Sherehe za Mapinduzi uwanja wa Amani Zanzibar Rais Magufuli na Dr Shein kuhudhuria

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,558
Sherehe hizi zitarushwa mubashara kupitia TBC, Channel ten, Azam tv, ITV nk

Rais Magufuli wa JMT na Rais Shein wa Zanzibar watawaongoza maelfu ya watanzania katika maadhimisho hayo.

Karibuni!

Up dates;

Viongozi wastaafu wameshaingia ukumbini wakiwemo mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Sumaye, Lowassa, Pinda nk
 
Ni siku nyingine Tena ya tarehe 12.01.2020,ikiwa ni kumbukizi ya Mapinduzi ya Zanzibar,binafsi nawatakia wazanzibar wote heri ya siku hii maalum kwao.
Mwaka 2012/2013 nilibahatika kuwa viunga vya Nchi hiyo japo nilifika kuelekea mwisho na kuondoka mwanzoni mwa mwaka hivyo sikubahatika kuhudhuria siku hii maalum kwa wazanzibar.
Niseme ni Nchi POA Sana nakumbuka tukiwa mafunzoni asubuhi tulikuwa tunafanya jogging kuweka miili sawa,lakini hatujawahi zenguliwa.na wazanzibar nimekutana nao Hadi huku bara kwenye mafunzo Tena na wengi wao ni marafiki Hadi leo hii.
Pale Mwanakwerekwe ndio soko lao/center yao nzuri kwa biashara.nazikumbuka zile gari zao maarufu Chai maharage zinazopiga route toka shamba to mjini.
Chakushangaza Kuna sehemu kunauzwa gongo!!!!
Naahidi ipo siku nitarudi Tena kutalii sio Tena kikazi.muwe na siku njema.
 
Leo ndio Leo machatos mtatuambia hizo sherehe zinaongozwa na she in au jiwe maana ninavyomjua boss wenu kupenda kila kitu kuongoza sijui Leo atafanya nini ! Jana aliona kuzindua hotel akaamua kuzindua na vijanjaweed na kuvichangia tzs 150m
 
Sherehe hizi zitarushwa mubashara kupitia TBC, Channel ten, Azam tv, ITV nk

Rais Magufuli wa JMT na Rais Shein wa Zanzibar watawaongoza maelfu ya watanzania katika maadhimisho hayo.

Karibuni!
Sema Rais wa Tanzania Bara na Rais wa Tanzania Visiwani.

Zanzibar ni nchi na ina mamlaka kamili. Mbona mnawanyanyapaa sana.
 
Sherehe hizi zitarushwa mubashara kupitia TBC, Channel ten, Azam tv, ITV nk

Rais Magufuli wa JMT na Rais Shein wa Zanzibar watawaongoza maelfu ya watanzania katika maadhimisho hayo.

Karibuni!

Acha uongo! Wataongozaje wawili? Sema Rais Mohammed Shein ataongoza sherehe hizo akishuhudiwa na waalikwa wote akiwamo John Magufuli, Samia, Lowassa, Bw. Juma Khamisi, Abdalla, Joseph, JohntheBaptist nk.
Mkuu wa nchi ni yule anayepigiwa mizinga na ndiye last in first out uwanjani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuongoza sherehe na kuongoza watanzania ni vitu viwili tofauti bwashee!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom