Shein asukumwa Z'bar kuwapisha Urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shein asukumwa Z'bar kuwapisha Urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 24, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,189
  Trophy Points: 280
  Mwandishi Wetu
  Raia Mwema
  Juni 23, 2010

  [​IMG]Nia ni kufuta ndoto ya Wazanzibar kutawala Bara
  [​IMG]Hakuwa chaguo la wanamtandao mwaka 2005
  [​IMG]Lowassa, Mwandosya, Membe, Masha watajwa kuwania


  HATUA ya Makamu wa Rais, Dk. Dk Ali Mohamed Shein kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais wa Zanzibar, imeelezwa kusukumwa na wagombea Urais wa Jamhuri walioko Bara, Raia Mwema limeelezwa.

  Raia Mwema limefahamishwa kwamba, ukimya wa Dk. Shein na kutokuwa kwake na makundi, pamoja na elimu yake, kungemfanya kuwa Rais wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kama akiendelea kufanyakazi Bara kwa miaka mingine mitano ijayo.

  “Wanaowania Urais kumrithi Kikwete wana nguvu sana, na sasa wanajipanga kwa kila njia…. Unajua Dk. Shein hakuwa chaguo la wanamtandao lakini kutokana na nguvu ya wazee na nguvu ya Mkapa (Benjamin Mkapa, Rais mstaafu), Kikwete alilazimika kumpendekeza,” anasema kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM Zanzibar.

  Kwa mujibu wa kiongozi huyo ambaye ni kada wa siku nyingi wa CCM, Dk. Shein hakuwa na nia kabisa ya kuwania nafasi Zanzibar, pamoja na kuwa ni mmoja wa wanasiasa waliowahi kusukumwa kuchukua fomu mwaka 2005 kumrithi Mkapa, lakini heka heka za wakati huo zikaonekana kuwa nzito kwake kabla ya kuamuliwa kuendelea kuwa Makamu wa Kikwete.

  “Baada ya Mkapa kumaliza muda wake, ilikuwa ni zamu ya Zanzibar kutoa Rais na Dk. Shein alitajwa sana kuweza kuchukua nafasi hiyo kwa kupanda kutoka Makamu wa Rais, lakini kilichotokea kila mtu anajua, maana Dk. Salim Ahmed Salim ambaye alibaki katika tatu bora alikwisha kushughulikiwa na wanamtandao.

  “Baada ya Dk. Salim kukwama, na Dk. Shein kutojitokeza mwaka 2005, hatua ya kuendelea kuwa Makamu wa Rais, ingemfanya kuwa na uzoefu wa miaka 15 na kwa uwezo wake na uadilifu, isingekuwa jambo rahisi kumnyima urais wa mwaka 2015 maana Wazanzibari wasingeelewa japo hata sasa kuna kazi kubwa kwao kuzuia Mzanzibari,” anasema mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kutoka Zanzibar.

  Wanasiasa wanaotajwa sana kuwania kumrithi Kikwete na ambao wanaelezwa kuwa na nguvu kubwa ni pamoja na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ambaye sasa ameanza kutajwa kama mstaafu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi. Anatajwa pia Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

  Taarifa zinasema wanaomsukuma Dk. Shein kwenda kuwania Zanzibar, wamepania kwa nguvu zote kukabiliana na vikwazo vilivyoanza kujitokeza kikiwamo kile cha kudai kwamba hana kitambulisho cha ukaazi cha Zanzibar na hakujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura Zanzibar, mahali ambako atalazimika kupigiwa kura bila kupiga.

  Lakini akichukua fomu ya kuwania kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar juzi, Jumatatu, mjini Zanzibar, Dk. Shein alisema kwamba hakujiandikisha kupiga kura Zanzibar kwa zaidi ya chaguzi mbili sasa, lakini huko si kuvunja Katiba wala sheria za uchaguzi na kumuondolea sifa ya kuwa Rais wa Zanzibar.

  “Wapo watu wanasema hivyo kuwa mimi sijajiandikisha kupiga kura Zanzibar ...nimekutupa kwetu....Si kweli, mimi naongoza kwa kuwasaidia wananchi wa kwetu Mkanyageni na wale ambao hawajui Katiba wakasome wasikurupuke tu,” alisema.

  Alisema ameingia katika kinyang’anyiro hicho kwa utashi wake mwenyewe, pamoja na kuwapo taarifa za karibu kabisa kwamba hakuwa amejiandaa kabisa kuwania nafasi hiyo.

  “Namalizia kwa kusisitiza niliyosema mwanzoni kuwa uamuzi huu nimeufanya mwenyewe baada ya kutafakari kwa makini na kupima uwezo wangu na kuzingatia mapenzi kwa chama changu na kwa Zanzibar na imani ya wana CCM wenzangu waliyonayo kwangu. Hakika nimetiwa moyo sana na imani na mapenzi hayo,” alisema Dk. Shein katika hotuba yake ambayo imechapwa kwa kirefu ndani ya toleo hili.

  Dk. Shein amekuwa akitajwa kuungwa mkono na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Karume anayemaliza muda wake, lakini kumekuwa na ukimya kumhusisha Rais Kikwete na uamuzi huo pamoja na kujengwa imani kwamba naye anaunga mkono.

  Hata hivyo, taarifa za Karume kumuunga mkono Dk.Shein zimeanza kutiwa doa na wafuasi wa mgombea mwingine wa Zanzibar ambaye naye alichukua fomu juzi, Dk. Mohamed Gharib Bilal, ambao wanasema kwamba hatua hiyo ya Karume ni sawa na “undumakuwili” kwa kuwa Dk. Salmnin Amour alipomuunga mkono Dk. Bilal alidaiwa kwamba anataka kujenga himaya yake na hivyo kusababisha kuachiwa kwa Karume kuwa mgombea wa CCM.

  “Huu ni undumakuwili, Salmin alipokuwa anamaliza muda wake, alimtaka Dk. Bilal lakini akaambiwa anataka kuweka himaya yake, lakini sasa kwa Karume kumtaka Shein ni sawa… na sisi tunaona anataka kuweka mtu atakayelinda maslahi yake, awaachie Wazanzibari waamue baada ya yeye kumaliza muda wake,” anasema shabiki mmoja wa Dk. Bilal.

  Wengine waliochukua fomu mbali ya Shein na Bilal ni Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud ambaye alisema Zanzibar hivi sasa iko kwenye mazingira mazuri zaidi kuliko nyakati nyingine zozote katika historia yake na hivyo anaamini kuwa anaweza kuiendeleza na kuahidi kuendeleza malengo ya maridhiano kwa amani na utulivu wa visiwa hivyo.

  Mgombea mwingine ni Balozi wa Tanzania Italia, Ali Karume ambaye alisema pamoja na kuwa anaunga mkono maridhiano, lakini suala la kura ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa ya ndio au hapana hawezi kutaja msimamo wake kwa kuwa kura ya maoni itategemea wakati husika.

  Kwa upande wake, Dk Bilal ambaye ni mtaalamu wa fizikia aliahidi kusimamia suala zima la elimu na afya na kusema kwamba endapo Wazanzibari watampa ridhaa ya kuongoza ataendesha nchi kwa misingi ya utawala wa sheria huku akisisitiza suala la nidhamu.

  “Najua kisasi ni haki, lakini mimi alipoingia Rais Amani hajanifanyia kisasi chochote kwa hivyo wananchi wasiwe na hofu juu ya hilo, sitalipiza kisasi,” alisisitiza Dk Bilal.

  Alisema kwamba msimamo kuhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa itategemea matokeo ya kura ya maoni itakayopigwa Julai 31, mwaka huu, lakini kimsingi anakubaliana na hali ya amani iliyopo.

  Kamishna wa Elimu na Utamaduni, Hamad Bakari Mshindo ambaye naye anawania urais wa Zanzibar alisema kwamba Zanzibar inahitaji mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuleta maendeleo ikiwemo elimu.

