Sherehe za maadhimisho ya miaka 100 ya Shirika la Kazi Duniani (ILO)

rose mzalendo

Member
Mar 5, 2019
71
114


Ofisi ya Waziri Mkuu inapenda kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa tarehe 14 Septemba 2019 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wanaadhimisha miaka 100 ya tangu kuanzioshwa kwa shirika la Kazi Dunia

Akizungumzia maadhimisho hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama amesema kuwa katika kushereheka maadhimisho ya miaka 100 ya Shirika la Kazi Duniani Serikali kwa kushirikiana na Shirika hilo itaadhimisha sherehe hiyo kwa kufanya mambo mawili ambayo ni uzinduzi wa programu ya mafunzo ya kukuza ujuzi kwa vijana wapatao 5000 katika Chuo cha Veta Donbosco jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo yatahitimishwa kwa zoezi la kupanda miti mia moja katika Mji wa Serikali litakaloongozwa na Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa ikiwa ni kumbuku ya Shirika hili kutimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake.

Maadhimisho hayo yanafanyika ikiwa ni miaka 60 tangu shirika hilo lianza kazi Barani Afrika na miaka 57 tokea lianze kufanya kazi nchini Tanzania.

Sisi kama Tanzania tunayo nafasi sasa ya kujitathmini wakati huu tukiwa katika kuadhimisha miaka 100 ya uwepo wa ILO, katika kujitathmini huko Tanzania kama mwanachama imepiga hatua zifuatazo;

  • Tanzania imeridhia mikataba 37 na kutunga sera na sheria zinazoendana na mikataba hiyo.
  • Tumetengeneza miongozo ya masuala mbalimbali yanayohusiana na mahala pakazi ie. Usalama mahala pakazi, Uhuru wa vyama vya wafanyakazi kuwepo mahali pa kazi, na afya na usalama mahali pa kazi
  • Fidia kwa wafanyakazi
  • Utoaji wa huduma ya hifadhi ya jamii
Shirika la Kazi Duniani(ILO) ni taasisi mahususi ya Umoja wa Mataifa inayoshirikiana na nchi wanachama kwa kutoa miongozi kupitia mikataba mbambalimbali kwa lengo la kuboresha mazingira na masuala ya kazi kwa ujumla.

Lengo hasa ni kujenga uchumi kwa nchi wanachama na kuleta maendeleo endelevu kwa jamii
 
Back
Top Bottom