,281
Likes Received: 27,954
Trophy Points: 280
The standard of proof is different. All you need is the preponderance of the evidence.

6. Pascal Mayalla

Pascal Mayalla JF-Expert Member

#6
Aug 17, 2011
Joined: Sep 22, 2008
Messages: 22,988
Likes Received: 12,501
Trophy Points: 280
Ruhazwe, kwanza kudaiwa sio kosa la jinai bali la madai hivyo hiyo RB isikutishe wala huwezi kutiwa ndani.

Aliyekushitaki atakuwa amekusingizia kesi ya wizi wa kuaminiwa lakini kama ni kudaiwa tuu sio kosa la kufunguliwa RB as if wewe ni mhalifu.

Dawa ya deni ni kulipa tuu, nakushauri kuwa mkweli kwa mdai wako mwambie your situation ya sasa na mpe commitment kuwa una nia ya dhati ya kulipa deni lake.

Kwa vile deni ni la muda mrefu, hivyo riba itakuwa imeliongeza mara dufu, kwanza lipa ile principal halafu omba waiver kwenye riba ili aipunguze to a reasonable ammount ambayo unajua utamudu kulipa.

Inawezekana ni wewe ndio umemfikisha mdai wako hapo alipofika kwa kutokuwa mkweli na longo longo nyingi.

Just feel good wala usijisikie vibaya kudaiwa. Hata hao matajiri unaowajua wewe, wana madeni lukuki.

7. Ruhazwe JR

Ruhazwe JR JF-Expert Member

#7
Aug 17, 2011
Joined: Jan 31, 2011
Messages: 3,412
Likes Received: 15
Trophy Points: 135

8. Ruhazwe JR

Ruhazwe JR JF-Expert Member

#8
Aug 17, 2011
Joined: Jan 31, 2011
Messages: 3,412
Likes Received: 15
Trophy Points: 135

pasco nashukuru sana kwa mchango wako,unanipa moyo,na kujiona si mpweke.nashukuru na kama una yakunijaza tena na zaidi am waiting for

9. Quinty

Quinty JF-Expert Member

#9
Aug 18, 2011
Joined: Mar 25, 2010
Messages: 463
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
Kama alivyosema Pasco kesi ya madai haihusiani na RB ya polisi. Itakuwa huyi ndugu yako ametoa taarifa za wizi au utapeli. Kama unavyosikiaga msemo wa mtaani kwamba mdaiwa hafungwi...huu msemo unaukweli 80%. Kisheria kinachotakiwa kufanyika ni huyo mdai wako kukuandikia hati ya nia ya kukushtaki kwa kushindwa kulipa deni ndani ya muda mliokubaliana kimkataba na baada ya muda atakao ainisha kwenye hati tajwa. Mara nyingi huwa ni siku 14 au 30 au yaweza kuwa zaidi. Ndani ya huo muda uliotajwa kwenye hati ya nia ya kukushtaki waweza ijibu kwa kumuomba akuongeze muda au waweza kupinga deni ama riba au waweza kukaa kimya. Muda ukiisha mdai wako atakupeleka mahakamani na utapata hati ya kuitwa mahakamani (summons) na nakala ya hati ya mashtaka (plaint), Hapo una siku 21 za kujibu kama wataka au waweza kaa kimya ukisubiri siku ya kusikiliza kesi kufika na kesi kuanza kusikilizwa. Mkataba mlioandikishana kwa wakili utakuwa ushahidi kwamba kweli alikukopesha pesa ambazo ulitakiwa kulipa ndani ya muda fulani. Kesi ikiisha na ikaonekana umeshindwa kesi basi hukumu itakuwa ulipe deni na gharama za usumbufu (kama zipo). Baada ya muda kupita na ukishindwa kulipa deni ataomba kukaza hukumu na kukamata baadhi ya mali zako, au kuomba fungwe mieze sita.
Pole kwa matatizo ila ni ya kawaida na yasikutie hofu ni vitisho tu. NB Polisi wakija na RB waambie hakuna kosa la jinai ila ni madai na awana haki ya kukukamata. Cha muhimu uwe na nakala ya mkataba mlioingia ili kuwashawishi polisi

10. Ruhazwe JR

Ruhazwe JR JF-Expert Member

#10
Aug 18, 2011
Joined: Jan 31, 2011
Messages: 3,412
Likes Received: 15
Trophy Points: 135

11. Ruhazwe JR

Ruhazwe JR JF-Expert Member

#11
Aug 18, 2011
Joined: Jan 31, 2011
Messages: 3,412
Likes Received: 15
Trophy Points: 135
Do!Quinty unatisha mkubwa,nashukuru kwa maelezo yako ya kina.je endapo atakua ameripot tofauti kama vile wizi/utapeli nitatumia njia gani kukanusha?

Nashukuru sana na ntazidi kuwafahamisha zaidi

12. E

Emanuel Mwasote Member

#12
Nov 8, 2015
Joined: Sep 2, 2013
Messages: 45
Likes Received: 0
Trophy Points: 13
da, wadau mko juu. naomba msaada pia
kuna jamaa nlifanya naye kazi, nikamkabidhi aendeshe Bajaji,ndani ya wiki akaondoka na 40000, na tairi sh 80000 na spanner 20000. yangu 2014 October, namdai kiheshma hanielewi.
sheria inasemaje?

13. daud donasian

daud donasian Member

#13
Nov 8, 2015
Joined: Nov 6, 2015
Messages: 79
Likes Received: 27
Trophy Points: 25
Angalia mahakama isifikie kupiga mnada mali zako,

14. dolevaby

dolevaby JF-Expert Member

#14
Nov 12, 2015
Joined: Aug 25, 2013
Messages: 6,911
Likes Received: 2,329
Trophy Points: 280
Nimegundua jambo watanzania ni waoga na tunadhuliwa haki zetu kwa kutojua SHERIA ...ndg mleta mada sijui mpaka leo mmefikia wapi manake uzi huu ni wamiaka mingi.....MTU anaekudai lkn anajifanya kujua kukupeleka Polis kwa utapeli manake hiyo ni Jinai banana nae Mahakamani....utamtupa kwesi ya utapeli then unampandisha yy Mahakamani kukufungulia KESI ya Uongo ikibidi unamtajia Fidia kubwa Kumfilisi ili akili imkae sawa kitu ambacho watu wengi hawajui...Polis hawafungui KESI za madai ukienda pale sanasana wakikuona hujielewi wanakwambia wamBakie kesi mdai wako wakiamini wee utawapoza Hela...ikiwa wanajua wee utashindwa Mahakamani lkn wameshakula kwako

15. D

Dhambi nguo na wew unazo New Member

#15
Feb 15, 2017
Joined: Feb 11, 2017
Messages: 3
Likes Received: 0
Trophy Points: 3
Habarini za muda huu ndugu zng,naombeni mwenye uelew na kesi za madai anitafte 0672805811 kuna tajir mmoja kamuweka ndgu yngu lokap toka juzi na hajpelekw mahkamni coz kesi ni ya ktukandmiza na amenymwa zamna

16. Padri Mcharo

Padri Mcharo JF-Expert Member

#16
Feb 16, 2017
Joined: Feb 28, 2015
Messages: 1,360
Likes Received: 1,958
Trophy Points: 280

Blaza unaandika vibaya sana. Hata hamu ya kutoa msaada inakata.

17. D

Dhambi nguo na wew unazo New Member

#17
Feb 16, 2017
Joined: Feb 11, 2017
Messages: 3
Likes Received: 0
Trophy Points: 3
Vbya kvp ndug kama hujaelew acha tyu kwasbabu sjaona nilipoandka ambapo mtu muelew atashndwa kusoma

18. H

Hute JF-Expert Member

#18
Mar 29, 2017
Joined: Nov 25, 2010
Messages: 5,014
Likes Received: 2,298
Trophy Points: 280
anachohitaji hapo ni procedure katika civil, nini kinaanza, nini kinafuata hadi mwisho ili kama hana wakili ajue kinachoendelea pale mahakamani. kama nimemwelewa nafikiri hivyo ndivyo anavyomaanisha.

19. M

Mwana wa Solomon New Member

#19
May 18, 2017
Joined: May 14, 2017
Messages: 1
Likes Received: 1
Trophy Points: 5
DAWA YA DENI NI KULIPA si kutafuta msaada wa kutokulipa
USHAURI:Mwende anayekudai mweleze nia yako ya kulipa na jinsi utakavyolipa lakini unapomwendea nenda angalau na kiasi cha fedha kama robo ya fedha unazodaiwa au kama hazitoshi tafuta mtu atakayesimama na wewe kama mdhamini kumhakikishia mdaiwa jinsi utakavyolipa HIVYO HASIRA YA ANAYEDAI ITAPUNGUA au kutoweka kabisa kwani yote hayo yamesababishwa na wewe.
Kama tukianza kutafuta watu wa kututetea tusilipe madeni matokeo yake UAMINIFU UTATOWEKA na Tutashindwa KUSAIDIANA SISI KWA SISI au tukitaka kusaidiana tutawekeana masharti magumu KUMBUKA BADO SHIDA ZAKO HAZIJAISHA BADO UTAHITAJI TENA MSAADA ambao Hautaupata Tena. Mimi nimeshapeleka kesi zaidi ya ishirini za madai mahakamani na hakuna hata kesi moja mdaiwa alishinda Bali wote walihukumiwa kulipa na wengine walikuwa na mawakili lakini kinachomtia mtu hatiani ni ule mkataba alioingia na Ushaidi wa vielelezo vya kuonyesha mdaiwa amekiuka mkataba na kukataa kulipa deni.

Loading...