Sheria duniani haki mbinguni- kufutwa kwa hati ya kukamatwa maaskofu

Madikizela

JF-Expert Member
Jul 4, 2009
643
403
Suala la kufutwa kwa hati ya kukamatwa Askofu Mokiwa lina mambo mengi ndani yake yenye kutia shaka juu ya uwezo wa MAJAJI wetu kuisimamia sheria na pia siasa kuingilia uhuru wa mahakama kwani angekuwa ni mlalahoi mwingine asingewezaza kufutiwa hati hiyo hata kama hakukosa kisheria

Hebu someni hapo chini halafu tujadili:-

MAHAKAMA ya Rufani imetengua amri ya kukamatwa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa na Askofu Stanley Hotay iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Mkuu Mohamed Chande akisaidiwa na Jaji William Mandia na Jaji Steven Bwana kwa kuwa Mahakama Kuu ilikiuka kanuni.

Juni 13, mwaka huu, Jaji Kakusulo Sambo wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alitoa amri ya kukamatwa maaskofu hao kwa madai ya kukiuka amri ya Mahakama; hali iliyowalazimu mawakili wao Joseph Thadayo na Albert Msando kuwasilisha ombi Mahakama ya Rufani wakiiomba ifanye mapitio ya uamuzi huo.

Katika uamuzi huo, Mahakama ya Rufani ilisema kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza uendeshaji wa mashauri ya jinai, Jaji huyo alipaswa kwanza kutoa uamuzi wa mapingamizi hayo, lakini badala yake, aliacha na kurukia mambo ambayo hayakuwepo mahakamani.

Ilieleza kuwa, hata ombi lililowasilishwa na wakili wa walalamikaji katika kesi ya msingi, kukamatwa kwa maaskofu hao lilikiuka kanuni kwa kuwa wakili huyo alipaswa awasilishe ombi rasmi ili upande wa pili nao uweze kupata nafasi ya kujibu.

Mahakama hiyo ilidai kuwa katika kumbukumbu za kesi za msingi walalamikiwa ni Bodi ya Wadhamini wa Kanisa hilo la Anglikana Tanzania na Mchungaji Hotay, lakini hakuna mahali panapoonesha kuwa Askofu Mokiwa ni mmoja wa wadhamini wa kanisa hilo.

Kwa uamuzi huo, Mahakama ya Rufani imefuta mwenendo wote uliosababisha kutolewa kwa amri ya kukamatwa kwa maaskofu hao na kumwamuru Jaji Sambo kutoa uamuzi wa mapingamizi aliouahirisha siku hiyo.

Maaskofu hao walidaiwa kukiuka amri ya Mahakama hiyo iliyositisha shughuli za kumsimika Askofu Hotay kuwa Askofu wa Anglikana wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.

source: Habari leo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom