Shein awashukia wapinga Muungano

KIGENE

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,552
813
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimeendelea kusisitiza msimamo wa kutetea na kupigania Muungano wa serikali mbili na kuvionya vyama vingine kuacha kukisemea.

Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, alisema jana mjini hapa katika mkutano wa wajumbe Baraza la Wazee wa CCM.

Alieleza kuwa CCM haina agenda ya kuvunja Muungano au kuwa na muundo wa serikali tatu au nne badala yake itaendelea kutetea na kuufanyia maboresho muundo uliopo.

Alisema pamoja na Tanzania kuwa na vyama vingi vya siasa kila chama kitabaki na sera zake hivyo kila upande una wajibu wa kulinda na kuheshimu matakwa na misimamo bila ya kushurutishwa.

"CCM haina agenda ya kuvunja Muungano ulipo na wala sheria iliyoanzisha mchakato wa katiba na ukusanyaji maoni haina kipengele kinachoeleza Muungano uvunjike" alisema Dk. Shein.

Alisema CCM haitoyumba wala kuyumbishwa na kundi, watu au misimamo ya vyama na kukiuka taratibu ilizojiwekea kwa kufuata mkumbo au soga za watu wengine.

Aliwahakikishia wana CCM wenzake kuwa amechaguliwa na wananchi ili kulinda usalama wa raia na mali zao hivyo hatakubali kuona amani na utulivu vikichezewa na kikundi chochote.

"Ole wao wanaotumia fursa ya kutoa maoni na kuleta ghasia, hakuna cha uamsho wala mlalo…" alisema na kuongeza
"Hakuna matabaka ndani ya CCM, hakuna mwanachama wa daraja la kwanza wala la pili wote wana haki na hadhi inayofanana mbele ya katiba ya chama chetu"

Akizungumzia Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Dk Shein alisema hiyo ni ajenda ya Serikali za CCM ambayo ilipitishwa na kufuata taratibu za vikao kwa lengo la kuendeleza umoja na kuleta utulivu wa kisiasa.

Hata hivyo, alikiri kuwa uharaka wa kuelekea katika muundo wa SUK uliwastukiza wananchi hususan wanachama wa CCM hivyo ipo haja na ulazima wa kuanza kuwaelimisha na kuutambua mfumo huo.

Akizungumzia mkakati wa serikali kuchukua hatua za kukabiliana na aina yoyote ya ghasia na fujo, aliwaeleza wananchi kuwa yeye ndiye Rais hivyo atatumia sheria ziliopo na kufuata taratibu ili kuhakikisha amani na usalama wa watu.

Source : Nipashe Jumapili
 
Ili Muungano upate uhalali na ridhaa ya Wananchi na kuepukana na chokochoko zote hizi, kura ya maoni ni muhimu sana ifanyike Zanzibar ili kujua ni wangapi wanaunga mkono Muungano!

Kamatakamata kwa kutumia Polisi na Jeshi au CCM kutisha wananchi sio dawa mujarabu kwa kuimarisha Muungano na kudumu kwake kutakuwa ni muda tu! hivyo chondechonde Serikali ya Shein na Serikali ya Muungano tunawaomba kuzingatia hili mapema vinginevyo itafika siku Wananchi watasema basi liwalo na liwe!
 
Dr. Shein hawezi kupingana na wakati,nakumbuka hata komandoo aliwahi kuwaweka ndani kina juma duni na wenzake leo wako wapi?huyuntutakuja kumuweka hadharani rekodi zake, mabadiliko wakati wake umefika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom