Sherehe baada ya kuteuliwa ukuu wa mkoa inaelekeza nini kwa wananchi haswa maskini?

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,488
257
Ndugu zangu naomba maoni yenu kwa hali hii iliyokithili kwa wateule wa rais baada ya kuteuliwa kufanya sherehe ya kujipongeza wangali wakijua majukumu waliyopewa ni mazito na hasa ukizingatia matatizo ya wananchi waliombele yao.
 
Hili sasa linageuka kuwa taifa la walalamishi au wanun'gunikaji. Huwezi kuwa mtu unakosoa kila kitu as if huna mambo mengine ya kufanya. This is too much! Ulitaka iwe kimya kimya kama mtu aliyechomwa sindani?
 
Mbona hausomeki.?
 
Kama Rais mwenye majukumu makubwa kuliko Mkuu wa Mkoa alisherekea sembuse wao!nadhani si dhambi na si sababu pia ya wao kushindwa kutekeleza majukumu yao.
 
Hili sasa linageuka kuwa taifa la walalamishi au wanun'gunikaji. Huwezi kuwa mtu unakosoa kila kitu as if huna mambo mengine ya kufanya. This is too much! Ulitaka iwe kimya kimya kama mtu aliyechomwa sindani?
<br />
<br />
Sindani ndio nini? Au umelewa mbege?
 
Wanasherekea ulaji 2 na hakuna kingine.Nakumbuka mara baada ya lowasa kujiuzuru na kupelekewa kuvunjwa kwa balaza la mawaziri lawrence kego masha aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani mara baada ya kuapishwa 2 alivikwa mataji na ndugu na marafiki zake kana kwamba mshindi lakini leo yako wapi tupo tunapiga nae polojo tu mtaani labda amsubiri mkuu wa kaya ampe mikoa iliyobaki lakini nachomaanisha kama uteuzi ni wa haki mungu nae utenda haki lakini kama ni wa magumashi mungu nae ushusha ghalika.
 
wacha watumie mali za umma HII SASA NI SERIKALI YA KISELA maskini tulishaambiwa tule majani toka enzi za Mramba
 
Kusherehekea vyeo ni utamaduni wa siku nyingi wa Watanzania, wengi hawaoni ni tatizo kabisa. Ninachofurahi ni kwamba siku hizi kitu hicho watu wameanza kukihoji, kukiona kimekaa kushoto. Taratibu huo utamaduni utaondoka kwa kadri kizazi cha wazee walioko madarakani kitakavyofifia.

Madaraka ni heshima, ni mafanikio ya kuyakaribisha, lakini pia ni majukumu. Katika kuonyesha unatambua majukumu mazito yaliyo mbele yako na dhamira ya kupambana nayo huwezi kufanya pati, labda ufanye misa kanisani, ualike maimam usomewe dua, uende kwa mganga uchanjiwe madawa ya kuongeza nguvu, nitakuelewa. Sio pati jamani.
 
Hili sasa linageuka kuwa taifa la walalamishi au wanun'gunikaji. Huwezi kuwa mtu unakosoa kila kitu as if huna mambo mengine ya kufanya. This is too much! Ulitaka iwe kimya kimya kama mtu aliyechomwa sindani?

pole wewe kwa sasa ni DC ntarajiwa?
 
umesomeka nami nilidhani hivyo ndiyo ilipaswa kuwa utamaduni wa asiliyetu.
 
Back
Top Bottom