Sheria gani inasimamia makosa ya Uharamia?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Siku chache zilizopita kumekuwa na habari ambayo imejaribu kuonesha umahiri mkubwa wa JWTZ kukabiliana na maharamia. Kwamba watu kama nane wanaosadikiwa kuwa ni maharamia walikamatwa walipojaribu kuiteka meli moja kwenye bahari ya Hindi. Watu hao walikamatwa na baadaye kupelekwa kikosi cha jeshi na sasa imeripotiwa kuwa wanapelekwa Polisi.

Najiuliza kama kuna sheria yoyote ya kusimamia Uharamia (Anti-Piracy in the High Seas) Tanzania. Isije kuwa tunajaribu kuita kosa kitu ambacho si kosa kisheria! Kama kuna sheria inayosimamia haya ni ipi nimejitahidi kutafuta lakini sijaona bado.
 
Hata mimi nilijaribu kujiuliza hasa baada ya hao jamaa kukabidhiwa kwa jeshi la polisi. Nilihofu wasije kupelekwa mahakamani halafu tukasikia mahakama imetupilia mbali au hakuna kesi ya kujibu!!? Ngoja tuwasubiri wanasheria.
 
Watawapeleka Marekani kwenye sheria hiyo hahaha ahahahaha ahahahah!!!!!!!
 
Basi tuseme hata kuteka ndege Tanzania si kosa kwa vile hakuna sheria ya Anti-Hijacking in the High Skies!!!!

Nina uhakika mkubwa unaamini kabisa moyoni mwako kuwa umesema kitu ambacho kina mantiki kweli. Well hakuna sheria ya Anti-Hijacking in the High Skies!
 
MMM, sina interest wala utaalam wa sheria kutokana na bias niliyonayo kwa hiyo taasisi nchini kwetu... but all i can say ni kwamba hao jamaa watapotezewa kwani mzunguko wao wa pesa unaneemesha hadi "vigogo" hapo mujini
 
Mkuu Mwanakijiji nasikitika tu kwamba hawa jamaa wataachiwa kwani maharamia ndo wenye hotel kubwa Bagamoyo, Dar na Morogoro. Kwa hiyo sioni mtu wa kuwafunga hata kama sheria ipo, Tanzania ya mwalimu siyo hii ya sasa.
 
Maritime piracy, according to the United Nations Convention on the Law of the Sea (UNCLOS) of 1982, consists of any criminal acts of violence, detention, rape, or depredation committed for private ends by the crew or the passengers of a private ship or aircraft that is directed on the high seas against another ship, aircraft, or against persons or property on board a ship or aircraft. Piracy can also be committed against a ship, aircraft, persons, or property in a place outside the jurisdiction of any state, and in fact piracy has been the first example of universal jurisdiction. Nevertheless today the international community is facing many problems in bringing pirates to justice.

We are the UN.
 
Siku chache zilizopita kumekuwa na habari ambayo imejaribu kuonesha umahiri mkubwa wa JWTZ kukabiliana na maharamia. Kwamba watu kama nane wanaosadikiwa kuwa ni maharamia walikamatwa walipojaribu kuiteka meli moja kwenye bahari ya Hindi. Watu hao walikamatwa na baadaye kupelekwa kikosi cha jeshi na sasa imeripotiwa kuwa wanapelekwa Polisi.

Najiuliza kama kuna sheria yoyote ya kusimamia Uharamia (Anti-Piracy in the High Seas) Tanzania. Isije kuwa tunajaribu kuita kosa kitu ambacho si kosa kisheria! Kama kuna sheria inayosimamia haya ni ipi nimejitahidi kutafuta lakini sijaona bado.

Kama hakuna sheria hiyo, basi tunawashitaki kwa kosa la uvamizi (ujambazi) kwa kutumia silaha, na hapo kila mmoja anakula mvua 30! Au haiwezekani?!manake ni kweli, wakikurupuka kuwa makini wa kuandaaa mashitaka, basi hakuna shaka kabisa wanaweza wasipatikane na kosa la kujibu!
 
... kuwa umesema kitu ambacho kina mantiki kweli. Well hakuna sheria ya Anti-Hijacking in the High Skies!
Well, kama hakuna sheria ya Anti-Hijacking in the High Skies, je kuteka ndege angani Tanzania ni kosa?

Halafu tutarudi kwenye swala la shauku yako ya kutaka tuwe na sheria ya "Anti-Piracy in the High Seas"....ha ha ha hahaaaa.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom