Sherehe za kufikiwa maridhiano ya kitaifa ya Wapalestina mjini Cairo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sherehe za kufikiwa maridhiano ya kitaifa ya Wapalestina mjini Cairo

Discussion in 'International Forum' started by mdau wetu, May 5, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sherehe za kufikiwa maridhiano ya kitaifa ya Wapalestina mjini Cairo [​IMG]Mji mkuu wa Misri Cairo, jana ulishuhudia sherehe za kitaifa za Wapalestina za kutiwa saini hati ya maridhiano ya kitaifa baada ya kuzaaa matunda juhudi na mazungumzo ya mwaka mmoja katika hali ambayo viongozi wa utawala wa kizayuni wa Israel wanahaha huku na kule ili kuhakikisha wanayafelisha maafikiano hayo. Katika kutekeleza mkakati huo, Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni Benjamin Netanyahu ameelekea Ulaya ili kuzungumza na viongozi wa Uingereza na Ufaransa juu ya suala hilo. Kuhusiana na maafikiano yaliyofikiwa kati ya harakati za Fat-h na Hamas, Netanyahu amesema maafikiano hayo yatakuwa tishio kwa Israel katika siku za usoni.
  Hatimaye baada ya mazungumzo ya karibu mwaka mmoja na nusu yaliyofanyika kwa upatanishi wa Misri, makundi ya Kipalestina yakiongozwa na harakati za Fat-h na Hamas yamesaini hati ya maafikiano ya maridhiano ya kitaifa. Maafikiano ambayo vyombo vya habari katika eneo vimeyaelezea kuwa ni tukio muhimu katika historia ya Palestina na ambalo limeonekana kuwa na mfungamano na mapambano ya umma yanayoendelea kushuhudiwa hivi sasa katika nchi mbalimbali za eneo hili. Hati ya mwisho ya maafikiano hayo ilisainiwa hapo jana na kiongozi wa harakati ya Fat-h Mahmoud Abbas na Khalid Mash'al, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, na hivyo kufungua njia ya uundaji serikali ya umoja wa kitaifa ya Wapalestina.
  Kwa mtazamo wa weledi wengi wa mambo, Mashariki ya Kati mpya iliyo dhidi ya Israel imo katika hali ya kudhihiri, na huu ni ukweli ambao utawala huo wa kizayuni na waungaji mkono wake wa Magharibi hawana budi kuukubali. Na hasa kwa kuzingatia kwamba baada ya kupita miongo miwili, mazungumzo ya mapatano yaliyofanyika chini ya usimamizi mbovu wa Marekani yamefeli; na hivi sasa baada ya kupita miaka 20 ya mazungumzo hayo yasiyo na tija yoyote Wapalestina wako katika hali mbaya zaidi kuliko ile waliyokuwa nayo mwaka 1991 wakati yalipoanza mazungumzo hayo yaliyoitwa ya amani ya Mashariki ya Kati. Licha ya ahadi ambazo Marekani ilitoa kwa Wapalestina kuhusiana na kutekelezwa maazimio ya Umoja wa Mataifa juu ya kuondoka Israel katika ardhi za Palestina inazozikalia kwa mabavu na kuundwa nchi huru ya Palestina, lakini tokea wakati ule ule yalipoanza mazungumzo hayo, Washington iliwaacha mkono Wapalestina kwa kuyaendesha mazungumzo hayo katika sura ya kupitisha muda tu, huku hatua hiyo ikikaribishwa na Wazayuni ambao waliutumia mchakato wa mazungumzo hayo yasiyo na tija kupoteza muda na kuchochea mifarakano baina ya Wapalestina na wakati huohuo kujiondoa katika hali ya kutengwa kieneo na kujipatia itibari ya kisiasa katika ulimwengu wa Kiarabu.
  Japokuwa hatua iliyochukuliwa na Fat-h chini ya kiongozi wa wakati huo wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO Yasir Arafat ya kujitumbukiza kwenye mtego wa mazungumzo ya mapatano na wazayuni ulikuwa mwanzo wa kuukengeuka mkondo wa historia ya mapambano ya ukombozi ya Wapalestina, lakini haukupita muda ikadhihirika kuwa maafikiano eti ya amani ya Oslo ulikuwa mchezo wa kisiasa tu waliochezewa Wapalestina na utawala haramu wa Israel. Na hapo ndipo wananchi wa Palestina walipoamua kuchukua maamuzi ya kishujaa katika uchaguzi wa Januari mwaka 2006 wa bunge walipoamua kuikabidhi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas hatamu za uongozi na kutoa ujumbe kwa viongozi wa Fat-h na Israel kwamba hawatoendelea kuwa watazamaji wa mchezo wa kisiasa wa kupoteza wakati unaochezwa na Wazayuni. Yaliyojiri baada ya hapo, yaani kutengana Fat-h na Hamas na kufuatiwa na kutenganika Ukanda wa Gaza na Ufukwe wa Magharibi kulitoa pigo kubwa kwa umoja wa Wapalestina; kwani kwa upande mmoja kulifungua njia kwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina chini ya uongozi wa Mahmoud Abbas kulegeza msimamo na kuridhia kila walilotaka Wazayuni na kwa upande mwengine kukaandaa mazingira kwa Wazayuni ya kuiwekea mzingiro Gaza na kuanzisha mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa eneo hilo.
  Kwa hivyo hatua iliyochukuliwa hivi sasa na Fat-h na hasa kiongozi wake Mahmoud Abbas ya kuamua kujiunga na safu za wananchi wake, kwa kuzingatia kwamba kusainiwa hati ya mardihiano ya kitaifa kumefungua njia ya kurejesha haki za wananchi wa Palestina, kumewatia kiwewe viongozi wa kizayuni; na bila ya kificho wanafanya kila wawezalo ili kuyavuruga maafikiano hayo. Ukweli ni kwamba baada ya miaka 63 ya kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu ardhi yao, makundi yote ya Kipalestina sasa yameamua kwa dhati kuwa yanataka kuunda nchi yao ya Palestina, suala ambalo limewatia kiwewe na khofu kubwa viongozi wa kizayuni.../

  Kwa hisani ya Redio Tehran, Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
   
Loading...