Sherehe za uhuru wa zanzibar 10 december 1963 zafanyika scandinavia leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sherehe za uhuru wa zanzibar 10 december 1963 zafanyika scandinavia leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fatal5, Dec 12, 2011.

 1. Fatal5

  Fatal5 Senior Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Zanzibar

  [​IMG]

  Wazanzibari kutoka sehemu mbalimbali za Skandinavia walikutana jana kusherehekea kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Zanzibar wa tarehe 10 Disemba 1963. Sherehe hizo zilifanyika katika mgahawa maarufu mjini Copenhagen ujulikanao kama Ankara Restaurant. Mbali ya wazawa wa Zanzibar, walihudhuria pia wageni mbalimbali kutoka Uingereza, Poland, Uturuki na sehemu nyingine duniani kuunga mkono hafla hiyo.
  Katika maadhimisho hayo, mwandishi na mtafiti wa siasa za Tanzania Ludovick Mwijage alipata nafasi ya kuhutubia hadhara hiyo kwa kuwaunga mkono Wazanzibari juu ya uamuzi wao wa kusherehekea siku hii adhimu. Pamoja na mambo mengine, Mwijage amewashajiisha Wazanzibari kuendelea kuikumbuka siku hii kwani ni siku muhimu sana katika historia ya visiwa vya Zanzibar.
  Kamati ya maandalizi ya sherehe za kumbukumbu ya siku ya Uhuru wa Zanzibar inapenda kuwashukuru wote waliohudhuria katika hafla hiyo pamoja na wale waliochangia kwa hali na/au mali kufanikisha siku hii.
  Kamati maalum,
  11 Disemba 2011
  Copenhagen
   
Loading...