Sheria inasemaje baba anapotaka kuchukua mtoto aliyezaa na mwanamke ambae hajaoana nae? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria inasemaje baba anapotaka kuchukua mtoto aliyezaa na mwanamke ambae hajaoana nae?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Upanga, Apr 1, 2011.

 1. U

  Upanga Senior Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Jamani naomba kuuliza,mdogo wangu amezaa na Mwanamke mmoja ambaye hawakuona nae na sasa mtoto ana miaka minane!
  Lakini cha ajabu huyu mtoto anavyozidi kuwa na umri mkubwa huyu dada ndo anavyozidi kuwa m_bishi kumruhusu mtoto kuja hata kumsalimia baba yake.
  Mtoto anahudumiwa kila kitu ikiwa pamoja na kulipiwa over 1m school fees sasa mama hataki hata baba aangalie madaftari ya mtoto.
  Nimemshauri aende kwa wana sheria je kuna ushauri wowote zaidi ya huo niliompa?
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ni vema waelewane na huyo mama aeleze wazi ni kwa nini hataki mtoto amtembelee baba yake. Kuhusu Swaua la kumchukua mtoto nalo linategemea na mambo mengi. Kama mama ana uwezo na baba ana uwezo ni vema wakubaliane matunzo na mtoto aendelee kuishi na mama yake. Akina mama wengi hawataki kabisa watoto wao wakaishi na mama wa kambo, hii inatokana na mahusiano mengi mabaya ambayo mama wengi wa kambo hata watoto wenyewe wameonyesha si mazuri. Kwa mantiki hiyo mwacheni huyo mama akae na mwanae hadi aridhike mwenyewe kumwachia mtoto wake, ila ni vema aweke wazi sababu zinazomzuia mtoto asiwe karibu na baba yake. Angalizo, tujitahidi sana kutozaa kabla ya kuoa/kuolewa, haipendezi watoto kulelewa na parents in separation, lazima migongano inakuwepo. pia watoto wanakosa one way behaviour, ataishia kudokoa order za baba na mama, hivyo utamchanganya mtoto. Poor us.
   
 3. U

  Upanga Senior Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Aksante kwa ushauri wako ila kwa case hii ipo tofauti kidogo maana sababu ya bwana mdogo kumuacha huyo dada ni kwa sababu alimuachia huyo mtoto akiwa na siku nne toka azaliwe na yeye kutimkia ulaya!!
  Hilo lilimuuzi sana bwana mdogo ndo sababu ya kuachana hata hivyo mama mtoto alirudi baada ya miezi minne na akataka mtoto wake ambaye alipewa!
  Huyu mama ni mfanyakazi na anajiweza lakini tunachokiona mapenzi kwa mtoto wake ni kama hakuna mfano mtoto anaweza kaa wiki mbili anavishwa uniform bila kufuliwa,mama hakaguwi vitabu,mara moja alikubali mtoto akae kwa baba na alifanya vizuri sana darasani hadi kushika nafasi ya tatu.
  Lakinni alivyoona hivyo alikuja kumdai haraka akakae nae sasa matokeo yake ktk mid-term exam ya safari hii mtoto amekuwa mtu wa mwisho kabisa darasani.Namuonea huruma sana mtoto na babake alipoulizwa mama yake alitoa jibu moja tuuuu!!!KAFELI SASA MI NIFANYE JE?
  NI HURUMA TUPU
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Mkome kuzaa bila ndoa, hayo ndio baadhi ya maafa yake.
   
 5. U

  Upanga Senior Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  SAWA ieleweke hakuna mtu anayepanga iwe hivyo ila inapotokea basi mtoto asinyanyaswe na nyie kina mama!!!!!!!!!!
   
 6. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Sijui sheria sana ila naangalia ma Boston Legal,
  akijenga hoja anaweza kupata haki mahakamani ya kukaa na mwanae. Wamama wakiwa nazo bwana, fujo tupu.
   
 7. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ITNOJE unamaanisha nini unaposema wamama wakiwa nazo fujo tupu?,, WASIPOKUWA NAZO MNAWAITA TEGEMEZI WAKIJITEGEMEA PIA TATIZO mmh!! binadamu kweli hatuna jema.
  Mama kuwa nazo si tatizo, tatizo la huyo mama ni uzembe alionao ktk kulea mtoto wake. ndiyo maana wanasema SIYO KILA MZAZI NI MLEZI,
  UZAZI NA ULEZI NI VITU VIWILI TOFAUTI,,,ULEZI UNAHITAJI KUJITOA KWA KILA HALI , na ndilo tatizo la huyo mama unayemwita mwenye nazo hana muda wa karibu na mwanaye, mama makin hawezi kuruhusu mwanaye aende shule mchafu.

  Huyu mwanaume ajaribu kuwaona wanasheria ili mtoto aweze kupata suluhisho la tatizo lake ili mtoto apate malezi bora na nadhani BABA ana malezi bora lakin je huyo baba kama kaoa huyo mwanamke mwingine je huyo mwanamke yupo tayari kuishi na mtoto wa nje ya ndoa??? huyu baba yawezekana anamalezi bora kwa mtoto wake lakin bado tatizo likawa kwa mke kama hayupo tayari kulea bado huyo mtoto atapata shida. Afanye juu chini wapate suluhisho la malezi bora ya mtoto wao ili awe na maisha bora , siyo bora maisha...na maisha bora ni yale yenye ELIMU BORA, SIYO BORA ELIMU.
   
 8. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Tafuta wanasheria watapeleka petition mahakamani kuangalia namna ya mzazi kupata haki yake ya kumtembelea baba na kukaa naye. Check na hawa jamaa watakupa usahuri na nini cha kufanya. Email yao ni info@sekaadvocates.co.tz watakupa details na nini cha kufanya. Wameanzisha law firm siku za karibuni tu ila washafanya kazi sehemu mbalimbali.
   
 9. U

  Upanga Senior Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nashukuru Caren nimekwisha waandika hawa jamaa nasubiri majibu yao maana hali inazidi kuwa mbaya,nimemtafuta Mwalimu wa kumpa tuition mtoto kipindi hichi cha likizo lakini huyu dada kakataaa na amempeleka mtoto kwa rafiki yake akaae bila kuwaza kuwa anahitaji msaada wa Elimu.
  Thanks alot kwa wote manaonisaidia kwa huyu mdogo wangu.
   
 10. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145


  mtoto akae na mama yake na kama ni swala la kumuona waweke makubaliano kupitia ustawi wa jamiiii

  ***huwezi kusema eti huyo mama hafai!
   
 11. U

  Upanga Senior Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Thanks MamaD hata mwanzoni alipewa mtoto akae naye pamoja alimuacha wiki moja tuuu baada ya kuzaliwa na yeye kutimkia Ulaya hakuna aliyesema MAMA HAFAI tatizo la sasa hivi jinsi anavyoshindwa kumsaidia mtoto kuanzia malazi,chakula na Elimu pamoja na gharama zote za matunzo anayopewa,hivi wewe mama kweli unafurahi mtoto anakwenda shule mchafu wiki mbili mfululizo?unafurahi mtoto anapokuwa wa mwisho darasni wakati alikuwa ktk top ten?unadiriki kumchukua mtoto akakae kwa rafiki ili amkimbie Mwalimu?
  Pamoja na kusema ni haki yake lakini kwa mtazamo wangu wengine wanatumia vibaya haki hiyo.
   
 12. semango

  semango JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hujasaidia kitu hapa.kaomba ushauri akiwa na maana swala limeshatokea sasa atakomaje tena wakati ameshazaa?
   
 13. semango

  semango JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kwa mtazamo wangu, kama waliweza kukaa na kukubaliana mpaka wakashirikiana na kupata mtoto then sioni kama kuna kikwazo kikubwa kitakacho wafanya washindwe kukaa na kuelewana sasa hivi.mambo ya sheria hapa Tz bado mlolongo wake ni mrefu.pia mara nyingi maamuzi ya kisheria huongeza uhasama kati ya pande mbili zinazolumbana.kwa hiyo silaha kubwa kwa sasa ni makubaliano for the sake of the child.jamaa ajitoe, aweke hasira pembeni na aweke mbele future ya mwanae.
   
 14. H

  Hambaza New Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani hapo cha kuzingatia ni malezi bora kwa mtoto kwanza, bila kujali itikadi pamoja na tofauti baina ya wazazi hao, chuki na uhasama visiathiri welfare ya mtoto huyo. Sio kosa kama mtoto atalelewa na mzazi mmoja!
   
 15. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #15
  Apr 9, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,030
  Likes Received: 7,427
  Trophy Points: 280
  Baada ya maelezo yote hayo bado unakuja na ushauri wa aina hiyo, japo ni maelezo ya upande mmoja lakini kwa kuanzia sikutegemea ungekuja na ushauri wa aina hiyo.
  Elewa kuwa hapa tatizo la msingi na kubwa si baba kumuona mtoto wake bali ni future ya mtoto mwenyewe, au wewe ndiyo mama anaeongelewa hapa????Jaribu kuamka na ieleweke kuwa hatusemi ni jinsia gani baba/mama ya kuishi na mtoto bali ni nani anaestahili hasa kumlea na ndiyo maana zikaletwa reference za matokeo darasani, uangalizi kwa mtoto n.k.
  Tuache kuingiza ushabiki wa kimakundi katika kila jambo
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  Apr 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama hilyo email itafika, b'se hata site yao haiko hewani. Labda awaone physically. Lakini sio kila suala linatatuliwa kwa kuwaona wanasheria. Mambo mengine yanaweza kujadiliwa na watu husika na yakatatuliwa. Mmeongea na ndugu wa pande zote mbili? Wanasemaje? Mmeshamwona mwalimu wa darasa au hata mkuu wa shule, mkamwelezea hilo tatizo? If so, walisemaje? Aliwapa ushauri gani? Kama kuna NGOs zinadeal na child protection aanze nazo kwanza kupata mwongozo. Au akamwone social worker kwenye wilaya yako. sio tuu wanaweza kukupa mwongozo mzuri, bali pia kama wote wakishindwa kutatua tatizo na mkiamua kwenda mahakanini, then mnaweza kuwatumia kama mashahidi wenu.

  Watumie hawa watu ili upate ushahidi na pia mkiamua kwenda mahakamani mnaweza kusema kuwa you have tried to resolve the matter out of court lakini limeshindikana. Tafuta ushahidi kwanza. Mahakamani should be the last resort, not the first resort. Huwa kuna dhana potofu sana; mtu akipatwa na tatizo, cha kwanza ni kwenda kumwona mwanasheria, wakati kuna professionals nyingine ambazo zikao kwenye nafasi nzuri zaidi ya kudeal na tatizo. Mwanasheria anajua where to find the law, not more. But a social worker aliyespecialise kwenye mambo ya child protection will know much better.

  Kama ungekuja kwangu ningekushauri tuu unamwone social worker wako, unless nataka kula pesa yako. kama mdau mmoja alivyosema hapo juu kawaone ustawi wa jamii, b'se kama huyo mwanaseria unayetaka kumwona anata kweli kukusaidia, swali la kwanza atakalo kuuliza ni kama tayari umeshawaona ustawi wa jamii. Nim-quote Semanga hapo juu "pia mara nyingi maamuzi ya kisheria huongeza uhasama kati ya pande mbili zinazolumbana". Zingatia sana hilo bearing mind that there is a child involved.
   
 17. s

  sugi JF-Expert Member

  #17
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  acha kuwa king'ang'anizi,anayemjua baba wa mtoto ni mama!lazima ujiulize n kwa nn anakukatalia!
   
 18. U

  Upanga Senior Member

  #18
  Apr 11, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana kwa Mawazo yote yaliyotolewa!Kuhusu kuwaona Walimu baba yake alikwisha waona na infact aliitwa plae shuleni na kuelezwa hayo yote ambayo yameelezwa zuri zaidi hii ni mara ya pili kwa Walimu kufanya hivyo!Bwana mdogo alikwisha enda hadi USTAWI WA JAMII na kueleza matatizo ya mtoto kwa mama yake yapata miaka miwiliiliyopita na USTAWI walitoa Ushauri ya kuwa mama hana uwezo wa kumzuia mtoto kutoenda kwa baba yake ni suala la makubaliano na mwisho iliamriwa kuwa kwa vile mtoto alikuwa mdogo basi mama akae nae lakini inapofika Ijumaaa mtoto aende kwa baba yake hadi jumapili jioni kisha arudishwe kitu ambacho kilikuwa kinafanyika,ispokuwa toka mtoto aingie darasa la nne Mama amekuwa hataki mtoto aende kwa baba yake na badala yake inapofika Ijumaa huwa anatoa amri arudi kwake na ikifika jioni yeye humchukua na kumpeleka kwa rafiki zake hadi jpili usiku ambako hurudi kwa ajili ya shule jumatatu.
  Tatizo tunaloliona ni maandalizi ya hovyo kimasomo kwa hali ya kawaida shule hizi za ENGLISH MEDIUM kama mtoto hasimamiwi vema zinaonekana kuwa ni ngumu kupita kiasi maana mambo mengine yanayo fundishwa mimi nilisoma nikiwa secondary school.
  HATA HIVYO tunaangalia ushauri wowote tunaopewa kwa makini sana hasa hawa watu wa USTAWI ambao wametoa maagizo ya kuitwa baba na mama tarehe 16th Mwezi huu waangalie jinsi ya kuweka utaratibu sawa.Nawashukuru na tunasubiri Mawazo yenu.
   
 19. L

  Loloo JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mtoto anayezaliwa nje ya ndoa kisheria ni mali ya ukeeni au mama na wajomba usijusumbue kulazimisha mbembeleze mama na akikubali umuhalalishe mtoto kisheria katika mahakama ya wilaya,usijisumbue kupita NGO na kwingineko
   
 20. U

  Upanga Senior Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 135
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Samahani hujaeleweka una maana gani?kuwa ni mali ya ukeeni?na una maanisha nini unaposema ahalalishwe kisheria Mahakamani?
  Mengine yote yalikwisha fanywa kama kujitambulisha kwa hao wajomba na kupewa masharti ya kimila chao kuhusu kutambuliwa kwa baba yake na mtoto sasa unaposema ahalalishwe Mahakamani naomba ufafanue umeniacha mbali.
   
Loading...