watanzania walipa kodi bila shaka sasa wanaugulia maumivu ya mabilioni yaliyotumika katika kilele cha sherehe za muungano, ni kweli sherehe zilifanya sana, acha vifaru, jwtz ilirudisha heshima yake kwa kuanika wazi silaha zetu za kivita, tumefaulu kuwapasha wale tunaowaita majirani wenye chokochoko akina banda na kagame
ni kweli ni sherehe nzuri , hata hivyo hakuna kumbukumbu itakayosalia baada ya sherehe hizi, leo nimeshuhudia lowloader za jeshi zikiwa mororgoro road kwenda kurudisha vile vifaru ngerengere, na huko mjini vijana wako busy wakibandua yale mabango! wiki mbili kuanzia leo labda kumbukumbu itabaki kuwa ni picha
tunaweza kujifunza kutoka afrika kusini katika kusherekea miaka 75 ya ANC walijenga na kuzindua Guntram train , treni ya umeme inayoenda kwa kasi kati ya johansburg na pretoria
tungeweza hata kutenga bilioni 50 tukajenga ile flyover ya ubungo na nyingine kule zanzibar na tukazindua siku ya muungano tukayaita haya madaraja kuwa muungano bridge ingebaki kumbukumbu ya kudumu, sasa tumetumia nasikia 76 bilioni na hakuna kumbukumbu yoyote zaidi ya mbwembwe za kuonyesha vifaru.
kama yote yangeshindikana basi tungeotesha miti ya muungano