Pepombili
JF-Expert Member
- Dec 20, 2010
- 439
- 58
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nasir amesema Sheria ya Kupiga Marufuku Kuingiza Vinywaji vyenye Kilevi katika kisiwa cha Pemba ya mwaka 1928 bado ipo na haijafutwa.
Kamanda Nassir alisema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Waislamu waliokuwa wakitishia kufanya maandamano kupiga kuwepo kwa ghala la kuhifadhi vinywaji vyenye kilevi huko Tibirinzi.
Nassiri alisema sheria hiyo inapiga marufuku watu binafsi kuingiza na kuuza vinywaji hivyo katika kisiwa cha Pemba isipokuwa kwa taasisi za ulinzi tu ikiwemo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika makambi yao.
Sheria ya Kupiga Marufuku Kuingiza Kinywaji chenye Kilevi kisiwani Pemba ipo na haijafutwa . ni marufuku kuingiza kinywaji hicho isipokuwa kwa taasisi za ulinzi tu na kinywaji hicho kipatikane katika kambi za jeshi, alisema.
Aliwataka Waislamu waliokuwa wakitishia kufanya maandamano kuwa watulivu wakati shauri lao hilo likifanyiwa kazi na taaasi husika ikiwemo vyombo vya ulinzi.
Safi sana wananchi wa pemba hakikisheni munalinda na kusimamia hio sheria