Shemeji Yangu Kamkimbia Mumewe na Mwanaye, Kisa, Mzungu na Range-Rover!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shemeji Yangu Kamkimbia Mumewe na Mwanaye, Kisa, Mzungu na Range-Rover!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Muke Ya Muzungu, Mar 15, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ukistaajabu ya Musa, utashangaa ya Firauni. Shemeji yaangu mwenye Umri wa miaka 28 ambaye amekuwa kwenye ndoa ya miaka 5 na kakaangu, hivi majuzi amemtoroka mumewe, bintiye wa miaka miwili na hata kuacha kazi yake kwa ajili ya mzungu mzee (kibabu) Huyu kibabu ambaye ni meneja (mkandarasi) wa barabara, alikutana na shemeji yangu kwenye club moja maarufu hapa mjini. Mkandarasi huyo akawa anampa shemeji yangu hela nyingi na hapo kiburi na jeuri ikamuingia akaanza kumfanyia kaka yangu vituko. Ikawa nyumbani hakai, hata wiki nzima haonekani sababu yake ni kwend kwa dadake tandika. Matokeo mume akaanza kumshuku mkewe, na uvumilivu wake ukawa unapungua. Siku moja mumewe akiwa kazini, hii ni miezi mitatu zilizopita, huyu dada alirudi siku moja mchana na Range-Rover kapakia vitu vyake kwenye gari na kutokomea. Hakujali cha mtoto wala cha nini. Akapotea kwa muda sasa, lakini kwa bahati kuna watu wamekutana naye Morogoro na huyo mzungu na taarifa hizo zikamfikia kaka yangu. alijikaza kisabuni bila kumwambia mtu. Sasa cha ajabu, baada ya kumtukana mumewe kwamba hana hela, yule mzungu pia kampiga chini wiki mbili zilizopita. Pa kwenda hakawa hana. Huku kwa kaka yangu hatakiwi, alimtukana mumewe wa ndoa kwamba mwanamme gani wa kununua VITZ wakati wapo wa Range-Rover kitu ambacho kilimuumiza kaka yangu mno. Hapa tunapoongea, shemeji yangu hana pa kwenda, anajaribu kurudi pale alipomimina matusi. Wadau mnashauri vipi na huu ugonjwa wa wazungu unao kua kwa kwasi bongo. Huu ugonjwa wa vibabu vizungu kutoka na wake, watoto na binti zetu? ufanyweje, huu ni mjadala
   
 2. F

  FredKavishe Verified User

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hahahaha kazi kweli usitukane mamba kabla hujavuka mto
   
 3. s

  shosti JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  sasa hapokosa la nani,mzungu au shemejio na mmewe..
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  ampotezeeeeeeeeeeeee. Huyo hafai hata akimsamehe anaweza kupata mzungu mwingine tena kama huamini nenda kwenye website ya U-TURN
   
 5. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Huyu shemji yako, lazima atakuwa ni mfuasi wa blogu ya U-turn. Kule ndo chuo kikuu cha mababu wazungu cha muzumbe. Kili Janga wa Babu Ralph na Kisa Maliq, naye kamuacha mumewe na mwanaye kusaka mzungu kwa binti mangeleza wa uturn
   
 6. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,804
  Likes Received: 6,314
  Trophy Points: 280
  MGsalon - unataka nini kijadiliwe sasa?
   
 7. innovg

  innovg Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aachane naye tu, si alifanya hayo akiwa na akili zake timamu
  utauliwa kwa maradhi kisa huruma za ajabu
   
 8. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  huyo dada ni kicheche mnataka ushauri gani? tumpe amletee ngoma ndani mumewe ndio mtajua hafai??watu wengine sijui mkoje?:embarassed2:
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Kosa ni la kakako kumuwachia mkewe kwenda vilabuni.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Haya mambo huwa yapo! Ila naomba kuwa na moyo mkubwa wa kuhimili balaa la kukimbiwa au mke kuhamia nyumba ya jamaa mwingine kisa hela.
   
 11. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
 12. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  msiwalaumu wazungu hao bureeeeeeeeeeeee,jamani message sent kwa wakaka wa kiafrica/tanzania/weusi..wenzenu dada zenu tunataka marangeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!:lol::lol::lol::lol::lol::lol:
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mkuu ulivounganisha matukio na hizo picha,daaah we noma
   
 14. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Haswa ingekuwa kama mke anapenda disco ni heri kwenda na mumewe anakwendaje clabu na yeye mke wa mtu
   
 15. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Wanamuita forensic expert. Namuona mama kili na kati ya masaki na babu Ralph.....makubwa !!! Toba. Tunasubiri ya Kisa Maliq
   
 16. s

  shosti JF-Expert Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  si mfanye kazi ili msaidiane kununua hilo range,kwani mmepungua kiungo gani mpaka mnapenda vya kupewa:washing:
   
 17. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  hebu acheni kuendekeza dhiki nyie maisha yenyewe ya kibongo mnayafahamu ya kua tumetoka kwenye familia duni.
   
 18. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ooooh mbona kwa mzungu huambiwi hivyo?hayo ya kusaidiana hayapo,sie tunataka ya kupewa hutaki kunipa range nikienda kwa mzungu akanipa usimlaumu mzunguu!!!:lol::lol::lol::hatari:
   
 19. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  usijali sitakudai range mwaya,kwako nitadai kibajaji tuuuu :lol::lol::lol:
   
 20. s

  shosti JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mhh kazi kwelikweli kama nihivyo wanawake wote wenye wazungu wangekuwa na marange mpenzi...ila range nzuri ni ile unayojua uchungu wake japo kidogo bure ghalii:lol:
   
Loading...