Sheikh Yahya Hussein afariki Dunia

sheikh-yahyabc.jpg

Mnajimu na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia asubuhi hii jijini Dar es Salaam.
Chanzo chetu cha habari ndani ya ofisi ya Sheikh Yahya kimesema mtabiri huyo amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitali ya Ukombozi iliyopo Morocco, jijini.
Sheikh Yahya amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na aliwahi kwenda India kwa matibabu

SOURCE: Global publishers
 
Aende salama!!!
Sijui sisiem watafanya mchakato gani kupata mnajimu mpya kwa maandalizi ya uchaguzi ujao!
 
R.I.P Sheh Yahya. Ni mtanzania mwenzetu na binadamu ana roho pia kama zetu; Bt tusiwe wanafiki ni kweli chama cha magamba wamepata pigo kwani walikuwa wanamtumia kugandisha akili za watanzania wengine wasielewe jinsi wanavyodhulumiwa
 
Kweli huyu alikuwa ni mnajimu, amefariki siku ya swalat, amefariki siku moja na Bob Marley, ameiwahi ile siku iliyotabiriwa kuwa ni mwisho wa dunia. Au yeye ndiye aliyekuwa dunia na mwisho wake ndo ulitabiriwa?

Nawasilisha...
 
pengo lake halitazibika,
alikua sehemu ya 'utamaduni wetu',
ikulu will never be the same,
hata hivyo alitabiri kufufuka kwake,
 
R.I.P Sheh Yahya. Ni mtanzania mwenzetu na binadamu ana roho pia kama zetu; Bt tusiwe wanafiki ni kweli chama cha magamba wamepata pigo kwani walikuwa wanamtumia kugandisha akili za watanzania wengine wasielewe jinsi wanavyodhulumiwa, sasa hivi nahisi Mungu atafungua mawazo yao
 
Kwani alijitabiria kwamba atakufa leo?

otherwise kama hakujitabiria atakufa leo na kafa kweli, basi kazi yote ya utabiri aliyoifanya katika maisha yake ni ya uongo kama hajaweza kujitabiria mwenyewe.

Haya Haya sasa, wale wanaotaka kumdhuru mkulu ndo nafasi yao hii maana mlinzi wake mkuu kaondoka now hadi atafute mwingine mtakuwa mmeshammaliza.

Kinyozi hajinyoi mwenyewe.
 
Mtu mwongo,mchawi,mchonganishi hawatauridhi ufalme wa mbinguni labda uko kwa mabikira 80.....

huyu shehe alikuwa mwongo,mchonganishi na mchawi vile vile
sheikh.yahyabc.jpg.jpg


Hizo ndio pete zake za majini alizompa JK aendelee kuwafanya watz mambumbumbu


mbona hilo ni li cocktail ring tu,
yapo mengi kama hayo hata 8020 fashions yanauzwa.
 
2peni News zaidi kwa walio karibu makazi ya kwake,maana Mi sijaamini kweli. Mmmmmh!!
 
Duuuuuuu!!!!!!! nakumbuka wakati marehemu kikongwe huyu anatabiri kuwa atakayesimama kupingana na Kikwete CCM atakufa, Askofu Josephat Gwajima alitangaza kuwa sheik Yahya Hussein atakufa yeye kwanza, sasa yametimia. Poleni sana wafiwa.
 
ina maana alishindwa kutabiri kifo chake,..duh kama ni kweli apumzike kwa amani,.nani atakyempa jk ulinzi mbadala?nafkiri jk atalia kuliko wengine wote...sijawahi kuukubali utabiri wake wa ubabaishaji hata siku moja..ashes to ashes,dust to dust..in ash we came in ash we shall return
 
mungu amlaze mahar pema pepon amen! bingwa mtabibu wa utabiri tanzania
 
Hihihii majini yatahamia kwenye mjengo mweupeeee kule ufukweni kuna mshirika wao,mi simo lakini
 
Mnajimu na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia asubuhi hii jijini Dar es Salaam.
Chanzo chetu cha habari ndani ya ofisi ya Sheikh Yahya kimesema mtabiri huyo amefariki dunia wakati akikimbizwa Hospitali ya Ukombozi iliyopo Morocco, jijini.
Sheikh Yahya amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na aliwahi kwenda India kwa matibabu. Habari zaidi tutawaletea katika mtandao huu na magazeti yetu.
 
Back
Top Bottom