  Kwa upande wake mgombe mwingine, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, alisema msimamo wake katika kura ya maoni yeye binafsi anataka iwepo amani, lakini katika hilo ni vyema Wazanzibari wakafanya maamuzi ya busara yenye kuendeleza umoja na mshikamano.

  Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamhuna alisema uadilifu wake katika chama chake na Serikali ndiyo nguzo yake kuu katika kuwania nafasi hiyo.

  Jumla ya wagombea wanane juzi walichukua fomu huku Waziri wa Elimu ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman akitarajiwa kuchukua fomu yake siku ya Alhamisi wiki hii na mfanyabiashara maarufu, Mohamed Raza akiliambia gazeti hili wakati tukienda mitamboni kwamba naye amekubaliwa na CCM kuchukua fomu ya urais kesho.

  “Nilikuwa safari. Lakini nimerudi nikakuta barua ya kukubaliwa kwenda kuchukua fomu. Kwa hiyo kifupi ni kwamba nami nimeingia katika kinyang’anyiro,” alisema Raza ambaye mwaka 2005 alinusa na kisha kujitoa katika mchakato kama huu.

  Aliongeza: “ Naijua Zanzibar. Nimetembelea majimbo yote.

  Nilikuwa mshauri wa Rais kwa miaka 10. Naujua Muungano vizuri, nikipita biashara zangu zote nitaacha kwa kuwa sitaki kuchanganya mambo haya. Lengo kubwa litakuwa ni kuweka umoja.

  “ Sitavumilia unafiki, wala hamtawaona ndugu zangu serikalini na nitainua maisha ya wenye hali ya chini kwa kutoa huduma bora za afya, maji na elimu. Lakini kama maamuzi ya chama yatakwenda kinyume na matarajio yangu, nitayaheshimu .”

  Hayo yakiendelea, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhamed Seif Khatib ambaye amekuwa akitwajwa sana kuwa ni miongoni mwa waliomo katika orodha ya watakaowania urais Zanzibar bado hajatangaza nia hiyo.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mhh! Kuna ka ukweli kidogo lakini Wazanzibari wenyewe hawaaminiki na ni watu wa ajabu sana -- kwani wenyewe kule walisaidia sana kuhakikisha dr Salim asipate urais wa muungano mwaka 2005, ingawa ilikuwa waziwazi kwamba ilikuwa ni zamu yao. Hawakui-grab nafasi hiyo kwa sababu za kipuuzi tu -- za kihistoria!

  Ni kweli kwamba Dr Shein, kama aikendelea kuwa Vice Pres had 2015 angekuwa mtu safi kabisa kuwa rais wa Muungano kutokana na uadilifu, uzoefu na kmutokuwa na makundi. Lakini hii ni ndoto kwani Watanzania wamezoeshwa kufanyiwa uharamia tu kupatiwa kiongozi wao mkuu, na mara zote mchakato wa uteuzi utokanao na vitendo vya kiharamia hutoa kiongozi haramia! Sorry to say this.

  Binafsi nilikuwa nategemea kuwa na rais wa muungano wa aina ya dr Shein mwaka 2015, lakini uharamia bado umejikita katika CCm na atakayekuja atakuwa even worse. Pengine zaidi ya huyu wa sasa, huyo atakayekuja atatumia muda wake mwingi, resources etc kujiwewka sawa kuliko kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Nyie mtaona tu!

  Swali sasa ni kwamba wale wanasiasa wa Unguja watakubali Dr Shein, kutoka Pemba angalau kuwa Rais wao? Swali gumu.
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Niliwasoma jana RaiaMwema. Kwa hili nadhani hawako sahihi sana. Kinyume chake, Dr Shein anaonekana hataimudu nafasi ya Urais wa Muungano na hivyo amewekwa kando ili kumpisha mtu mwingine ambaye ni mwanasiasa wa kweli kwa vigezo vya CCM.

