Shemejiye Dk. Shukuru Kawambwa auwawa na majambazi shambani kwake Dk. Kawambwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shemejiye Dk. Shukuru Kawambwa auwawa na majambazi shambani kwake Dk. Kawambwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, May 27, 2009.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Habari zilizopatikana jioni hii (Jumatano, Mei 27, 2009) zinasema kwamba shemeji yake Dk. Shukuru Kawambwa, ambaye ndiye aliyekuwa msimamizi wa shamba la Dk. Kawambwa (Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu na Mbunge wa Bagamoyo - CCM), ameuwawa jana, Jumanne, Mei 26, 2008, takriban saa 2 usiku, baada ya tukio la uhalifu ambalo watu kadhaa walivamia kwenye shamba hilo wakiwa na nia ya kufanya uporaji.

  Chanzo cha habari hizi kinasema kwamba katika purukushani hizo, shemejiye Dk. Kawambwa, ambaye alikuwa akisimamia shamba hilo lenye idadi kubwa ya mifugo na mazao kadhaa, akishirikiana na mkewe (dada wa Dk. Kawambwa), alipigwa risasi kwenye miguu yote miwili na kuanguka chini. Akipambana na maharamia hao, alifanikiwa kumvua soksi ambayo ilikuwa imeuficha uso wa mmoja wa wahalifu hao, akamtambua. Alihamaki na kuonesha kwamba amemtambua, jambo ambalo linasadikiwa kuchangia kifo chake, kwani majambazi hao waliokuwa na silaha za moto pamoja na mapanga waliamua kummaliza kwa kumkata mapanga shingoni.

  Chanzo kimeeleza zaidi kwamba katika siku za karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la uhalifu kwenye Wilaya ya Bagamoyo, jambo ambalo limewafanya wakazi wa mji huu wenye historia kongwe kuishi maisha ya hofu na wasiwasi mkubwa.

  "Tumekuwa tukivamiwa, wakiingia wanachukua chochote kile chenye thamani kwao, TV, redio, kompyuta, chochote kile... ukiwabishia utaumizwa..." kilisema chanzo hiki.

  Inasadikiwa kwamba baada ya uvamizi kwenye shamba hilo la Dk. Kawambwa iliwachukua takriban muda wa saa moja askari polisi wa Kituo cha Bagamoyo kufika hapo, eneo la Sanzale, wakati huo wahalifu wakiwa wameshafika mbali na kutoweka kabisa.

  Kwa maoni ya chanzo cha habari hizi, inashangaza ni kwa sababu gani mpaka sasa habari za tukio hilo la uhalifu lililotokea kwenye shamba kubwa la mmojawapo wa viongozi waandamizi wa Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na CCM halijatangazwa kwenye vyombo vya habari. Maoni ya wadau kadhaa yameelezea kuwapo kwa jitihada za kuficha habari hizi ili kuficha ukweli kwamba Waziri huyo mwandamizi ni mkulima na mfugaji hodari, jambo ambalo linashangaza, kwa kuwa kilimo na ufugaji ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania. Hata hivyo, wadau wamesema, pengine ni ukubwa wa shamba hilo ndio unaoweza kuwa sababu ya Waziri huyo kutotaka habari hizo kutangazwa, kwani zinaweza kumwaibisha na kumharibia nafasi yake kwa namna fulani.

  Wachunguzi wa habari zaidi watazidi kutuletea habari na maoni zaidi kuhusu tukio hili la kusikitisha.
   
 2. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Say whaaat?

  Hivi hawa waandishi wa habari wanaokotwa wapi?
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Only in Tanzania,

  Ati ukubwa wa shamba utamuaibisha Waziri! We got it twisted.
   
 4. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ''Hata hivyo, wadau wamesema, pengine ni ukubwa wa shamba hilo ndio unaoweza kuwa sababu ya Waziri huyo kutotaka habari hizo kutangazwa, kwani zinaweza kumwaibisha na kumharibia nafasi yake kwa namna fulani.''

  MwanaHaki,

  Kama yeye ndio ametaka zisitangazwe basi kipo kitu hapo.How big is the shamba?
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wabongo ndiyo maana hatuendelei, mawazo yetu yamekaa ki Sokoine Sokoine tu.

  Inakumbusha jitihada za watu kujenga makwao zilivyodorora kwa hofu ya "kulogwa". Waziri si ndiye atie mfano kwa kuwa na shamba kubwa, akiwa na shamba dogo atasemwa si wa kupigiwa mfano, akiwa na shamba kubwa automatically mikingamo inaanza kama vile njia pekee ya kupata shamba kubwa ni ufisadi, yaani tabu tupu.

  Na habari yenyewe ilivyoletwa imeletwa kiudakun udaku, so what watu hawajaripoti kuvamiwa kwa shamba la waziri? Pengine kuna juicier stories zaidi zinazoweza kuuza magazeti yao vizuri, sasa huyu muandishi anakuja na assumption ambayo haijafanyiwa hata tone la uchunguzi, assumption kwamba kuna cover up. I would not b surprised if his political rivals are behind this, they seem to be close to him.

  Lazima tuelewe kuwa hatuwezi kuendelea bila classes, hii ndoto ya a classless society inatufunga katika umasikini.Kimsingi ukisema hutaki classes katika society unasema unataka wote muwe maskini. Na swali la "kapata wapi mali" unless linaulizwa katika justified legal impeachment proceedings ni la kichimvi na kichawi, mtu halazimiki ku reveal alivyopata mali, it is against the laws of economics.Akwambie halafu wewe umzidi?

  Kampeni za 2010 zishaanza mapemaaaa!
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,637
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Maoni ya kimajungu hayo!
   
 7. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #7
  May 28, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kwani kuwa na shamba kubwa ni kosa? Wapo wanaotafsiri hivyo ndani ya CCM yenyewe, ndio maana wakubwa wenyewe (mawaziri, nk) hawataki ijulikane ukubwa wa mashamba yao, wasijeambiwa wamejilimbikizia mali. Kama huo ni ufisadi mimi simo.
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  watanzania bana

  uktoka madarakani umechoka...ati kaisha huyo
  ukiwa na vijiekari duh......mwizi

  waacheni wale jamani;biblia inasema wa madhabahuni ale madhabahuni
   
 9. L

  Limbukeni Senior Member

  #9
  May 28, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tofauti ya walionacho na wasionacho ndio tatizo
   
 10. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Pole sana namjua huyo mzee alieuawa..ila sikujua kama ni ndugu..(shemeji)du poleni sana familia..ya Kisawaga.Tusijisahau wanadamu kuwa hapa duaniani si petu....tujiandae wakati wowote......maana huwezi jua lini...wapi saa ngapi bwana atakuita.............
   
 11. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi nyie watu si kila kitu lazima mkilete as Breaking News hapa JF, mnaboa sasa mweh
   
Loading...