Sheria inasemaje katika hili la Mama kutaka kuuza nyumba

kwenda21

JF-Expert Member
Mar 11, 2014
3,419
3,388
Mama anataka kuuza nyumba na aliyojenga na marehemu baba then arudi kijijini ,vipi kuhusu sisi watoto? Wote ni watu wazima je tunachetu hapo? Au hatuna haki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo mnachenu kwasababu nyie ni wanufaika wa Mali za baba yenu. Thamani ya hiyo nyumba mama yenu chake ni robo 1/4, ndugu wa baba ni 1/4 na watoto ni 1/2.

Kama watoto msingekuwepo chake ilikua ni 1/8 na sehemu inayobaki ni ndugu wangechukua.

Kwakuwa watoto ni wakubwa na wanajitegemea inashauriwa wamuachie mama 3/4 na robo wagawane.

Nje ya hapo tutatakiwa kujua msiba wa baba uliishaje yaani kwenye ugawaji wa mirathi nyumba alipewa nani. Kama nyumba alipewa mama kama mrithi halali hamna chenu hapo.

Lakini kama nyumba ilibaki katikati bila mrithi na iliachiwa familia kwa ujumla mgao lazima uwepo na lazima amshirikishe msimamizi wa mirathi katika zoezi hilo.
 
Hapo mnachenu kwasababu nyie ni wanufaika wa Mali za baba yenu. Thamani ya hiyo nyumba mama yenu chake ni robo 1/4, ndugu wa baba ni 1/4 na watoto ni 1/2...
Mkuu nami naomba ufafanuzi kidogo.. Baba mkubwa hakuzaa na kaacha nyumba mbili.. Baba mzazi na Shangazi wamefariki.. Sasa tupo watoto upande wa Baba wakiume wawili kike 2,na upande wa shangazi wa kiume 1 wakike 3
Mgawanyo hapo ukoje?
 
Mkuu nami naomba ufafanuzi kidogo.. Baba mkubwa hakuzaa na kaacha nyumba mbili.. Baba mzazi na Shangazi wamefariki.. Sasa tupo watoto upande wa Baba wakiume wawili kike 2,na upande wa shangazi wa kiume 1 wakike 3
Mgawanyo hapo ukoje?

Hapo wanufaika wa Mali hizo ni ndugu wa marehemu ambao ndio hao baba yako na Shangazi yako. Lakini nyinyi ni watoto hivyo sehemu iliyotakiwa kupewa familia Ndio mnatakiwa mgawane.

Hivyo kisheria ilitakiwa hesabu au thamani za nyumba ipatikane kisha igawanywe lakini kibanadamu nawashauri mdai nyumba moja na nyingine mumuachie mjane ingawa atakuwa amwnufaika pakubwa kuliko uhalisia lakini hamna namna maana hata nyinyi sio wanufaika wa moja kwa moja.

Hiyo nyumba moja Ndio mgawane watoto wa wanufaika. Vile vile ili suala lisiwe gumu sana muwasiliane na huyo mjane ili mlimalize kwa mfumo huo but mngekuwa ni wanufaika wa moja kwa moja ilitakiwa awaachie zote na yeye kupewa hiyo 1/8 ya thamani halisi. Lakini akikataa kutoa ushirikiano basi waoneni wanasheria kwa ufafanuzi zaidi na ghalama ni elfu 60 ya ushauri.
 
Mkuu hapa raha sana, sidhani kama kuna sehemu baba kaandika kuwa mama awe mrithi ila ninachojua ni kwamba wameishi wote mpaka kifo kikamkuta Mzee, na kumuacha mama humo ndani ya nyumba na familia nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu pia kumbuka mama nae akiuza then atugawie watoto chetu akaenda Kujenga yake ili aepuke usumbufu,maana kuna sababu ya kuuza nyumba ni kwamba kuna watoto wanamsumbua, sasa akienda Kujenga nyingine baada ya kuuza ,je watoto waliokwisha pata chao watakuwa na haki tena kwenye nyumba yake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama anataka kuuza nyumba na aliyojenga na marehemu baba then arudi kijijini ,vipi kuhusu sisi watoto,?wote ni watu wazima je tunachetu hapo?au hatuna haki?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mna chenu.

Baba akifariki mnatakiwa kufungua mirathi na warithi ni mama na watoto.

Hapo akiuza lazima awagawie asilimia kadhaa Kila mtoto kwa uwiano sawa, Kama hamtaki habari za mirathi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo mnachenu kwasababu nyie ni wanufaika wa Mali za baba yenu. Thamani ya hiyo nyumba mama yenu chake ni robo 1/4, ndugu wa baba ni 1/4 na watoto ni 1/2.

Kama watoto msingekuwepo chake ilikua ni 1/8 na sehemu inayobaki ni ndugu wangechukua...

Hapana ndugu wa baba hawana haki zaidi ya wazazi wake tu.

Kama Kuna bibina Babu wa kumzaa huyo baba yao ndio wanastahili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila mkuu pia kumbuka mama nae akiuza then atugawie watoto chetu akaenda Kujenga yake ili aepuke usumbufu,maana kuna sababu ya kuuza nyumba ni kwamba kuna watoto wanamsumbua,sasa akienda Kujenga nyingine baada ya kuuza ,je watoto waliokwisha pata chao watakuwa na haki tena kwenye nyumba yake?

Sent using Jamii Forums mobile app

Basi mkae Kama familia mjadili. Muuze mkajenge nyumba nyingine au mgawane halafu kila mti ashike lake, mama akijenga nyumba japo akifariki lazima watoto warithi kwakuwa ni mali ya mama....teh

Hivi watoto mnamsumbuaje mama jamani? Tafuteni zenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nami naomba ufafanuzi kidogo.. Baba mkubwa hakuzaa na kaacha nyumba mbili.. Baba mzazi na Shangazi wamefariki.. Sasa tupo watoto upande wa Baba wakiume wawili kike 2,na upande wa shangazi wa kiume 1 wakike 3
Mgawanyo hapo ukoje?

Kama mama yenu mkubwa yupo basi ndio mwenye haki kwa asilimia mia, Kama Babu na Bibi wapo nao wanahaki.

Ila Kama ma mkubwa hayupo basi nyie watoto na washangazi mna haki sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo wanufaika wa Mali hizo ni ndugu wa marehemu ambao ndio hao baba yako na Shangazi yako. Lakini nyinyi ni watoto hivyo sehemu iliyotakiwa kupewa familia Ndio mnatakiwa mgawane. Hivyo kisheria ilitakiwa hesabu au thamani za nyumba ipatikane kisha igawanywe lakini kibanadamu nawashauri mdai nyumba moja na nyingine mumuachie mjane ingawa atakuwa amwnufaika pakubwa kuliko uhalisia lakini hamna namna maana hata nyinyi sio wanufaika wa moja kwa moja...
Wazazi wote wamefariki.. Baba mkubwa alifariki 2001.Shangaz 2003.Mzee 2013.Mwenyezi Mungu awasamehe makosa yao na awapunzishe mahali pema peponi.

Amiinn, Tulio baki watoto haya maswala baadhi tunataka yakae sawa. Shukrani sana kwa ufafanuzi wako... Mungu akubariki..
 
1. Hamna chenu (hamna haki), isipokuwa kama marehemu aliacha wosia.

2. Mama na (marehemu baba) walikuwa mwili mmoja-waliunganishwa na ndoa, pasipo wosia basi mama ana haki kufanya kwa kadri anavyoweza.

3. Mtoto, kwa mujibu wa sheria ni mwenye miaka 18 kushuka chini.

Naamini umeelewa kidogo uko kwenye nafasi gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom