Mr. Marangu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2013
- 1,566
- 1,516
Nipe namba ya shemu wako ntakua nampa na yakutolea...
Hizi ni salamu kwa watu wote wenye tabia hizi, reference ni shemeji yangu.
Shemeji yangu tabia yako ya kunipiga vizinga vya mara kwa mara inanikera sana, inanirudisha nyuma.
Wewe una ajira yako, mumeo ana ajira riziki kwenu sio shida, maisha yako/yenu sio shida. Tayari mshajenga na mumeo kashapata hadi kipando/gari la kutembelea.
Sina hakika kama bro anashindwa kutimiza wajibu wake wa kuhudumia familia ikiwemo mahitaji yako binafsi.
Siku za mwanzo nilizani ni shida tu ya ghafla na hukuwa na jinsi ukaamua kuniomba assist na bila hiyana nikakusave, ila kauli ambayo sikuielewa ni pale uniponiambia "hii inatakiwa iwe siri yetu" ili mumeo asijue kuwa unaombaga assist ukiwa na shida zako binafsi. Kwa kuwa sikujua dhamira yako nilikubaliana na kauli hiyo.
Vizinga vyako hivi vinanirudisha nyuma sana, tena huna haya unaomba na ya kutolea.
Nilitarajia watu wa karibu yangu kama wewe uwe unanishauri namna ya kusave na mbinu za kuongeza kipato badala ya kutegemea malipo ya malipo ya vibarua pekee ila imekuwa tofauti na ndio kwanza umepata mteremko wa kutatua shida zako binafsi ambazo kimsingi zinakuwa nje na bajeti yako ya kila siku ambayo jukumu la mumeo kuitekeleza na nina imani anaitekelza ipasavyo.
Nipumzishe shemu wangu na mimi nijikongoje, ulipofikia wewe ni mbali mimi bado nipo mwanzo.