Sherehe kubwa ya Dk Slaa; Nilidhani CHADEMA ni watu wenye utu...

Ukiwaona bungeni wakitetea maslahi ya wanachi utaamini ni watu. Angalia wakisahau tu utawaua ukweli wao
leo Mh tundu Lissu alitaka kujienyesha anawapenda watz kwa kutaka kuleta Hoja ya Meli ya ZANZIBAR. Kumbe akitaka Kumtia ubayani mama yetu.

Ikiwa Tanzania inamaombelezi kupata msiba. Dk slaa anafurahika na Kunywa. kula na vigelegele juuu.
huku wabunge wake wakijifanya wanalia Kilio cha Kudangaya, Kumbe Jioni wanakimbilia DANSI kukata kucheza, kuimba na Kupiga bia.

watz tushukuru na tuamke kwamba Mungu ametuonyesha Mapema jinsi wanasiasa hasa Chadema wasivyojali watu


KESHO MAGAZETI MENGI YATATOA TAHAHARIRI NA PICHA ZA DK SLAA AKIPIGA MZIKI HUKU TAIFA LIKIWA KWENYE MAOMBOLEZI

Kwa hiyo ulitaka Dr Slaa asioe kwa sababu Meli imezama? Ndo sio anaamua yeye kuwa leo nafunga na kesho naacha ila inaandikishwa na kufuata taratibu zote za kisheria.

Hii ni issue ya kifamilia na sio kichama, wewe unaishi ili iweje km huwezi hata kufikiri jambo dogo km hilo then unaibuka nalo tu hapa?

Km wewe sio fisadi basi maisha yako yatakuwa magumu sana maana huonekani km uwezo wako wa kufikiri upo sawa. Sasa ulitaka Dr Slaa aseme nasogeza ndo mbele na leo kumetokea ajali WAMI pia asifunge ndo kuna ajali Wami, etc.

Akili yako inakutuma kuwa Dr Salaa alivyofunga ndoa waliokuwepo ni Chadema peke yao sio? Hili jambo la family halina uhusiano na vyama so pale ni kadi ya mwaliko kutoka kwa family na sio kwa chama fulani.
 
Haiwezekani watu tunaomboleza jamaa anaoaaaa Daaaaaaamnnnnnnnn!!huu ni ubinafsi wa hali ya juu

Watu waliozoea ndoa za mkeka utawajua tu, mkuu kwani we hufahamu ndoa za kikristo huwa seme setiwa hadi tarehe? na huwa aidha kuna matangazo kanisania aua bomani, sasa hiyo pia ipo kisheria, hivi unakumbuka wakati ule Nyerere alipo fariki? Serikali haikuzuia ndoa bali ilizuia sherehe zenye mwelekeo wa mbwembwe nyingi, nakumbuka ndoa kadhaa wakati huo zilifungwa vizuri tu, sasa hapa issue ni nini? tuwe wakweli, hivi MV Victoria ilipo zama, Zanzibar kulikuwaje? mlisitisha kila kitu hadi ndoa za mkeka? Mawazo mengine bana, full kichefu chefu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom