Sheria 13 za mpira wakati tukiwa watoto

Dana dana kuhesabihana, iwe ya mguu mmoja au iwe ya miguu miwili.

Kontroo, Vichwa, Tobo bao.

Mtu kati (unasafa), hapa zipo za aina mbili. Kuna ile moja ukigusa tu Mpira kwa yule aliekuwa nao, ujue hapo umejikomboa na yeye inakuwa zamu yake kusafa.

Na kuna ile nyingine lazima unyang'anye Mpira ndio ujikomboe na yule uliemnyang'anya inakuwa zamu yake kusafa.

Hapa kwenye kusafa panakuwaga patamu, pale inapotokea mmoja wenu kusafa kwa muda mrefu, mpaka anaesafa anakasirika.

Kabla ya kuanza napenda zaidi pale mnapoanza kuweka uamuzi kusafa kwa aina gani, Kugusa au kunyang'anya.

Maisha haya.

Eti sasa hivi na mie HARUFU naitwa Baba.

Jamani
Ukisafa mpk mwisho ujue umelala nacho na wimbo unaimbiwa.
 
Kweli kabisa yani kwa wasichana siku hizi hata rede,makida na mdako ni nadra sana kukuta wakicheza..utandawazi pia umetuathiri tunajenga nyumba ndani tiles nje vitofali vile chini hatubakizi ata kasehemu ka mchanga na udongo mtoto ata achimbe shimo la mdako na vishimo vya bao au achore kipande aruke aruke mtoto siku hizi akishika tu udongo mzazi anafoka minyoo akienda kucheza rede anaambiwa chokoraa...nitoe wito kwa wazazi watoto ni michezo ukiruka stage za mchezo utotoni matokeo yake ukikua sasa unaanza kuruka ruka kama mtoto
Hapo kwenye Mdako umenikumbusha mbali.

Mie mwenyewe nilikuwa najichanganya kwenye Mdako.

Tunachora Duara Kibarazani na Chaki ya kokoto.

Kokoto zinakuwa kumi na mbili (12), na Ndimu inakuwa inarushwa juu na kuidaka huku ukizitoa kokoto nje ya Dimba na kuziingiza.

Nakumbuka, unatoa kwa kiganja kimoja zote kumi na mbili (12) kwanza nje ya Dimba, huku Ndimu ikiwa hewani kisha unarudisha ndani kumi na moja (11). Moja unaishika na mkono mwingine ambao haurushi Ndimu.

Kisha na unatoa tena nje ya Dimba kumi na moja (11), unarudisha ndani kumi (10) huku Ndimu ikiwa hewani. Nyingine unaishika na mkono mwingine ambao haurushi Ndimu. Jumla hapo zinakuwa mbili nje.

Unaendelea, unatoa tena nje ya Dimba kumi (10), unarudisha ndani tisa (9) huku Ndimu ikiwa hewani. Jumla hapo zinakuwa tatu nje.

Unaendelea na zoezi hilo mpaka unamaliza zote kumi na mbili (12). Kisha unaziingiza ndani zote kumi na mbili (12) na kuzitoa tena nje zote kumi na mbili (12) kwa mkupuo.

Mimi HARUFU natisha sana kwa Mdako, nna hakika hata sasa hivi ukiomba Mechi na mie lazima nikugalagaze.

Jamani
 
Vingne;
Faulo ya kwanza haikingwi

Faulo ya pili inakingwa na ukingwaji wake sasa mpira unakaa katikati ya miguu ya mkingaji

Kujifunga vitambaa,kamba kichwani ili uonekane noma..

Mkiwa wengi mnagawa timu zinakua tatu atakae fungwa anatoka..

Wengne tulikua na wazazi wakali ukitoka kucheza umepauka miguu unajipaka mate ili uonekane hujachafuka

Mara nyingi mechi ilkua inaanza saa kumi

Mchezaji mkubwa kuliko wote mara nyingi alkua anadaka

Lakini watoto wa siku hizi wamekalia singeli
 
Nakumbuka wakati wa kuchagua team mnajipanga mstari mmoja mrefuu halafu yule mbabe ndio anasimamia zoezi la waliojipanga,mmoja anarudi nyuma na anayefuatia anapiga hatua mbele,ilikua mmoja anasogea mbele anayefuata anarudi nyuma mpaka zinapatikana team mbili,team ya waliorudi nyuma na waliopiga hatua mbele!!
Hyo kwetu inaitwa toka ingia hapo kama marafiki na mnapenda mcheze timu moja mnatafta mtu mnamuweka katikati yenu
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Kweli kabisa yani kwa wasichana siku hizi hata rede,makida na mdako ni nadra sana kukuta wakicheza..utandawazi pia umetuathiri tunajenga nyumba ndani tiles nje vitofali vile chini hatubakizi ata kasehemu ka mchanga na udongo mtoto ata achimbe shimo la mdako na vishimo vya bao au achore kipande aruke aruke mtoto siku hizi akishika tu udongo mzazi anafoka minyoo akienda kucheza rede anaambiwa chokoraa...nitoe wito kwa wazazi watoto ni michezo ukiruka stage za mchezo utotoni matokeo yake ukikua sasa unaanza kuruka ruka kama mtoto
Mimi hata REDE nilikuwa najichanganya pia.

