Shemeji kumlinda mdogo wa mke wake wa kike inaelewekaje?

skfull

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
2,944
2,376
Niliwahi kuwa na Mpenzi wangu ambae tulipendana sana lakini ikatokea kuwa kila anapochelewa kurudi nyumbani hata kwa dakika 10 basi shemeji yake huja juu sana
Siku moja Mpenzi wangu akaniomba kuwa bora ahame pale na kwenda kukaa kwao nikamwambia muda bado vumilia kwa muda mfupi nitakuambia cha kufanya
Hazikupita siku mbili akaja kwangu tukakaa Kwa muda wa masaa kadhaa nikampeleka kwao yaani Kwa shemeji yake nikarudi kwangu kupiga simu haipatikani SMS aiku mfikia nikajiuliza kuna nini wakati akitoka hapa cm ilikuwa chaji na imejaa? Nikatulia maana tuliaminiana sana kiasi cha kutomtilia shaka.

Asubuhi sana nikashangaa mtu anaingia kwangu sikuwa na tabia ya kufunga mlango nikiwa nimelala mwenyewe ndani kuangalia ni my love akaniomba niamke nkamuuliza kuna nini akanambia we amka ukaoge kabiandalia maji ya kuoga akanisindikiza kuoga kurudi akaandaa cha tukanywa,
Baada ya kumaliza kufungua vunywa akaniuliza hny Jana tulivyoachana ulinipigia nilamwambia ndiyo! Kasema mwenzako simu imevunjwa nikamuuliza nani kavunja akasema shemeji nikamuuliza tena kwanini eti kaniuliza natokea wapi kabla sija mjibu kanisogelea kapokonya cm na kuipigiza ukutani nimekuja kukupa taarifa usijesema nimekuzimia simu Mpenzi.

Mwanaume nikamwambia usijali tulia we nenda kazini jioni ukitoka utanikuta hapa nyumbani maana alikuwa anafanya kazi ya muda alikuwa anasubiri kwenda CHUO sasa yule shemeji MTU ni polisi traffic alitaka ampeleke CCP Mimi Kwa mipango yetu nikamwambia upolisi sitaki aende Kwa mapenzi yetu akaridhika tuakachagua kuwa aende ualimu nitampa saport tukaridhiana wote.
Jioni kutoka job kwake anakuta nimemletea cm ya kisasa maana ile ya kwanza ilikuwa ya kawaida nikamkabidhi cm yake baadae nikampeleka kule anapo kaa, hazikupita cku nyingi maana ilikaribia pasaka ya mwaka huu 2015 tukapanga mikakati yetu lakini cku moja kabla ya pasaka ikatokea mabadiliko kwanza mpnz wangu alikuja nyumbani mchana nikiwa nimetoka akaniuliza hny ukowapi na una hali ya kuumwa? Nikamwambia nipo hapa karibu na nyumbani akanambia njoo nipo home nikaja home nikamkuta kaka ndani anaangalia TV tukapeana salamu zetu pale.
Baada ya salamu akataka kujua nakula nini aniandalie nikamweleza akiwa anaandaa tunaendelea kuongea na yeye akiniomba kwenda na Dada yake kwao likini wanaenda na kurudi na baada ya kurudi itakuwa ni pasaka pili atakuja home tukakubaliana na baada ya kula aliniaga na kuondoka maana Dada yake alimpigia cm nikiwa na sikia akimuambia awahi maana anataka wafike mapema kabla ya jioni basi nikamruhusu Mpenzi wangu wote tukiwa na furaha akaondoka,

Dakika 20 baada ya kuondoka akaja rafiki yangu kama mdogo WANGU akanambia brother vipi hali yako nikamjuza hali yangu akaniomba Gari yake ikae pale kwangu maana yeye anasafiri nikamkubalia akaniomba nimpeleke stand na gari lake na nimpelekee carwash. Nikamfikisha stand nikaelekea carwash wakati nipo carwash nikaona Gari ndogo ipo mbele yangu naifahamu ni ya yule polisi traffic shemeji wa Mpenzi wangu Mara simu inaita natoa mfukoni naona 'my love' ndiye mpigaji nikapokea akanambia nakuona nikamuuliza ukoapi kanambia Kwenye Gari kweli kuangalia namuona yeye na Dada yake na mtoto wa dadaake dadaake ndiye anaendesha Gari yeye kakaa pembeni akanambia cc ndiyo tunaondoka hivyo nikamwambia sawa akaniuliza wewe c unaumwa unafanya nini hapo? Nikamwambia nipo na gari ya dogo nimemleta stand sasa inaoshwa ndiyo nirudi home karidhika mtoto wa watu mwenye mapenzi ya kweli kwangu.