  2015 Rais wa JMT atatoka Zanzibar kwa sababu ya minyukano na kuharibiana kutakakoendelea huku Bara.
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ukweli ni kwamba kina Lowassa, wanajiandaa, hakuna wa kuwazuia maana hata hao kina Karume wamewekwa na hao hao. Hakuna tena Mzanzibari, na ikitokea ujue ni mtu wa aina ya Masauni thena anaang'olewa kumuachia "Beno Malisa" wao na "Riz" Wakiongoza
   
 5. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mwanahalisi wao wanamuona kuwa Kikwete atamteua Karume kuwa Makamu wake na ndiye atakuwa Rais ajaye. Jamani sitoshangaa kwa JK lakini tutafakari. Karume amekuwa Rais wa Zanzibar kwa miaka kumi, kwa Wazanzibari wanajua kilichotokea huko katika masuala ya kodi na mafuta japo sasa wapinzani wamemuaona kama "mkombozi" wao (ni mjadala mpana). Sasa kwa ilivyo baada ya miaka kumi ya URAIS wa Zanzibar aje kuwa Makamu wa RAIS kwa miaka mitano halafu aje kuwa RAIS kwa miaka kumi (2015-2025)!!!!! Jamani tusiwe wavivu wa kufikiri, na Watanzania si MABWEGE TENA. Huo USULUTANI wa kuwa hakuna afaaye kuwa RAIS ila ukoo wa Karume na kadhalika umepitwa na wakati. Halafu kwamba Shein hakuwa anafaa kuwa RAIS linatoka wapi? Ina maana Karume ni bora kuliko Shein? ama Muhamed SEIF KHATIB ni bora zaidi ya Shein? Huo ndio uzezeta wetu. Shein anaweza kuwa hafai lakini si kama Karume jamani, japo kwa nchi hii na chini ya JK lolote linaweza kutokea hata kama tairi za gari zitachomoka.
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Jamani, Lowassa pamoja na ujasiri wote alionao hawezi kuchukua fomu ya kugombea Urais. Na hata akichukua, atafanyiwa kama mzee wetu JSM. Hili analijua na ndio maana hata 2005 alimtanguliza JK.
   
 7. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Magazeti haya haya yaliandika mambo mengi kuhusu uchaguzi wa urais Tanzania 2010. Mimi nilianza hata kuamini kwamba kuna watu watampinga JK mwaka 2010. Kumbe ulikuwa mwendelezo wa kutudanganya Wadangayika.

  Sasa ya 2010 yako wazi, wameanza kuhamia mwaka 2015. Jamani tuhurumieni wenzenu na acheni kutudanganya. Naona lengo hapa ni kuuza magazeti tu.
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Magazeti hayasemi, ila hao wanasiasa ndio wanaosema ama moja kwa moja ama kwa njia ya pembeni. Hata mtu akiua ikiiandikwa, si gazeti lililoua
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  MS, hamtelekezi kwani ana fadhila za kulipa, akithubutu tu amekwisha. Sasa ndo wakati wake wa kukutwa na ANGUKO KUU!!!
  :dance:
   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mods, hizi za Umakamu ziunganishwa
   
 11. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaaazi kwelikweli!!
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Siasa bwana uongo uongo tu. Anyway naona sasa ni muda muafaka wa kuyauza magazeti yao mara Karume VP, mara Dk Salim, mara Khatib mwishoe mtasema VP Dr Mwinyi. sasa sijui mwisho wake itakuwa nini. Maana kuna akina Pinda?, Membe, etc naona nasikia wanataka urais 2015. Hasa Benard Membe nasikia anaandaliwa for presidency.
   
 13. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  :dance:Ni Karume yupi wanayemzungumzia?mbona siwaelewi nyie watu.Kule Zanzaibar kuna wakina Karume wengi tuu wako wengine kwenye balozi zetu huko nje sasa ni yupi hasa ambaye anakuja kuwa makamu wa rais?Naona mmeshaanza kampeni ole wenu Takukuru wawakamate kama wale jamaa wa chama cha.......
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Jun 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mungu apishilie mbali kansa ya uongozi itakayokuja kuimaliza Tanzania kama hao walitjwa ndio aspirants wa kiti cha urais wa jamhuri ya Tanzania. Nina imani Dr. Shein angeweza kuwa Rais mzuri wa Tanzania kuliko takataka nyingi ninazoona hapo juu.
   
 15. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kichuguu umenena sana
   
 16. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Anayetajwa UMAKAMU WA RAIS NA URAIS WA JAMHURI BAADA YA JK NI KARUME AMBAYE SASA ANAMALIZA MUDA WAKE WA URAIS ZANZIBAR, YAANI HAWEZI KUKAA NYUMBANI KAMA MSTAAFU, NA BAADA YA MIAKA MITANO HAWEZI TENA KUPUMZIKA MAANA ANAHITAJIKA KUENDELEZA MEMA ALIYOANZISHA. JAMANI MAANA YA KUWEKA UKOMO WA URAIS (MIAKA KUMI) NI KUEPUKA HAYO MAMBO YA WATU KUONA KWAMBA UTAWALA NI HAKI YAO PEKEE
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kichuguu unajua kuna msemo unasema Simba mwenda kimya ndie mla nyama. Mie nashangaa watu wanasema eti Shein Mkimya nikiuliza amefanya kazi hajafanya? hamjibu. Nikiwauliza je si muadilifu jibu napata ni muadilifu. Je kazi ya UVP anaiweza au la jibu anaiweza sasa kwanini asiwe rais. Binafsi namuona Shein ni better off kwa CCM wakamteua yeye kuliko hao wengine kwani wananuka ufisadi na I donot trust them hata kama wakikoga maziwa!!!!
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwani lazima awe rais wa Jamhuri ya Muungano??? Ameshakula vya kutosha Zanzibar akijilimbikizia viwanja mpaka akapewa ubatizo "Mr hapa pangu". Amejaza ndugu zake kibao Benki Kuu hata kama hana degree aajiriwe kamuuliza Juma Reli anakoma na kukubali UDG kwa adha anayoipata!!! Sasa anataka urais wa Jamhuri wa Muungano aendelee kula??? au ndio ile mikataba ya uchimbaji wa mafuta wanataka kuiweka sawa maana Tanzania Bana!!!!! Vitu vingi vinaendelea nyuma ya pazia watanzania wanakuja kujua watu washamaliza kila kitu
   
 19. bona

  bona JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  nadhan si sahihi, yeye amepushiwa ule ili tu amkandamize bilal ambaye ana support ya wengi kule zenji hasa unguja, hata maskani zote, wazee na vijana kule unguja wanamlilia kwani uyu ndie kiongozi anayeongoza kuhakikisha siasa za karume wa kwanza zile siasa za chuki na ubaguzi dhidi ya wote ambao sio decentant wa ASP! yeye muasfaka na cuf hautakuwepo na chuki itarudi palepale! kwa muungano ni obvious hao wote kutoka zenji wala mliowataj hawawezi kua marais kwani, nchi ii tunabadilishana urais pia kwa kigezo cha dini! rais ajaye baada ya kikwete lazima awe mkristo so chances za zenji kutoa rais ni slim! na ccm watafanya kosa kubwa ambalo watajuta kama baada ya kikwete wasipompitisha mgombea mkristo! aya mambo ni hayaweki wazi kwenye majukwaa ila yapo na yanafuatliwa chinichini kwa sana na watu wengi!
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wapi katiba inasema rais wapishane kwa imani zao za kidini??? Ila navyojua mie zamani kulikuwa na kipengele kuwa Rais miaka kumi bara kumi zanzibar. Kikwete hakutakiwa kuwa rais sasa hivi ilikuwa zamu ya Dk Salim ila uhafidhina wa mtandao ukamaliza hasa historia yake ya Uhizbu. Sasa wazanzibar nao wasipotoa rais 2015 Muungano CCM ilikuwa ikijisifu utakuwa mbio kuvunjika sijui utasemaje na hilo???
   
Loading...