Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,800
- 34,189
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amemtaka Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuikosoa Serikali yake pasipo kuvunja sheria za nchi.
Akizungumza jana Ikulu mjini hapa wakati akiadhimisha mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani kupitia uchaguzi wa marudio wa Machi 20 mwaka jana, Dk Shein alisema Maalim Seif ana uhuru wa kusema akitakacho wakati wowote, lakini asitumie lugha za matusi.
Dk Shein alisema kuna maneno mengi yamekuwa yakisemwa mitaani juu ya kuwapo kwa Serikali nyingine badala ya anayoiongoza, kauli alizosema hazina mashiko.
Alisema njia ya kupata Serikali ni mbili tu duniani kote, ya kupigwa kura au kufanyika mapinduzi kwa upande unaoona umedhulumiwa.
Chanzo: Mwananchi