Sherehe Za miaka 49 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania bara)

Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
64
Wanabodi,

Leo 9 December tunaadhimisha miaka 49 ya Uhuru na miaka 48 ya Jamhuri ya Tanganyika.
Kwa wale wenzetu wenye access ya TV au walioko uwanjani sio mbaya wakichukua picha za matukio kadhaa na kuyaweka hapa.
Japo matendo ya baadhi ya viongozi wetu wa leo yamewasaliti wale waliopigania uhuru, lakini bado siku hii ni muhimu kwa historia ya nchi yetu.

Nawakilisha,
 
Wacheni kutuchanganya, Hakuna kitu kinachoitwa Tanganyika, sasa tutasherehekea vipi kitu ambacho tumesema tukiuwe. Kama vipi tuifufue Tanganyika iwepo then tuanze kusherehekea uhuru wake.
Tusidanganyike Tanganyika haipo, kusherekea uhuru wake ni kujichanganya.
Tupiganie Tanganyika irudi na tutakuwa tayari na tutajisikia faraja kushiriki katika sherehe za Uhuru.
May got bless Tanganyika may God resurrect Tanganyika and Tanganyikans.
 
Huu ukaaji hapo uwanjani unanichanganya. Kaanza rais kafuata makam wake kafuata salma kikwete kafuata w-mkuu alafu spika. Je ni sahihi ki protokali?
 
hivi rais hatoi hata hotuba au anaongopa CHADEMA watatoka...maana naona anatoka
 
Huu ukaaji hapo uwanjani unanichanganya. Kaanza rais kafuata makam wake kafuata salma kikwete kafuata w-mkuu alafu spika. Je ni sahihi ki protokali?

Mi nafikiri umefika wakati nafasi ya firstlady ikatambulika kisheria, sababu ukiachana na hii ya kwenye masherehe ambayo unaweza ukasema hakuna tatizo kwa yeye kuwepo pale, mkanganyiko huwa unatokea huyu mama akienda kwenye ziara za mikoani maana kunawakati huwa anasomewa hadi taarifa za maendeleo za wilayani na rasilimali za serikali huwa zinatumika hata kama kaenda kwa shughuli za CCM.
 
TBC 1 mbona walikuwa hawarushi? niliangalia kidogo kwa nusu saa kupitia ITV lakini nili-tune TBC 1 walikuwa na programme nyingine. au walijiunga baadae?
 
Wanabodi,

Leo 9 December tunaadhimisha miaka 49 ya Uhuru na miaka 48 ya Jamhuri ya Tanganyika.
Kwa wale wenzetu wenye access ya TV au walioko uwanjani sio mbaya wakichukua picha za matukio kadhaa na kuyaweka hapa.
Japo matendo ya baadhi ya viongozi wetu wa leo yamewasaliti wale waliopigania uhuru, lakini bado siku hii ni muhimu kwa historia ya nchi yetu.

Nawakilisha,

Siko mbali sana na wewe ndugu yangu,kweli siku hii ni ya kihistoria zaidi than anything else.Utumwa tulionao leo ni mbaya zaidi kuliko wa miaka hamsini iliyopita!Sasa ndugu yangu katika hali hiyo bado una hamu ya kuona picha za hiyo geresha,una moyo.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom