Da Asia
JF-Expert Member
- Sep 25, 2011
- 731
- 819
Mwezi wa 11 mwaka jana kijana wangu wa kazi ambaye alidumu kwa siku 6 tu, alivunja ndani kwangu na kuiba vitu vya thamani karibu Tzs mil 30. Lap top, simu za mikononi ambazo nilikua situmii, vitu vya dhahabu na vingine vingi alivyoweza kubeba na kutoroka. Nilitoa taarifa polisi kama kawaida na kupewa RB.
Wakati niko katika mchakato wa kumtoa gazetini, hii ni baada ya juhudi za kumpata kugonga mwamba, kijana alirudi tena baada ya mwezi na nusu, mchana tukiwa kazini na kujifungia kwenye chumba kidogo cha nje ambacho mara nyingi hua hakifungwi. Nitafupisha hadithi kidogo maana ninachotaka ni kujua tu sheria inasemaje.
Nilihisi kuna mtu niliporudi toka kazini mida ya jioni kutokana na harufu tofauti. baadaye usiku wa saa 5 kijana huyo alijitokeza akiwa ameshika kisu na kujifunika uso. nilijua ni yule kijana wangu wa mwanzo maana mtu baki asingeweza kuja bila kujua ramani ya nyumba yangu.
Nilikimbia baada ya kumuona na tulijifungia kwenye chumba kimoja wote tulio ndani na tulianza kupiga kelele za mwizi. Nashukuru sana majirani zangu ambao walikuja kwa wingi sana.
Vilevile nilikua nimeshafunga milango, kijana hakuna na pa kutokea. pamoja na majirani kufika lakini pia tulipiga simu polisi, askari wa doria walifika mapema sana. Sisi tulitolewa dirishani, na mabomu ya machozi yalipigwa ili kumlewesha kijana, baadaye nikawaelekeza askari funguo zilipo wakaingia ndani na kumtoa kijana.
Vha ajabu tukamkuta na simu yangu ambayo niliiacha sitting room wakati na nakimbilia chumbani na shs. 330,000 ambazo aliiba toka kwenye hand bag yangu. Kijana alinusurika kuuwawa na watu wengi waliofurika kwangu vile askari walimuokoa kama ilivyo kawaida. alipelekwa kituo cha polisi na sisi tulifuata kuandika statement.
Kesi ilipelekwa mahakamani, baada ya muda hukumu zikatoka. kesi ya kwanza ya kuvunja na kuiba alihukumiwa miezi 11 na kesi ya pili ya kuvunja na kudhamiria kuiba alifungwa miezi 9. kesi zote mbili zinaenda tofauti.
Naomba kujua sheria inasemaje juu ya mtu aliyevunja na kuiba vitu vya thamani, na kurudi tena kukutishia maisha na kutaka kuiba tena. Sikuridhika na hizi hukumu ndio maana nauliza.Nilitegemea japo afungwe miaka si chini ya mitano lakini kutungwa miezi tu, mtu aliyotolewa ndani kwangu na mabomu ya machozi na askari wakiwa ndio mashahidi wangu haikuniingia akilini.
Msaada wenu tafadhali