Baada ya Gari kukamilika kuoshwa nilalipia na kuondoka wakati naoelekea nyumbani nikakutana na Gari ya polisi katika kupishana ile Gari ikawa kama inanifuata nikakwepa na baadae kaileta kabisa Kwa kasi wakati tunakaribia kupishana nikapata wazo la kiudereva kuwa hii gari Kwa ukaribu huu nikisimama nitagongwa Kwa mbele nitaonekana nimechomekea Gari ya polisi ss cha msingi niongeze mafuta kama dereva huyu hana akili anigonge ubavuni Kwa nyuma hayo ni mawazo ya sekunde moja Kwa professional driver!

Kweli nikaongeza mafuta mengi nikaponea chupuchupu nikapita na kuambuulia tusi zito toka Kwa Dereva wa gari la polisi nikafunga break Mara gafla yule Dereva akashuka kuangalia ni yule kijana shemeji wa Mpenzi wangu.
Kushuka Kwenye Gari na kunifuata na matusi yanaongezeka nikabaki nimeshikwa butwaa maana najiamini sijakosea kiudereva kuja akawahi kuzima switch ya gari nikasha tena nashikwa tai duh nikamsukuma kule katua na matako kucheki switch kachomoa key tayari kunyanyuka mwenzake kashasogea pale nilipo na kuniomba niwe mpole twende kituoni niasema sawa kaja kanibetua cm yangu kaifunga kakuta picha za shemeji yake kacharuka zaidi ya kichaa.

Nikapelekwa kituoni nikachezea virungu sana na kudai natembea na Mke wake kaona picha sasa baadae kidogo akaja mwenzake akawa ananitukana sana akachukua ile simu yangu kuangalia picha inayompa yule kijana hasira kuiona akaishiwa nguvu akamzuia yule shemeji MTU asiendelee kuniadhibu akamttoa pale chumba cha adhabu kidogo nasikia wakiteta Kuwa mbona unadai ni mkeo wakati ni shemeji yako? Akamwambia eti Mimi nimempa kiburi Sana yule binti sasa anataka anikomeshe na lazima tuachane hata Kwa kutumia uchawi.

Sikutilia maanani maana ukweli tulipendana sana na mipango yetu ilikuwa endelevu sana na baada ya mpenz kusikia nipo ndani alitaka kuchanganyikiwa akaleta shida sana nikatoka akaniambia kuanzia siku ile hatafika tena kwa dadaake tena na ikawa hivyo, tukaendelea na mawasiliano yetu vizuri na mipango safi sasa nikisikia eti uchawi utatumika kutusambaratisha niliona kama MANENO ya mkosaji lakini mpaka sasa nishapatikana maana baada ya wiki mbilili mbele Mpenzi wangu alinipigia cm siku moja ucku tukaongea saana baadae cm yake ikakatika nikampigia tukaendeleà kuongeaa saana akan iomba Kuwa nikikata cm nimfanyie lounge wa vocha nikafanya hivyo ndiyo ukawa mwisho wetu nilijaribu kweñda mpaka kwào nikamkuta alilia sana anasema anaona kama kichwake hakipo sawa japo ananipenda sana ila hajielewi nimwache kwanza tangu mwezi wa nne saivi cm zake zote hazipatikañi. Lakini Mara ya mwisho wezi wa sita alinipigia Na kunilaumu kuwa kimya na kuniaga anaenda CHUO morogoro ukweli nampenda sana lakini nilikuwa nikipiga cm anachukia sana
 
Pole ila kuna uwalakini let it be investigated then findings will suggest recommendation.
 
Nishapata mikwaruzano na mashemeji wa aina hii!! jamaa anakuwa mkali kwa mdogo wa mkewe utafikri ni mdogo wake wa damu au mkewe!!! Inafikia kipindi unajiuliza au huyu shemeji alikuwa anamla binti kabla yangu nini????
Nisha
 
Huyo shemeji yake alikua ana mpango wa kuzima taa.
Umenikumbusha ule wimbo wa mashemeji shemeji huku mwazima taa..... Inawezekana Trafiki alikuwa anataka kula kuku na mayai au pia jamaa ndie anamfanya demu kama mkewe hivyo jamaa kaamua kumwaga mboga, pia inawezekana amejiloga mwenyewe kwa hofu maana mlogaji hasemi zaidi anakufanya rafiki huku anakuuwa kimya kimya
 
hizo ni chuki na wivu wa shemeji ila kama mnapendana kweli mtashinda hayo yote hata shemeji aende kwa waganga wa nigeria
 
As long as hajamfanya shemeji yake chochote kibaya...amlinde tu!
 
anipige kisa demu tena shemeji yake tu kwangu angehama mtaa laa sivyo tungegawana majengo ya serikali mm jela yeye hosptal hakuna kitu kinachonikera kama uone dunian hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom