Elections 2010 Sheria gani iliyompa madaraka Kilavu kuzuia watu wasipige kura ?

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
966
536
kama mnakumbuka vizuri Kilavu alizuia watu wote waliokuwa mbali na vituo walivyojiandikishia kupiga kura mahali walipokuwepo. Ukiangalia vipengele vya katiba, sababu zilizotajwa, aliyoitoa Kiravu haipo!

Haki ya kupiga kura Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 2000 Na.3 ib.4​
5​
.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.

(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo-
(a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;
(b) kuwa na ugonjwa wa akili;
(c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;
(d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kamampiga kura,
mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyote inayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.

Kilavu sababu yake aliitoa wapi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom