Shemeji kuwa karimu. Tabia yako usijetulaumu shemeji zako (marafiki wa mmeo)

Mzee Mchochezi

Senior Member
Apr 3, 2018
126
242
Salaam wananzengo,

Jana nilisafiri kwenda kumtembelea rafiki fangu Fulani huko wilayani.

Jamaa kaja stand kanipokea, tumekwenda kwao, ile nafika nakutana na mama mtoto wake, daaah! Jinsi alivyonikaribisha tu, nikajua hapa kuna tatizo na jinsi jamaa yangu alivyo nikashangaa kwa nini azalishe demu mbaya kama yule hana mbele wala nyuma wakati kuna demu wake nzuri tu tena mkarimu kamzalisha yupo mkoani huko.

Baada ya muda nikaandaliwa ugali yaani unga mchungu kinyama, kidume nikavumilia nikala ule ugali mchungu na nyama nikamaliza.

Nikatoka na jamaa kwenda kusafisha macho, jioni tukarudi tukakalishwa nje yule mwanamke hakuwepo hadi muda aliorudi na hapo alipigiwa simu tupo nyumbani njoo ila akapotezea hadi alipojisikia kurudi mwenyewe.

Basi amerudi akaandaa dinner tukala mimi nikaelekea sehemu kulala, mwenyeji wangu akaniambia asubuhi utaenda home kunywa chai mimi nitaamkia kazini,nikamwambia poa.

Imefika morning nimejiandaa fresh naenda kwa shemeji nafika pale namsalimia kaitikia fresh, anaitikia nikakaa nione ukarimu wa shemeji yangu na nilifanya hivyo makusudi nione akili na ukarimu wake upoje, nikakaa kama dakika 15 hakuna chochote kinachoendelea nikamuaga Shem mimi ndio naondoka hivi so tutaonana siku nyingine Mungu akipenda ,akasema "Sawa Shem karibu"

Kumbuka hapo nimelala lodge na mimi ndio mgeni wao na nilifika kwa dhumuni la kuwatembelea wao,lakini cha ajabu ile asubuhi yule mwanamke hata kusema shemeji nimekuandalia chai kunywa uondoke hakuna.

Hivi kwa style hii ya nyie wanawake mlio kwenye mahusiano na marafiki zetu ,jamaa wakichepuka wakawasahau mtamlalamikia nani?

Maan yake sie marafiki ndio tunajuana tabia zetu tunafichiana siri lakini kama shemeji umekosa ukarimu kwangu unadhani nitakuonea huruma nikiona jamaa yako anachepuka? si ndio nitazidi kumchochea achepuke tu kwa sababu siwezi kumpa ushauri wa kumheshimu mke wake ambaye hajielewi hawaheshimu na kuwajali shemeji zake.

N.B: Sina shida ya chakula wala hela ya matumizi ila nilitegemea mimi kama mgeni basi nijaliwe mno na wenyeji wangu hasa shemeji yangu mke wa rafiki yangu ila nimetembelea kwa rafiki yangu ambaye akija kwangu mke wangu anamjali mno lakini mke wake kaonesha dharau ya hali ya juu na hajanijali kabisa kama mimi na familia yangu tunavyomjali mume wake anapokuja kwetu.

End of thread.
 
Ulivyoenda kuwatembelea mkuu ulibeba Nini au ulienda unapunga mikono? Hiyo moja, la pili kwanini unamuita dada wa watu mbaya? Umeambiwa umuoe wewe? Mwenyewe mwenye mke wake kamuona mzuri we kwann umuone mbaya? Na tatu la mwisho we ulishasema chakula Chao kibaya(ugali mchungu ka Nini) Sasa si ndio ungefurahi asubuhi hawajakupa kitu kichungu na kibaya Tena mkuu?

Anyways we muhimu umeenda kuwasalimia (Sana Sana kumsalimia jamaa yako) inatosha. Hujaenda kumthaminisha mkewe Kama mzuri au mkarimu au kula. Shukuru jamaa yako hajambo Basi inatosha.

Kaswali ka mwisho mkuu, we umeoa na unafamilia? Kama tayari umeoa, ungependa mkeo awe mkarimu Sana kwa rafiki zako? Sure?
 
Wewe pale cha muhimu rafiki ako, habari za shemeji ziache kama zilivyo, km mnasaidiana endeleeni kusaidiana na kuwa karibu, anapokuja kwenu kuweni na mioyo km mlivokuwa mwanzo, kuna watu awajui kuchangamka, kukaribisha, kupokea, yaan ule ucheshi haupo na unakuta sio mchoyo, km kipo utakula, km hakipo basi mnaangaliana
 
I can believe dat,manake nimeshangaa sana Mara ya kwanza kwenda kwa jamaa nimemkuta na mke wake Fulani alinikarimu vizuri sana tena sana halafu mwanamke ni mzuri mno na msomi sana na ana kazi yake, ila nimetembelea tena daa kituko,nisiongee mengi sana
Unaweza ukadhani shida ipo kwa shemeji yako kumbe shida ni rafiki yako, ya ndoani ni ngumu kuyajua
 
Back
Top Bottom