Sherehe za muungano zapoteza mvuto! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sherehe za muungano zapoteza mvuto!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jidu, Apr 27, 2011.

 1. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,130
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Kwa mara ya kwanza nashuhudia kupoteza mvuto kwa sherehe hizi za Muungano,kwani ukianzia na mahudhurio pale uwanja wa amani hayakuwa mazuri sana na Kilicho nistajabisha ni juu ya vyombo vya habari hasa Runinga ukiachia TBC na channel ten ndivyo vilikuwa vinaonyesha lakini ITV haikuonyesha na vinginevyo!na Je mbona sherehe hizi kama sikosei zilifanyika mwaka jana Pemba,na kwanini mwaka huu hazikufanyika Bara?anayejua atujuze!
   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 23,087
  Likes Received: 10,404
  Trophy Points: 280
  ukiona moshi????.......
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Maadhimisho ya matukio muimu hapa nchini, ikiwa ni pamoja na haya ya muungano yaliyo azimishwa jana, yanaendelea kupoteza mvuto wake, hasa kutokana na ukweli kwamba kwa mazoea maadhimisho hayo yanahusishwa tu na gwaride na pengine , maonyesho ya zana za kivita. Kwa maana nyingine, yanatumika kama fursa ya viongozi wakuu, kuonyesha kwa umma nguvu na utukufu wao. Ili maadhimisho hayo yawe na maana kwa mtu wa kawaida nilidhani ingelikuwa vyema kama yangelikuwa yanatumika kufanya tadhmini ya kweli ya kujipima; nchi yetu imetoka wapi? iko wapi? na inakwenda wapi? Leo hii hata vyombo vya habari vinavyojaribu kufanya tathmini hiyo, vinafanya hivyo kinafiki kama kwamba tangu mwanzo vina lengo la kujenga picha ya kuwa mambo ni murua hata kama ushahidi wa mambo unatoa picha tofauti.
   
 4. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,817
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Muungano umechosha wengi,
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,033
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  na pia ni kwa manufaa ya wazanzibari kupata ardhi ya kuishi (bara) wa bara hatuihitaji zanzibar, bora usumbufu huo ukafanyikia huko huko kila mwaka.
   
 6. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #6
  Apr 27, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna maana gani kutumia hela nyingi kama kuandaa vikosi vyote vile kufanya zoezi la gwalide, wale watoto kufanya vile walivyofanya ilibidi wasafirishwe, walishwe na wanywe, wapatiwe mahali pa kulala, wapewe posho, wapewe vifaa vya kufanyia kazi, wakuu wote wale wasafirishwe, walazwe, wapewe posho, vipuri vya magari au usafiri kwa ujumla, muda vyote hivyo ili kukagua gwaride tu, huu ni wendawazimu kungekuwa na matamko kusinge leta mijadala hii, nakutumia rasmali za watanzania ambazo zingej enga hospitali, shule zingepatiwa waalimu vifaa vya kufundishia etc.

  Tutafakari jinsi ya kusherehekea siku hizi ni mzigo kwa taifa maskini kama Tanzania
   
Loading...