Sheria ifanyiwe amendment, wabunge viti maalumu wasiwepo ili kubana matumizi

Dnashon

Member
Feb 19, 2016
58
33
Nimekuwa mfuatiliaji wa bunge kwa muda mrefu, michango ya hoja za wabunge viti maalumu kiukweli nidhahifu sana.Kwani hatuwezi kuwa na bunge dogo lenye wabunge mahiri wa kujenga hoja na kuisimamia serikali?Hawa viti maalumu naona kama mzigo tu, napendekeza sheria ya kuwateuwa ifanyiwe marekebisho, tuwe na bunge la wawakilishi tu.

Nanyi changieni.
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa bunge kwa muda mrefu, michango ya hoja za wabunge viti maarumu kiukweli nidhahifu Sana... Kwani hatuwezi kuwa na bunge dogo lenye wabunge mahili wa kujenga hoja na kuisimamia serikali? Hawa viti maarumu naona kama mzigo Tu, napendekeza sheria ya kuwateuwa ifanyiwe marekebisho, tuwe na bunge la wawakilishi Tu. Nanyi changieni.
Nenda shule ukajifunze tena kuandika.

=Maalum na sio Maarumu

=Ni dhaifu na sio Nidhahifu

=Mahiri na Sio Mahili

=Viti na sio Viiti
 
Hilo linaeleweka na wala hawatuongezei tija na ufanisi ndani ya Bunge. Hata mwenge unaokimbizwa hautusadii kwa Enzi za sasa hivi. Bunge lichukue maamuzi magumu tubane matumizi tuboreshe sekta muhimu kama elimu na afya.
 
Nimekuwa mfuatiliaji wa bunge kwa muda mrefu, michango ya hoja za wabunge viti maalumu kiukweli nidhahifu sana.Kwani hatuwezi kuwa na bunge dogo lenye wabunge mahiri wa kujenga hoja na kuisimamia serikali?Hawa viti maalumu naona kama mzigo tu, napendekeza sheria ya kuwateuwa ifanyiwe marekebisho, tuwe na bunge la wawakilishi tu.

Nanyi changieni.
naunga mkono hoja kwa mantiki ya kubana matumizi ili badala yake mishahara,marupurupu na mafungu yaliyotengwa kwa ajili yao yaelekezwe katika kuanzisha viwanda huduma za umeme vijini pamoja na kuwakomboa watanzania wengi ambao ni masikini kabisa. tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi wanaofaidi nyadhifa hizi ni watoto wa vigogo ama rafiki na jamaa wa karibu wa vigogo wa serekali na chama husika ambao wengi wao tayari wanatoka familia bora na za kitajiri.
 
Back
Top Bottom