Wanachukua Soksi wanazifiringisha inakuwa kama Kajimpira, wawili kazi yao kurushiana Kajimpira kumlenga aliekuwa kati.

Aliekuwa kati kazi yake kukwepa.

Mara utasikia "HARUFU nimekubabua" najibu, jamani hamjanibabua. Wanaendelea tena "HARUFU mlalamishi umebabuliwa toka nje" mimi naendelea kukomaa, jamani hamjanibabua, Vilimbwende vinaanza kusema "HARUFU hii mara ya mwisho ukibabuliwa unatoka" nawaambia sawa.

Mchezo unaendelea, mara tena "HARUFU umebabuliwa", nakomaa tena, jamani hamjanibabua , Vilimbwende vinaanza kelele kwa pamoja "hatutaki, HARUFU toka, wewe Mzurumishi" wanapiga kelele mpaka nakuwa matawi ya chini, inabidi nitoke niwapishe wengine.

Utoto raha sana.

Jamani
 
Kuna watu ambao ilikuwa ukipigana nao Bambi lazima mguu uvimbe.
Nakumbuka nilijikata Mguuni (Nyayoni), na kwa jinsi nlivyokuwa naupenda Mpira nilikuwa nakosa raha sana.

Sikudanganyi, mpaka MAZA aligundua kuna kitu nakikosa, sababu anajua fika mimi napenda sana Mpira wa Miguu. Ikafika mpaka kunipeleka sehemu tofauti tofauti zenye starehe za Watoto, mara kwa mara, mtu mbili tu mimi na yeye, lakini mimi amani haikuwemo kabisa. Nawaza kupona ili niendelee na Mpira.

Kisa cha kuumia.

Tulikuwa kwenye Mechi za Kitoto, Mpira ukatoka ukaangukia Jalalani. Mimi si ndio nimeenda kuUkota Mpira ili niurushe, nakwambia balaa,

Pale Jalalani kumbe kulikuwa na kipande cha Chupa iliyovunjika, mimi nilipoenda okota Mpira ili nirushe si ndio kwa bahati mbaya nikakikanyaga kipande cha Chupa, ebwana zilitoka Damu nyingi sana. Na mechi ikaishia hapo hapo ikabidi mimi nipelekwe Hospitali.

Ila huwezi amini Nyayoni hivi sasa sina alama, mkato wa Chupa wote umefutika
 
Screenshot_2016-12-22-07-55-18.jpg
Mechi kati ya waliovaa mashati Vs waliovua mashati.
 
Wengine wamefurahishwa na huu uzi.Lakn mi nimeumia san.Nimekumbuka maisha ambayo hayatarudi had naingia kaburini
Mkuu usiumie sana,furahia maisha kwa wakati ulio nao coz hata huu wakati ulionao sasa pia utaujutia au utaukumbuka baada ya miaka 10 au 20 ijayo,

Sometimes you will never know the value of a moment until it becomes a memory.
 
Nakumbuka siku moja nilipewa dakika chache za kucheza halafu nitoke nimpishe mwingine, sasa sinikafunga goli ebwanae nikaambiwa hakuna kutoka mpaka mpira uishe. Hahahaha
 
SHERIA 15 ZA MPIRA ZA KIPINDI CHA UTOTONI
1. Mkubwa Hachezi Na Akicheza Mnaingia Wawili.
2.Mwenye Mpira Hatolewi Hata Akicheza Vibaya.
3.Inaruhusiwa Kubadili Kipa Kama Penati Imetokea Na Baada Ya Penati Anaruhusiwa Kurudi Wa Mwanzo.
4.Yule Mtaalam Wa Soka Hakosi Namba Hata Siku Moja.
5. Dogo Mnene Lazima Awe Golikipa.
6.Mwenye Mpira Ataamua Nani Asicheze.
7.Penati Itatokea Tu Pale Mchezaji Akiumia Sana Na Kutoka Damu.
8.Mechi Itaisha Kama Kila Mchezaji Atakuwa Amechoka.
9. Hakuna Free Kick,refa Wala Offside.
10. Ukichaguliwa Mwishoni Ujue Uwezo Wako Mdogo Kuliko Wote Uwanjani.
11.Mtaalam Wa Timu Akipewa Kazi Na Wazazi Wake Lazima Mumsaidie Ndo Mwende Kucheza.
12.Ukiumia Kidonda Kinawekwa Mchanga.
13.Kipa Anaruhusiwa Kudaka Popote.
14. Wale Ambao Wamekosa Namba Kazi Yao Ni Kufata Mipira Ikitoka.
15. Mwenye Mpira Akikasirika Mechi Ndo Inakuwa Imeisha

Vizazi vya science na technologia hawajui haya kabisa, kweli tuliyaenjoy maisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom