Sherehe za TANU: Rais Kikwete akutana na mabalozi wa nyumba kumi na viongozi wa mashina na kata

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
* It is fascinationg the ruling party for the case of it being valuable and respected they go back to embrace TANU and trying to Correct their Meany Demenor by Embracing Tanu the Party which was run perfectly Under Nyerere and Rashid Mfaume Kawawa with Moses Nnauye as Katibu Mwenezi!!! Do U see the PIC?

The Party in Power has power of Using Artists; Government Places such as Mnazi Mmoja, POWER Management and POSHO

If people behaved like governments, you'd call the cops as you see all members of ruling Party in this celebrations.

Politicians are like diapers. They both need changing regularly and for the same reason... BUT CCM POLITICIANS are there for LIFE.
H.JPG


Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa nyumba kumi na viongozi wa mashina na matawi ya CCM katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam, mchana, ubungo Plaza ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa TANU na madhimisho ya miaka 50 ya Uhuru.

C.JPG


Kikwete akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa Wilson Mukama baada ya kuingia ukumbini
A.JPG



Viongozi wa nyumba kumi na viongozi wa mashina na matawi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.

D.JPG


Wakimshangilia Kikwete

E.JPG



Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihamasisha mkutano huo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama
F.JPG



Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akizungumza akwenye mkutano huo


G.JPG



Mmwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete, Msekwa na Mukama wakimfurahia mmoja wa waasisi wa TANU kati ya watatu walio hai, Costantine Milinga (90) alipokuwa akieleza alivyoshiriki kuanzisha chama hicho.


I.JPG



Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru naye akapata fursa kueleza alivyojiunga na TANU


CCM YATUMIA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU KUKUMBUKA KUZALIWA KWA TANU




1.JPG



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais, Jakaya Kikwete alipowaili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, katika sherehe ya mkesha wa kuzaliwa kwa TANU. Kulia ni Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abdulrahman Kinana.


2.JPG



Wana-CCM wakiserebuka nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba wakati wa mkesha huo wa kuzaliwa kwa TANU usiku wa kuamkia leo.


3.JPG



Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiliza king'ora kuashiria kuzaliwa kwa TANU, kwenye Ofisi Ndogo ya makao makuu ya CCM Lulumba. Shughuli hiyo ilifanyika katika jengo ilimozaliwa TANU 7/7/1954


4.JPG



Kikwete na mkewe, Mama Salma Kikwete wakiondoka Lulumba, kwenda viwanja vya Mnazi Mmoja kuendelea na mkesha wa kuzaliwa TANU


5.JPG



Rais Kikwete akimsalimia Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, aliposalimia wana-CCM mbalimbali kabla ya kuondoka Lumumba


6.JPG



Wananchi waliofurika viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye sherehe hizo


7.JPG



Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akiwa na Makamu wake, Pius Msekwa, Katibu Mkuu Wilson Mukama na mkewe Mama Kikwete baada ya kuwasili viwanja vya Mnazi Mmoja. Kushoto ni, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Wapili kushoto Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita na kulia ni mlezi wa CCM mkoa huo, Abdulrahman Kinana.


8.JPG



Kikwete, Msekwa na Mukama wakijadili jambo wakati wa sherehe hiyo



Mamia ya wana-CCM na wananchi kwa jumla waliohudhuria sherehe hizo.


10.JPG



Mamia ya watu upande wa lango la kuingia viwanja vya Mnazi Mmoja


11.JPG



Burudani zilikuwepo, Marlow akitumbuiza


12.JPG

Halafu Ze Top In Town au TID naye akafanya mavituz yake kama hivi

Nape akaona haitoshi, akapanda jukwaani na kucharaza gita zito la bass, kuwapa tafu Vijana jazz
14.JPG

Kisha akazikung'uta tumba

Mama Salma Kikwete akamkubali kuwa kweli Nape ni mwanamuziki mahiri, akaenda kumtuza nteze kibao
16.JPG

Baada ya burudani, Kikwete akiambatana na muasisi wa mstari wa mbele wa TANU kati ya wawili waliopo hai Costantine Milinga, kwenda kuliza king'ora ilipotimu saa sita kamili usiku wa kuamkia leo

Rais Kikwete na Mzee Milinga wakishirikiana kubonyesha king'ora hicho
18.JPG

Wakati akiendelea kubonyeza king'ora, mafataki nayo yalikuwa yaiendelea kuunguruma huku watu wakishangilia. Kushoto ni Nape, Mama Kikwete, Msekwa, Mukama na kulia ni Kinana wakishangilia



Baadhi ya fataki zilizorindima Mnazi mmoja

Nape na JK wakifurahia tukio hilo
21.JPG

Kikwete akizungumza jambo na Nape, Guninita na Msekwa
22.JPG



Kapteni Komba akiongoza kundi la TOT kuimba wimbo maalum wa kupongeza miaka 57 ya TANU

23.JPG


Rais Kikwete akaanza kuondoka uwanjani kwa kusalimia wadau na viongozi mbalimbali, hapa anamwaga Katibu wa UVCCM, Martine Shigella. Kushoto ni Mama Kikwete


24.JPG



Akamuaga Nape



Akawaaga wadau mbalimbali kama hivi


26.JPG


JK akiondoka akisindikizwa na Msekwa, Mukama na
na vion
gozi wengine

27.JPG


Nape akatumia fursa hiyo kuzungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kwa nyakati tofauti baada ya Mwenyekiti, Rais Kikwete kuondoka. Hapa anazungumza na watangazaji wa Uhuru FM
 
duh watz hatuna vipaumbele , mnafanya birthday ya babu aliyeshafariki , mnatumia fedha nyingi kwa tukio lisilo na manufaa wananchi wanaokufa kwa kukosa huduma za afya, ajira hakuna umeme hakuna njaa ndiyo imetamalaki maeneo kedekede hivi rais anapata wapi ujasiri huu ?
 
Naona Nape ndo kaonekana mara nyingi sana, ndo Rais ajaye nini? Au ndo wewe mkuu uliyepost.
 
Yeah ni kweli Sherehe hizi zote hazina Maana; Yaani Wamemtuma Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kusherekea Tanu Day - Singida; matumizi mabaya ya Pesa za Nchi
 
Nchi masikini lakini kwa starehe inaongoza. Huu wote ni uvivu wa kukusanya kodi kiasi cha watu kubaki na pesa nyingi mfukoni za kufanyia mambo ya ajabu ajabu. Ingekuwa taiti kila kona, na kila mtu anapata pesa kwa haki hayo mambo yasingekuwepo!! Just look at the way walivyoshiba bila kujali wanahatarisha afya zao!!
 
Hakukua na tija ya kutumia vibaya Resources za wa Tz wakati huku ikisemekana kuna mikoa 16 kuna uhaba wa Chakula,hii kazi kweli kweli hawa ndio Magamba nawapeni pole nikijua za 40 za matapeli zinakaribia.
 
Marehemu TANU akifufuka leo atamshangaa sana mtoto wake alivyobadili dini na kuitwa Magamba.
 
duh watz hatuna vipaumbele , mnafanya birthday ya babu aliyeshafariki , mnatumia fedha nyingi kwa tukio lisilo na manufaa wananchi wanaokufa kwa kukosa huduma za afya, ajira hakuna umeme hakuna njaa ndiyo imetamalaki maeneo kedekede hivi rais anapata wapi ujasiri huu ?
Hebu fananua hapo kwenye bold, na Jipongeze hapo kwenye red!
 
Kuna tatizo! Kuna tatizo!

Angalia viongozi wanaowakilisha wanachama au wapiga kura tunaowategemea walivyokalishwa chini!

Ingekuwa mimi rais ningegoma mpaka waletewe viti hata mabenchi basi kama ni wengi! KUNA TATIZO jamani tumsaidie rais wetu - Miaka hamsini bado tunashabikia watu wenye heshima zao kama hawa kukaa chini? Jamani angalieni CHINA au DPR au USA au Britain jinsi chama kinavyo heshimu watendaji wake!

KUNA TATIZO!
 
Ajabu kweli' kuanzia Lumumba,Mnazi mmoja mpaka Ubungo plaza! Hiki chama kinatumia pesa nyingi sana! Hivi wanapesa eeh' hawa si ndiyo wanaongoza serikali masikin? Kazi ipo? Mwezi wa pili birthday ya ccm,mwezi wa saba Tanu!.
 
Sidhani hii inatakiwa wakati huu nchi ipo kwenye njaa, mgao wa umeme na matatizo kedekede
 
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Katibu Uenezi na Itikadi CCM Nape Moses Mnauye wakati wa shehere za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa chama cha TANU zilizofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jana usiku.

Sijui wanateta nini maana zimebakia siku 3 kati ya zile siku 90. Still counting.

GO9G8813.jpg
 
nisamehe dogo kwa kukutoa kafara,..yale majamaa huyawezi na hata mimi siyawezi,ila nakupigia makofi kwa kujitutumua,umewatisha hawajatishika,najicheka hata mimi sijui ni rais gani?!!!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hebu fananua hapo kwenye bold, na Jipongeze hapo kwenye red!
Soma vizuri we mvivu, ustafsiri neno mojamoja. Jamaa kaandika bila koma we umerukia bila kukifikirisha kichwa, msome vizuri utamtambua achoandika. Au nikusaidie sehemu hiyo. "........umeme hakuna, njaa imetaharamaki........."
 
Hakianani magamba watakufa hata kabla ya 2015. Wanaweza wakawa wanatawala lakini chama kitakuwa kiko ICU. Naona wamechanganyikiwa sasa wanaanzakutamani kujivua gamba wawe TANU, wanasahau kuwa CCM ni muungano wa TANU nna Afro shiraz. Au ndo wanavunja muungano ninii?

Nadhani wakiona wameshindwa kujivua gamba la kuwa TANU watarudi nyuma zaidi na kuwa TAA.

Huyu dogo Nepi wasipoangalia anawapeleka kuzimu haraka zaidi kuliko hata akina makamba.

Makamba alisema anaenda kuwaandalia makao nadhani alimaanisha hawatakawia yatawashinda na watamfuata yeye aliko sasa hivi.

Nadhani siyo muda mrefu watu wataanza kukataa uongozi wa ccm live, tusbiri
 
nisamehe dogo kwa kukutoa kafara,..yale majamaa huyawezi na hata mimi siyawezi,ila nakupigia makofi kwa kujitutumua,umewatisha hawajatishika,najicheka hata mimi sijui ni rais gani?!!!

Wote hali ngumu. Wanawaza nini?

c7.jpg
 
Kijana:Je! Mzee wafahamu Yanga wameingia nusu fainali kombe la kagame kwa njia ya matuta baada ya dk 90 na nyongeza? je waonaje wale triplet tutumie njia ya matuta baada ya siku 90 tu?

Mzee: Hapana bwamdogo, naona tuvute nao pumzi mdogo mdogo na ikibidi tuongeze siku30.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
bills.jpg

Kitu Pesa iko sumbua sana - Kitu Pesa iko sumbua akili za watu - Kitu Pesa haribu heshima ya mtu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom