Sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara(Tanganyika): Babu Seya na Wafungwa wengine 8,157 Wasamehewa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,566
2,000
Ndugu Watanzania,

Leo, Disemba 09, 2017 Tanzania inaadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika?).

- Sherehe za kumbukumbu hizi zinafanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

- Sherehe hizi zinaadhimishwa huku kukiwa na simanzi kitaifa kufuatia askari wetu wanaolinda amani DRC kuuawa na wengine kujeruhiwa vibaya kufuatia shambulizi lililofanywa na waasi.
Rais anaanza kuhutubia;

Rais Magufuli: Kabla sijazungumza lolote ningewaomba tusimame tuwaombee wenzetu maaskari wetu mashujaa ambao wameuawa kule DRC mpaka sasa 14 wamepoteza maisha, 44 wamejeruhiwa ambapo 8 wapo mahututi na 2 hawajapatikana.

Siku kama ya leo Desemba 9 1961. Jamhuri ya Tanganyika ilipata uhuru.
Kama mnavyojua harakati za ukombozi ziliasisiwa na TANU.
Uhuru wetu uliletwa na TANU na ASP na hilo haliwezi kubadilika.
Tunawakumbuka wazee wetu 17 ambao walipigania ukombozi wa nchi yetu.

Toka uhuru wa nchi yetu tumepata mafanikio makubwa sana.
Naomba nitoe mifano michache.

Nchi yetu wakati tunapata uhuru ilikuwa na barabara zenye urefu wa km33,600 ambapo km1360 zilikuwa na lami. Leo hii tuna barabara zenye urefu wa km 122,500 ambapo km12,679 na km2480 ujenzi unaendelea na km7,087 zipo kwenye hatua mbalimbali za maandalizi. Madaraja makubwa zaidi ya 17 yamejengwa.

Tulipopata uhuru kulikuwa na vituo vya afya 1,095 leo tuna vituo vya afya 7,293

Tulipopata uhuru tulikuwa na shule za msingi 3100 leo tuna shule za msingi 17,379

Tulipokuwa tunapata uhuru shule za sekondari zilikuwa 41, leo shule za sekondari ni 4817

Wakati tunapata uhuru tulikuwa na chuo kikuu 1, leo tuna vyuo vikuu 48

Wakati tunapata uhuru tulikuwa na madaktari 408; watanganyika walikuwa 12, leo tuna madaktari 9,343.

Tulipopata uhuru tulikuwa na wahandisi 12, leo tuna wanandisi 19,164 waliosajiliwa

Tulipopata uhuru tulikuwa na makandarasi 2 leo tuna wakandarasi 9,350 waliosajiliwa

Tulipopata uhuru tulikuwa na wastani wa umri wa kuishi ulikuwa miaka 37, leo wastani wa umri wa kuishi ni maika 61

Tulipopata uhuru tulikuwa na watu milioni 9 na milioni, leo tuna watu milioni 52.

Hata Dodoma haikuwa hivi wakati tunapata uhuru.Mifano ni mingi mno

Maendeleo yamepataikana kwenye maji, uchumi, usalama,mifugo, madini, diplomasia za kimataifa, demokrasia vita vya rushwa n.k

Tumeendelea kulinda uhuru wetu pamoja na muungano wetu.
Hongereni sana watanzania kwa miaka 56 ya uhuru.

Ninapenda kuwapongeza wazee wetu. Ninafurahi kuona wazee wetu Mwinyi, Mkapa, Kiwete na Bilal na mimi afurahi siku moja niwe mstaafu.

Napenda kuwapongeza wote waliotoa mchango wao kwa kutoa mchango uliowezesha kufanikisha mafaniko yote niliyotaja.

Aidha navishukuru vyombo vya ulinzi kwa kufanikisha maendeleo haya.

Sherehe za uhuru mwaka huu zinafanyika hapa Dodoma na yataendelea kufanyika hapa Dodoma.

Tutaendelea kutekeleza ahadi tulizoahidi na kwatumikia watanzania bila kubagua watu kwa dini zao, makabila au vyama vyao.

Napenda kutekeleza ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Kutokana na haya Tanzania tuna wafungwa 39,000 mpaka jana; 37,000 wanaume na 2000 wanawake.

Waliohukumiwa kunyongwa ni 522; 503 ni wanaume na 19 ni wanawake.

Waliofungwa maisha 666; 655 wanaume na 11 wanawake

Kwa mujibu wa ibara hii ya 45 na hasa kwa kuzingatia kuwa sisi ni binadamu. Nimeamua kuwasamehe wafungwa 8,157 ambapo wafungwa 1,828 watatoka leo na 6,329 wamepunguziwa muda wa kukaa gerezani na watatoka kwa mujibu wa vifungo vyao.

Lakini pia kwa mujibu wa ibara hiyohiyo ya 45, wapo waliohukumiwa kunyongwa; wapo wenye umri zaidi ya miaka 85.

Wapo wafungwa ambao wametubu kweli dhambi zao.

Ndugu zangu baada ya kukaa na kufikiria na kwa sababu sisi wanadamu kila siku huwa tunaomba kusamehewa.

Nimeguswa ndugu zangu watanzania na hasa ukiangalia hawa waliofikisha mpaka miaka 85 ni wazee.

Nimepata taarifa magerezani.

Nimewasamehe wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa. Wahusika wafanye process ya kuwatoa leo au kesho.

Yupo mzee mmoja anaitwa Mganga Matonya ana miaka 85 na amekaa gerezani miaka 37, na mahabusu miaka 7.

Ninaomba orodha hii nitamkabidhi waziri mkuu awashughulikie.

Kutokana na hiyo ibara ya 45 familia ya Nguza Viking jina lingine anaitwa Babu Sea na mwanaye ndugu Jonson Nguza 'Papii Kocha' nao waachiwe huru.


Nimeeleza mambo mengi sana na naomba niishie hapa lakini naomba nitoe hongera sana kwa wanakamati kwani sherehere zimefana sana.

Navishukuru sana vyombo vya ulinzi, mabalozi na nawahakikishia ushirikiano na nchi zenu.
Nawashukuru wana Dodoma

Mheshimiwa makamu wa Rais yupo kwenye hatua za mwisho kuhamia Dodoma na mimi mwaka kesho nitahamia Dodoma.

Baada ya kusema hayo, niwashukuru sana maraisi wastaafu na viongozi wastaafu.

Niwashukuru sana; Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania wote.
Asanteni sana
 

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
15,828
2,000
Napenda hizi sherehe ziwe zinajitofautisha na mambo ya siasa na vyama.

Jana nimesikitika sana kuona kampeni ya uzalendo ikigubikwa na uchama.

We have a long way, very long way to go and it is likely we will never get there.
Ndiyo maana ni ngumu kuhubiri uzalendo.Maana ukichanganya tu na uvyama basi tena maana ya sherehe Za kitaifa zinapoteza maana yake Na watu kuanza kuziona kama sherehe Za kichama tu.
 

Sharif

JF-Expert Member
Mar 13, 2011
2,471
2,000
Mnafanya sherehe wakati ndugu zetu wameuwawa Congo..
si vibaya sherehe hizi zingeahirishwa kwa heshima ya wanajeshi waliouawa.
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,322
2,000
Mnafanya sherehe wakati ndugu zetu wameuwawa Congo..
si vibaya sherehe hizi zingeahirishwa kwa heshima ya wanajeshi waliouawa.
Wanajeshi wengine wapelekwe DRC tukalipe kisasi kwa ADF wameua askari wetu wengi sana roho inaniuma
Nitashangaa sana kama makomandoo wa kuvunja matofari kifuani nao watakuwepo uwanjani.
 

Kodjoe Borris

Member
Jan 15, 2017
95
125
Kwa kweli kati ya mambo yanayokera sana ni hili la wafuasi wa chama tawala kuvaa sare za chama chao katika shughuli mbalimbali za kitaifa amabazo kimsingi si za kiitikadi kwa kisingizio cha kuwa wao ndio chama dola hakika si sawa kwani suala la wao kuwa chama dola linfahamika na linapokuja suala la kitaifa umoja usio na itikadi ni jambo la msingi zaidi kuliko kuleta viashiria vya kichama.
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,633
2,000
Mliopo kwenye hiyo sherehe mwambieni Raisi kuwa wananchi tumepatwa na hasira baada ya wanajeshi wetu kushambuliwa kule DRC na waasi ambao inajulikana wafadhili wake ni akina nani (Ngongoti PK, na M7)
 

Muyobhyo

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
8,162
2,000
Kwa kweli kati ya mambo yanayokera sana ni hili la wafuasi wa chama tawala kuvaa sare za chama chao katika shughuli mbalimbali za kitaifa amabazo kimsingi si za kiitikadi kwa kisingizio cha kuwa wao ndio chama dola hakika si sawa kwani suala la wao kuwa chama dola linfahamika na linapokuja suala la kitaifa umoja usio na itikadi ni jambo la msingi zaidi kuliko kuleta viashiria vya kichama.
Nilishasema kitambo kuwa nchi sasa iitwe nchi ya ccm, isiitwe tanzania, tunaomba nchi hii itambulike ni nchi ya ccm tuvae kijani mwanzo mwisho
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom