Sheria inasemaje juu ya wanaume kuvaa mavazi ya kike hasa kwenye sanaa

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,955
3,636
Kuna sanaa za maigizo tunaziona huko mitandao ya kijamii wanaume wakivaa mavazi ya kike nakuigiza uhusika wa wanawake.

Hili limezidi kuenea na sasa kuhamia upande wa television now tunawaona mbele ya familia zetu mbele ya watoto wetu tena huko kwenye tv kimeniuma zaidi.

Kuna joti kiboga wa joti tv,kuna mama imma wa ze comedy dstv na daa zuu kitimtim dstv.

Lalamiko langu ni kuletewa hawa wanaofanya mambo yanafananishwa na USHOGA kwenye television yani nawaza hawa bodi ya sanaa na utamaduni je haya ni katika utamaduni wetu .Kama ni sanaa kuna haja gani kuwekwa mwanaume nafasi ya mwamke wakati naamini kabisa wapo wanawake zaidi wanawaweka kwa kuwavisha madela jamani hii imekaaje.

Lalamiko langu ni hizi television kuachana na sanaa za namna hii wanaume kuvaa mavazi ya kike na kujifananisha na wanawake kwa mwamvuli wa sanaa ya maigizo ya kuchekesha.

Kwakweli Dstv kwa sasa nishaipiga marufuku ndani ya nyumba yangu kuangaliwa THE COMEDY YA MAMA IMMA na KITIMTIM YA DADA ZUU .

Hao wanaoigiza huko mitandao ya kijamii kwenye chanel zao hao nawaachia bodi ya sanaa na utamaduni ila hizi television kutuletea vipindi vyenye maudhui hayo kwakweli wizara husika lisiwachukulie poa nahofia jamii inavyokwenda kuharibiwa kwa mambo hayo kuchukuliwa kawaida kwa mwamvuli wa COMEDY.

images (20).jpeg
images (19).jpeg
images (18).jpeg
 
Back
Top Bottom