BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,887
Waungwana,
Kama mtakumbuka wiki chache zilizopita mwenzetu mmoja wa Sweden (kama sikosei) aliandika hapa kuonyesha kushangazwa kwake na sherehe ya Muungano ya 2008 ambayo ubalozi wa Tanzania Sweden ulitangaza itafanyika na hivyo kuwaalika Watanzania toka miji mbali mbali ya Sweden na nchi za jirani. Mwenzetu huyo alidai kwamba alishangazwa baada ya balozi kutotokea kwenye sherehe hizo na hata hakukuwa na ofisa yeyote toka ubalozini. Ninachofahamu ni kwamba balozi zetu zinapewa fungu maalum ili kufanyia sherehe za Muungano.
Je, inawezekana hizi sherehe zinatumika kufanya ufisadi? Hapa kuna uwezekano ubalozi haukutumia hata senti tano, lakini labda huko mambo ya nje inapelekwa bill kwamba walialikwa Watanzania 300 na zilitumika kiasi kadhaa kugharamia sherehe hizo.