Shein awatupa vijana. Kikwete jifunze.

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,405
2,953
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Kanal Mstaafu Miraji Mussa Vuai kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Idara Maalum Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee amesema kuwa uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais chini ya kifungu 34(4) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Zanzibar no.2 ya mwaka 2011.

Hoja

Unajua katika ulimwengu ulioendelea serikali au viongozi wa serikali huwa wanapigia kelele sana juu ya ajira na maendeleo ya vijana katika nchi zao.Sasa utakuta huku kwetu yaani Zanzibar ni kinyume chake.Katika uteuzi wa baadhi ya nafasi nadhani ingeliwezekana kuteuwa vijana wenye uwezo wa kuzitumikia nafasi hizo badala yake vijana wamewekwa mbele katika mambo ya kisiasa ambayo kwa vijana hutumia jazba zaidi kuliko hikma.Miaka ya karibuni nilipata kutembelea maeneo ya mashamba na ng’ambo niliweza kuona jazba na malumbano ya siasa either baina ya wanachama wenye itikadi moja na pia wenye itikadi tofauti ambao hawatumii ujuzi wa kuyatafakari matatizo ya nchi kama vile uchumi na maendeleo ya elimu bali ni kulumbano katika mambo kwa upande wangu hayaingii akilini.


Well…ningependa kutoa mfano kutoka nchi ya BOTSWANA.Hii nchi imefanya mabadiliko mengi sana katika ajira.Vijana wamepewa kipaumbele katika sector zote.Hata ile muhimu kama vile ya kidiplomasia basi utakuta vijana wengi katika balozi zao ndio wenye nafasi za juu.Mwanzoni mwa mwaka 2000 niliwahi kukutana na M’botswana mmoja katika kiji mkahawa huku ughaibuni.Nilikua nimeketi katika kiji counter napata kiburudisho na huku Euro football match inaendelea.Alitanabahi kuona kuna mweusi mwenziwe na alikuja ungana na mimi.Tulisalimiana na tukawa tunaulizana masuala ya kijamii na mengineyo.Katika maswala niliyomuuliza moja ni”hivi wewe ni mwanafunzi au uko kibiashara?” mana nilikwisha jua kwamba Wabotswana si aghlabu kutoka nje ya nchi yao kutafuta ajira mana maisha yao ni mazuri mno kulinganisha na nchi nyengine za kiafrika hususan Zanzibar.Jibu alilonipa yule bwana nilibwata mdomo wazi nikawa mduuuuchu!..yule bwana alinijibu”I’m a diplomat..as a first secretary of economy”…..lililoniwacha mdomo wazi sio hilo tu bali yule bwana alikua na umri wa miaka 27 tu!

Sasa tuone kwetu kama kijana wa umri wa miaka 27 kama ataipata nafasi kama hiyo hata kama yuko na uzowefu nayo.

Ninachotaka kusema ni kwamba sio vibaya kuwaweka wazee waliostaafu katika utendaji wa kazi lakini tutumie njia nzuri za kuwatumia mana najua wako wengi wao wenye uwezo na ujuzi wa kutoa michango yao katika nchi.
Kwa mfano kungelikua na Advisory board kwa wale wote wastaafu ambao wanaonekana bado wanaweza kutoa mchango wao katika serikali basi wangewekwa katika hii board.Kama vile kaitka mambo ya:-
elimu
finance
health
infrastructure
engineering
sociology
religion
Agriculture&fisheries….nk
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom