Shein ateua wawakilishi, wamo wawili kutoka CUF


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,975
Likes
5,344
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,975 5,344 280
Shein%201%2819%29.jpg

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed SheinWakati wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanatarajiwa kuapishwa leo, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, ameteua wajumbe wanane wa Baraza la Wawakilishi, akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Juma Duni Haji.
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ibara ya 66, Rais wa Zanzibar amepewa uwezo wa kuteua watu 10 kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wakiwemo wawili kutoka kambi ya upinzani.
Taarifa ya Ikulu Zanzibar iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi, Abdulhamid Yahya Mzee, imetaja walioteuliwa kuwa ni Juma Duni Haji, na aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Fatma Ferej Abdulhabib kutoka CUF.
Wengine ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano, Omar Yussuf Mzee, aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano, Balozi Seif Ali Idd na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisia:link { }
ya Rais (Kazi Maalum), Zainab Omar Mohammed.
Dk. Shein pia amewateua aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Katiba na Utawala Bora), Ramadhan Abdalla Shaaban, aliyekuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud, na mtaalamu wa masuala ya afya Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya.
Wajumbe hao walioteuliwa na Rais, leo wanatarajiwa kuungana na wenzao 71 kutoka majimboni na viti maalum katika kuchagua Spika wa Baraza hilo pamoja na kuapishwa na Spika huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana huko katika ukumbi wa ofisi mpya za Baraza hilo, Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ibrahim Mzee, alisema kikao hicho kitaanza saa 3:00 asubuhi kwa uchaguzi wa Spika. Spika mpya atakula kiapo na baadaye kuwaapisha wajumbe wa Baraza.
Mzee alisema katika mkutano wa Baraza hilo la nane pia wajumbe watachagua wajumbe watano wa Baraza hilo ambao watawakilisha Baraza hilo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Aidha, alisema kwa mujibu wa marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar, wakuu wa mikoa mitano ya Zanzibar hawatakuwa tena wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Katika hatua nyingine, Wajumbe hao mapema leo wanatarajiwa kumchagua Spika wa Baraza kabla ya kuapishwa rasmi huko katika ukumbi mpya wa Baraza hilo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Waliopendekezwa na vyama kuwania nafasi ya uspika wa Baraza la Wawakilishi ni Pandu Ameir Kificho (CCM) na Abas Juma Muhunzi (CUF), ambao watapigiwa kura na wajumbe wa Baraza.
Wakati huo huo, Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) imetangaza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 31.


CHANZO: NIPASHE
 
F

Fishyfish

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
231
Likes
0
Points
0
F

Fishyfish

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
231 0 0
CUF is CCM - 2, so this comes as no surprise.
 

Forum statistics

Threads 1,235,381
Members 474,523
Posts 29,220,560