Shemejio akija hivi utamjibu nini?

Mtu B

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
919
51
Jamani mhusika wa hii story si mimi, ni kwamba imenivutia tu nikaikopi hapa ili nipate pia mawazo yenu, maana leo ni kwa huyu pengine kesho inaweza kuwa wewe. Kisa chenyewe mhusika kakieleza kama ifuatavyo:

Kuna siku mume wa demu wangu wa zamani aliwahi kuniita tukutane mahali ana jambo la kujadili nami. Bahati nzuri tunafahamiana kiasi kwani wakati anamchumbia huyo demu bado nilikuwa nae, tulikuwa chuoni na mambo yangu yalikuwa hayajawa na msimamo, kwa hiyo demu aliponieleza kuna mtu kaonesha interest nimpe msimamo wangu, tukakubaliana aendelee nae. Hata hivyo hakuwa amemwambia tuna uhusiano, kwa hiyo jamaa akawa ananiita "shemeji". Tukakubaliana na yule msichana kuwa tuwe kaka na dada, na tumeendelea hivyo hadi leo. Basi hiyo siku jamaa alivyoniita (ilishapita miaka 4 na walikuwa na mtoto), kwa kuwa hatukuwa tumepanga lolote, "chale" likanicheza nikampigia "dada" simu, akanijibu hana habari kuwa mwenzie ana kikao nami, nikajua kuna mtego. Nimefika pa kukutania nikamkuta yuko peke yake, keshaagiza nyama choma na bia, tukaendelea. Akiwa ameshalamba bia nne za fastafasta (haikuwa tabia yake, nadhani alikuwa anaondoa nishai), akaanza kunihoji kipolisi, nimwambie ati mkewe nilishamlala mara ngapi?

Kama ni wewe ungemjibu nini "shemejio" huyo?
 
Swali gumu kweli lakini nitajikaza tu, nitamjibu sijawahi kulala na mkeo. Kwani kama nililala naye kabla ya kuoana basi hakuwa mke wake, hivyo basi nikisema sijawahi kulala na mkeo nitakuwa sijakosea!!!! Sijawahi Kulala na Mkeo na Naomba uniheshimu na kuniuliza hili umenikosea heshima yangu!
 
hilo nalo neno....
 
Ningemuuliza swali moja tu!!! DOES IT MATTER?? Maana kuna magwiji wa kuhamishia matatizo yao ya ndoa kwa wenzao
 
Akiwa ameshalamba bia nne za fastafasta (haikuwa tabia yake, nadhani alikuwa anaondoa nishai), akaanza kunihoji kipolisi, nimwambie ati mkewe nilishamlala mara ngapi?[/B][/I]

Ningemjibu sikumbuki ni mara ngapi ila kipimo ni idadi ya magoli yanawoweza kujaza kindoo kidogo cha lita 10, akafe mbele huko na presha.
 
Akiwa ameshalamba bia nne za fastafasta (haikuwa tabia yake, nadhani alikuwa anaondoa nishai), akaanza kunihoji kipolisi, nimwambie ati mkewe nilishamlala mara ngapi? Kama ni wewe ungemjibu nini "shemejio" huyo?[/B][/I]

Kwanza ningemtaka aniombe radhi kwa kunivunjia heshima....! Kitendo cha kuuliza nimelala mara ngapi na mkewe ni kutaka shari na kwa vile yeye kajiandaa kwa shari mimi sio mtu wa shari.

Pili, ningemuomba hiyo ajenda tupange siku tufanye kamkutano kadogo tuijadili....sio wakati huo na sio baa...!
 
Ningemjibu sikumbuki ni mara ngapi ila kipimo ni idadi ya magoli yanawoweza kujaza kindoo kidogo cha lita 10, akafe mbele huko na presha.

Duh!...wewe kweli huna imani na hawa.Unampa mwenzio levo ambayo
kwamba akienda nyumbani anatoa talaka moja kwa moja.
 
mie ningemuuliza hivi, huyo mkeo ulimkuta bikra na kama sio ushawafata wote waliomlamba na kuwauliza the same qn kwamba wamemlala mara ngapi?
 
Jamani mhusika wa hii story si mimi, ni kwamba imenivutia tu nikaikopi hapa ili nipate pia mawazo yenu, maana leo ni kwa huyu pengine kesho inaweza kuwa wewe. Kisa chenyewe mhusika kakieleza kama ifuatavyo:

Kuna siku mume wa demu wangu wa zamani aliwahi kuniita tukutane mahali ana jambo la kujadili nami. Bahati nzuri tunafahamiana kiasi kwani wakati anamchumbia huyo demu bado nilikuwa nae, tulikuwa chuoni na mambo yangu yalikuwa hayajawa na msimamo, kwa hiyo demu aliponieleza kuna mtu kaonesha interest nimpe msimamo wangu, tukakubaliana aendelee nae. Hata hivyo hakuwa amemwambia tuna uhusiano, kwa hiyo jamaa akawa ananiita "shemeji". Tukakubaliana na yule msichana kuwa tuwe kaka na dada, na tumeendelea hivyo hadi leo. Basi hiyo siku jamaa alivyoniita (ilishapita miaka 4 na walikuwa na mtoto), kwa kuwa hatukuwa tumepanga lolote, "chale" likanicheza nikampigia "dada" simu, akanijibu hana habari kuwa mwenzie ana kikao nami, nikajua kuna mtego. Nimefika pa kukutania nikamkuta yuko peke yake, keshaagiza nyama choma na bia, tukaendelea. Akiwa ameshalamba bia nne za fastafasta (haikuwa tabia yake, nadhani alikuwa anaondoa nishai), akaanza kunihoji kipolisi, nimwambie ati mkewe nilishamlala mara ngapi?

Kama ni wewe ungemjibu nini "shemejio" huyo?

Kama nimekuelewa mahusiano yenu yalikuwa kabla hajaolewa hivyo hakuwa mke wa mtu, hivyo hukumlala mke wake bali ukimlala rafiki yako wa kike (girlfriend)endapo baada ya kuolewa uliendelea kumlala hapo ndo unahaki ya kutoa hesabu. Huo ni mtazamo wangu.
 
ningemlamba kibao halafu nikacheka kama chizi! hii ni kumuonesha kama yeye hajali hisia zangu basi mimi sijali taimz 2 into breketi kanikera sana.
 
.........Huyo mwanaume naye alikuwa na lake jambo, kwani kwa akili yake alifikiri watu huwa wanahesabu kwamba wamelala mara ngapi?
 
Hivi huwa mnajisumbua kuchunguza vya zamani vya kazi gani? Vinawasaidiaga nini kwani? Mie mnanibore
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom