singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amesema kuwa hatua ya serikali yake kuimarisha huduma za afya vijijini ni sehemu ya utekelezaji wa shabaha ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kufikisha huduma bora za afya hadi vijijini kwa nia ile ile waliokuwa nayo waasisi wa Mapinduzi.
Shein alisema hayo katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Ikulu na Utawala Bora, Dk Mwinyi Makame Mwadini, baada ya kufungua jengo la wagonjwa wa nje katika hospitali ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Dk Shein alisema huduma bora za afya kwa wananchi wote bila ya ubaguzi ni miongoni mwa malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na kwamba chama cha ASP kilichoongoza mapinduzi hayo katika Ilani yake kiliweka bayana azma yake ya kutoa huduma za afya bure bila ya ubaguzi.
Alisema jitihada kubwa zimefanywa na serikali ya Zanzibar katika kipindi cha miaka 52 ya Mapinduzi katika kuimarisha huduma za afya kwa kutambua kwamba afya bora ni muhimu kwa wananchi ili waweze kuishi vyema katika kazi ya kuleta maendeleo ya nchi yao.
Alisema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa mipango na mikakati ya kuiendeleza sekta ya afya visiwani kupitia vitengo na programu mbalimbali zinazoendelezwa na serikali kwa ushirikiano na washirika wa maendeleo.
“Nyote ni mashahidi wa kuimarika kwa huduma za afya katika hospitali na vituo vyetu vyote vya afya... Aidha, kuna ongezeko kubwa la vituo vya afya vya madaraja mbalimbali kiasi kwamba hivi sasa wananchi wa Zanzibar hawawezi kwenda zaidi ya kilomita tano bila ya kukuta kituo cha afya,” alisema Dk Shein.
Akieleza historia ya huduma za afya katika Mkoa wa Kaskani Unguja, Dk Shein alisema kabla ya Mapinduzi mwaka 1964 katika mkoa huo kulikuwa na vituo viwili tu vya afya ambavyo vilikuwepo Mkokotoni na Chaani.
Alisema katika kipindi cha miaka 52 ya Mapinduzi, Mkoa huo hivi sasa una vituo vya afya 26 ambapo vituo 18 ni vya daraja la kwanza na saba ni vya daraja la pili. Kadhalika alisema kuna hospitali ya Koteji ya Kivunge ambayo lengo la Serikali ya awamu ya Saba ni kuipandisha daraja kuwa hospitali ya wilaya.
Dk Shein alisema kuwa lengo la mradi huo ulioanza mwaka 2012 ni kuziimarisha huduma za afya katika hospitali zote za Koteji ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Alisema serikali imekusudia kuzisogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi, ikiwa ni pamoja na huduma za upasuaji kwa kinamama wajawazito na huduma za uchunguzi. Alitumia pia fursa hiyo kutoa shukurani za dhati kwa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Uingereza HIPZ, Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na ROTARY Club kwa kuiunga mkono serikali katika juhudi zake za kuimarisha hospitali hiyo.