Shein ateua mawaziri wa mseto wa ccm na cuf

Firdous

Member
Apr 27, 2009
42
0
Salma Said, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein ameteua Baraza la Mawaziri la serikali ya umoja wa kitaifa lenye mawaziri 25 kutoka vyama viwili vikuu visiwani humo.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar jana ilieleza kuwa uteuzi wa mawaziri hao 15 kutoka CCM na 10 kutoka CUF unaanza mara moja na kwamba wataapishwa leo jioni katika Viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.

Rais Shein amewateua mawaziri hao kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42 (1) na (2), 43 (1) na (2) na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

Dk Shein ameunda Wizara 16 na kuwateua Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mawaziri na Naibu.

Walioteuliwa ni Dk Mwinyihaji Makame (Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi), Omar Yussuf Mzee (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais: Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo) na Haji Omar Kheri Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora).

Wengine na wizara zao katika mabano ni Fatma Abdulhabib Fereji (Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais) na Mohammed Aboud Mohammed(Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais).

Aboubakar Khamis Bakary (Waziri wa Katiba na Sheria), Hamad Masoud Hamad (Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano) na Ramadhan Abdulla Shaaban (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali).

Juma Duni Haji anakuwa Waziri wa Afya, Zainab Omar Mohammed (Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake na Watoto), Abdilahi Jihad Hassan (Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo) na aliyekuwa Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna anakuwa Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati.

Pia wapo Mansoor Yussuf Himid (Kilimo na Maliasili) Nassor Ahmed Mazrui (Biashara, Viwanda na Masoko), Said Ali Mbarouk (Mifugo na Uvuvi) na Haroun Ali Suleiman (Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika).

Mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu wa Baraza la Mapinduzi ni Suleiman Othman Nyanga, Haji Faki Shaali na Machano Othman Said.

Naibu Mawaziri walioteuliwa ni: Issa Haji Ussi (Miundombinu na Mawasiliano), Zahra Ali Hamad (Elimu na Mafunzo ya Amali), Dk Sira Ubwa (Afya) na Bihindi Hamad Khamis (Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo).

Wengine ni Haji Mwadini Makame (Ardhi, Makazi, Maji na Nishati) na Thuwaiba Edington Kissasi (Biashara, Viwanda na Masoko).
 

Nono

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
1,475
2,000
Hii inawezekana Afrika tu! Nchi yenye watu wasiozidi Milioni moja mawaziri 25. Hii ni wastani wa waziri mmoja kwa kila wananchi 40,000. Mnategemea uchumi wa nchi zetu utakuwa vipi tunapokuwa na walaji wengi kiasi hiki? Hebu tujiulize ofisi moja ya waziri inakuwa na wafanyakazi wangapi ambao sio wazalishaji zaidi ya kuponda tu keki ya taifa? Mimi nadhani kwa Zanzibar ingekuwa na wizara takribani 8 tu, ambapo wangelipunguzia sana taifa matumizi yasiyokuwa ya msingi na kuimarisha huduma za jamii.

Haka kanchi kadogo, wawakilishi 50 kabla ya viti maalum, na hapo 1:2 anakuwa waziri. Wabunge 50 kabla ya viti maalum. Achilia mbali wakurugenzi, makamishna/manaibu na mazagazaga mengine, yet wanajidai wanataka kuiendeleza nchi, kwa kutumia nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom