Shenzhen: Alama ya mafanikio ya sera ya mageuzi na ufunguaji mlango nchini China

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
71
110
Miaka 40 baada ya kuanzishwa kama eneo maalum la kwanza la Ukanda wa Kiuchumi nchini China, Shenzhen imeibuka na kuwa alama ya mageuzi na ufunguaji mlango wa China. Mji huo umebadilika kutoka kijiji cha uvuvi na kuwa mji mkubwa wa viwanda na fedha.

Utafiti uliofanywa na Program ya Makazi ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa mwaka 2019 unaelezea maendeleo ya kasi ya Shenzhen tangu mwaka 1979 yanaweza kuelezewa katika awamu nne.

Kabla ya China kuanza kufungua milango yake kwa uwekezaji wa kigeni na kuhamisha mpango wake wa uchumi kuelekea soko la uchumi kuanzia mwaka 1978, Shenzhen ilikuwa kijiji kidogo chenye wakazi 330,000 tu. Katika awamu ya kwanza, kuanzia mwaka 1978 hadi 1992, Shenzhen ilifanya kazi katika maendeleo ya nguvukazi ikiungwa mkono na sera ya taifa ya kufungua mlango na mageuzi ya kitaasisi. Kutokana na eneo lake kijiografia, kupakana na kuungana na eneo la Asia Kusini Mashariki na mkabala na Hong Kong, Delta ya Mto Pearl, Shenzhen ilikuwa sehemu ya kwanza nchini China kuanzisha “biashara ya pande tatu ya uingizaji na fidia”.

Kutokana na mtaji na uzoefu wa uzalishaji uliopatikana katika awamu ya kwanza, Shenzhen iliendelea mbele na kuingia awamu ya pili kuanzia mwaka 1992 hadi 2003, ambapo mji huo ulifikia nafasi ya chini-kati katika thamani ya mnyororo wa dunia, ukilenga maendeleo ya mitaji ya kina. Kutokana na China kutambulisha uchumi wa soko, Shenzhen ilivutia uwekezaji zaidi wa moja kwa moja wa kigeni, na hatimaye kuhamia kwenye sekta ya vifaa vya kielektroniki na mawasiliano. Katika kipindi hicho, Shenzhen ilikuwa kituo cha uzalishaji wa vifaa vya mawasiliano ya simu duniani.

Kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2013, Shenzhen ilifikia ngazi ya kati ya thamani ya mnyororo wa ugavi wa kiviwanda duniani, ikiwa na matawi ya kampuni binafsi za teknolojia ya juu. Mwaka 2010, Kampuni ya Teknolojia ya Huawei, ambayo ilianzishwa mwkaa 1987 mjini Shenzhen, iliingia kwenye orodha ya Fortune Global 500 kwa mara ya kwanza.

Baada ya mwaka 2013, Shenzhen ilifanikiwa kufikia ngazi ya juu ya thamani ya mnyororo wa ugavi duniani. Ikiungwa mkono na kampuni kubwa nyingi za teknolojia, kama vile kampuni maarufu ya mtandao ya Tencent, mji wa Shenzhen umebadilika na kuwa kitivo cha teknolojia katika bara la Asia. Mwaka jana, idadi ya hataza zilizoombwa kutoka Shenzhen ziliongoza nchini China, zikichukua asilimia 6.23 ya mombi yaliyotolewa nchi nzima.

Wengi wanajiuliza, ni nini kimeufanya mji huu wa Shenzhen kupata maendeleo makubwa na ya kasi ndani ya muda mfupi? Tofauti na Beijing na Shanghai, uwekezaji mkubwa wa teknolojia mjini Shenzhen unaendeshwa na soko. Makampuni yanachangia karibu asilimia 90 ya uwekezaji katika utafiti, na zaidi ya asilimia 90 ya maombi mapya ya hataza. Shenzhen pia imekuwa kitovu cha dunia kwa uvumbuzi wa vifaa. Siri nyingine kubwa ni sera zinazounga mkono ukuaji. Mfano, mwaka 1982 benki za kigeni ziliruhusiwa kufungua matawi yao mjini Shenzhen, mwaka 1992 Soko la Hisa la Shenzhen lilifunguliwa, nan i moja ya masoko mawili ya hisa China bara. Pia, kama wewe una kampuni ya teknolojia ya juu na unatengeneza software ama vifaa vya kompyuta, inawezekana usilipe kodi kwa miaka miwili ya mwanzo, na kama wewe ni mwajiriwa, na unaonekana kuwa na ujuzi wa hali ya juu, serikali inaweza kukupa unafuu katika kodi ya nyumba na kipato. Kutokana na hilo, katika eneo la biashara huria la Shenzhen, kampuni zinaweza kufurahia kodi za chini zaidi na kanuni zinazonyumbulika.

Kwa siku za baadaye, China inalenga kujenga mji mkuu wa Shenzhen kuwa mji wa kisasa duniani wenye ushindani wa kipekee, uwezo wa uvumbuzi na ushawishi. Shenzhen pia inatarajiwa kuwa kiongozi wa majaribio ya ujenzi wa eneo la ujamaa wenye umaalum wa Kichina. Mwongozo uliotolewa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali la China Agosti mwaka 2019 unaelekeza kuwa, mpaka kufikia mwaka 2025, mji wa Shenzhen unapaswa kuwa mji wa kisasa wa kimataifa wa uvumbuzi kutokana na nguvu yake ya kiuchumi na unora wa maendeleo katika miji yote duniani. Pia kufikia mwaka 2035, mji huo unapaswa kuwa kitovu cha uvumbuzi, ubunifu na ujasiriamali, na pia mfano wa China wa kujenga nchi kubwa ya ujamaa wa kisasa katika ngazi ya mji. Pia mwongozo huo umeelekeza kuwa, Shenzhen inapaswa kuwa mfano wa jamii ya kistaarabu na maisha bora kwa wakazi wake, na kiongozi katika kutimiza maendeleo endelevu.
 
Shenzhen ni moja wapo wa maeneo manne ya mkakati wa kiuchumi wa China kupitia sera ya ufunguzi.

“ Four Special Economic Zones ”.
 
Back
Top Bottom