Sheikh Yahya: Aidha Kikwete au Slaa kufa kabla ya Oktoba 31!

Hivi hawa jamaa, siasa na uchawi wapi na wapi? Mbona wako so narrow-minded hivyo jamani, wananitia kinyaa, mimi nafikiri huyu babu ana matatizo mawili kati ya haya
1. Uzee unamsumbua hivyo kujikuta akiropoka tu kama Babu Makamba au kwa sababu ya kigugumzi labda watu hawajamuelewa
2. Ni mbinu ya kibiashara ya kujitangaza apate wateja, ulidhani asipovuna msimu huu wa uchaguzi atampata nani tena?

Ashindwe kwa JINA la MUNGU aliye HAI
 
Habari za siku nyingi Malaria Sugu, kumbe upo bado, nimefurahi sana kusikia tena toka kwako kwani umenifanya nipate kitu cha kuiburudisha nafsi yangu kwa jinsi unavyochangia pointi zisizohusika.... kama kuona huoni hata kusikia pia???
 
Mimi wala siamini huu utabiri lakini najua kuwa Mungu daima anawachukia watu wenye kuvunja heshima za watu hata kuliko mafisadi na waizi.

Kwa kupora mke wa watu Dkt Slaa iwapo watanzania watafanya kichwa ngumu na kumpa kura zao basi uwezekano wa mabalaa kuikumba Tanzania ni mkubwa sana.

Usishangae hata siku ya kuapishwa kwake kukaambatana na kimbunga.

Mkapa kulikuwa na nia mbaya katika kuingizwa kwake katika urais. Angalia utawala wake ulishuhudia mabalaa yasiyo kawaida hapa Tanzania. Kwa Slaa hali itakuwa vurugu tupu.

Ni afadhali hayo matatizo yamkumbe sasa wakati wa kampeni ili tuokoke huko mbele.

Ndugu yangu usimseme Slaa wakati hujui usafi wa mgombea wako. Kuna wagombea wengi majina kapuni (ingawa najua wengi wenu mnawajua) wana vimada mia kidogo tena nje ya ndoa. Walau yeye katangaza kuwa kamuoa at least kaonekana yuko serious. Halafu mjue kuwa hili swala lina utata na linaonekana kukaa kisiasa zaidi. Wewe mke wako asionekane japo siku mbili halafu wala usitoe taarifa polisi wala kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki; leo umuone kwenye majukwaa useme "jamani mke wangu yule...!!" tena baada ya kuonekana mara nyingi sana....??? Anyway, hata kama kaiba, nafikiri tukianza kuchambua usafi, tutagundua wengine ni wachafu zaidi.
 
yesu analinda? sasa kama dk slaa alindwe na yesu mimi siemuamini yseu wako nimchague nani? tupunguze udini utamyima kura dk slaa

Kukurupuka kubaya sana hasa kwa mtu ambaye umekuwa member wa JF kwa muda mrefu. Jamaa kasema awalinde JK na Slaa; hivyo nawe unaweza kusema Mtume awalinde, Allah awalinde n.k. Inaruhusiwa kila mtu kwa imani yake kuwaombea wagombea wote. Mchangiaji hakuwa na mlengo wa kutetea mgombea yeyote hivyo sijaona swala la kumpotezea Slaa kura. Je hao wanaotumia ndumba na kutangaza kumlinda JK kwa ndumba zao, mbona husemi kuwa wanampunguzia kura JK especially kwa wale wasioamini uchawi..?? Hofu yako ya udini inaonyesha jinsi gani ulivyo mdini. Au unaogopa jina la Yesu...??? Isijeikawa na wewe ni mfuasi wa wana ndumba, ukashtuka ulivyosikia jina hilo linatamkwa hapa jamvini...!!!

Nawasilisha hoja.
 
Kukurupuka kubaya sana hasa kwa mtu ambaye umekuwa member wa JF kwa muda mrefu. Jamaa kasema awalinde JK na Slaa; hivyo nawe unaweza kusema Mtume awalinde, Allah awalinde n.k. Inaruhusiwa kila mtu kwa imani yake kuwaombea wagombea wote. Mchangiaji hakuwa na mlengo wa kutetea mgombea yeyote hivyo sijaona swala la kumpotezea Slaa kura. Je hao wanaotumia ndumba na kutangaza kumlinda JK kwa ndumba zao, mbona husemi kuwa wanampunguzia kura JK especially kwa wale wasioamini uchawi..?? Hofu yako ya udini inaonyesha jinsi gani ulivyo mdini. Au unaogopa jina la Yesu...??? Isijeikawa na wewe ni mfuasi wa wana ndumba, ukashtuka ulivyosikia jina hilo linatamkwa hapa jamvini...!!!

Nawasilisha hoja.

Malaria sugu hayupo hapa siku nyingi, kaja mwaka jana kutetea maslahi ya mafisadi. Na anashinda hapa 24 hrs/7days. Analipwa na Rostam
 
Hizi ni dalili za kuanguka kwa chama tawala.

Hapa inabidi dini zote kama ziko makini kuanza kupiga vita huyu bwana anapeleka taifa mahala kubaya sana.

Inabidi akamatwe mara moja kwa uchochezi. Hivi usalama wako wapi kumuoji huyu? Hatuwezi kuwa na taifa ambalo kiongozi wake anapatikana kwa Ushirikina.

Alishasema kwamba yeye ndio mkuu wa ulinzi wa rais JK, na rais kama the highest institution in the government, this means huyu mtabiri Yahaya ndio MKUU WA ULINZI WA NCHI, na kwa maana hiyo hawezi kuwajibishwa na chombo chochote (including Usalama wa Taifa) kile isipokuwa tu rais JK mwenyewe ambaye ndio mteuzi wake. Tanzania kazi tunayo, haya mambo ya ulozi na uchawi wenzetu waliacha karne nyingi sana zilizopita, lakini sisi ndio kwanza rais JK anakumbatia kama the sole means of his survival, shame on you Kikwete.
 
Jamani nyie ndio mnampa ujiko Yahaya. Wala hatakiwi kujadiliwa kihivyo. Kwanza tulishamfunika Dr Slaa kwa damu ya Yesu. Hivyo anafanya kazi bure. Labda kama anataka kutuambia kuwa rafikiye ndiye atakufa.
BTW Yahaya mwenyewe niliona akifa kabla ya uchaguzi huu. Hivyo kabla ya 31.10 Yahaya mwenyewe atakuwa amekufa. Ajiweke tayari.
 
Tanzania tuna rais wa awamu ya nne ambaye ni Jk. Na katika mfuatano wa tarakimu, namba nne huaminiwa kuwa ni namba ya shetani. Tukijaribu kuinasibisha hii namba na rais tulie nae na tabia yake ya kuwatumainia wachawi tunapata jibu kwamba huenda kweli namba hiyo imedhihirisha ushetani katika taifa la Tanzania.
Hakuna taifa lolote duniani linaloweza ruhusu mtu yeyote awe mchawi ama mchamungu kumtabiria rais aliyepo madarakani kifo likamnyamazia. Hii imeonekana Tanzania tu. Na kama vyombo vyote vya usalama vimenyamaza kimya basi inatupa picha kuwa mkuu wa nchi aliishawaelekeza kwamba huyo mchawi ndio dira ya taifa katika kipindi cha utawala wake. Sasa wachamungu wote nchini tumepewa home work ya kuomba Mungu kwa bidii sana ili kama mamlaka ya nchi kupitia kwa mchawi wao wamekusudia mabaya kwa mwenye haki mmoja, kisa kawa mpinzani wao kisiasa, basi kusudio lao ovu likawarudie wao na watoto wao wenyewe. Na kila mwenye kuipenda haki na aseme AAAMIN!!
 
huyu mganga nafikiri tumpuuze,anatisha watu.
lakini tukumbuke pia kwamba kula yake inapatikana kwa kutisha watu namna hii.hiyo ndio ajira yake.
no kutisha(utabiri),no food.
 
Hakuna Mgombea atakaekufa, Tatizo hamuelewi mafumbo ya huyo mzee wa MAJINI, anamaanisha Kati ya JK na Slaa lazima mmoja atashindwa japo wote ni maarufu. Hapo katumia lugha Ngumu ya uwakilishi ambayo anajua lazima itawachanganya watu kwa kiwango kikubwa including wagombea wenyewe haswa huyo Slaa maana kwa hakika kila mtu anajua he is backing JK, hiyo ni technique ya kudhoofisha kasi ya kampeni za Slaa, watu aanze kujadili kufa badala ya kunadi sera.

Ila zingatio kwa Viongozi wa Chadema, you better be very careful of what Dr Slaa will be eating, sleeping and drinking. Kwa CCM kusababisha vifo ni kitu cha kawaida. Mliona walivyomwondoa Mama Mbatia, Horace Kolimba, Sokoine na juzi juzi walimkosa kosa Mwakyembe. They can buy ushindi at any price. Na kama mjuavyo watu watalalamika na kuhuzunika after a month maisha yanaendelea nao wataendelea kutawala.

Kwa kweli is better kutumia hiyo tabiri za huyo Yahya into security motive wakati huo huo mambo mengine yasonge mbele. Huyo aje kushughulikiwa Mteja wake mkuu atakapotoka kwenye madaraka.
 
anataka tuache kujadili mambo ya msingi tuanze soga si unajua tabia za masheikh sio kuongea vitu vya muhimu ni kupiga soga na kunywa ghahawa anataka tuache kujadili mustakabali wa nchio yetu .,............yaani tuache kujadili ufisadi wa bosi wake na mteja wake wa majini kikwete kuhusu ufisadi wake na jinsi anavyowalinda mafisadi....
 
Hivi kwa nini hakamatwi?...........anayatisha hata majeshi ya ulinzi ya tanzania?........nchi imeoza, au kwa kuwa kikwete ndiyo mteja wake mkuu ndiyo maana hakamatwi?........hivi katiba inawaruhusu watabiri upumbavu km hawa?.....watz tuko tayari kuwa wapumbavu pamoja na mpumbavu huyu kwa kumwacha mpaka jumuiya za kimataifa zinatushangaa?.....kwa nini hapigwi risasi akafia huko badala ya kuiachwa anawapotosha watu?........
 
Tunaambiwa huyu analindwa na majini atafika salama? msilikize anavyosema

 
Last edited by a moderator:
Imeandikwa Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe.Ategaye mtego utamnasa mwenyewe.Abomoaye Boma nyoka atamwuma.Huyu shikh na mteja wake wamefika mwisho ikiwa alitaka kuuwa mpinzani wake aelewe atakufa yeye,na hili ameshaliona maana amepiga manyanga yake lakini wapi,sasa kilichobaki ni yeye,na huyo mteja wake kunaswa na mtego aliouweka.
 
Ni mtu mwendawazimu tu anayeweza kutilia maani mambo ya kishirikina ya huyu Mzee. Maisha ya mwanadamu hayaendeshwi na kushirikiana na majini. Kama yeye anafanya hivyo, basi aendelee kubakia yeye. Tutafanya makosa makubwa kama Taifa, kama leo hii tutaanza kumsikiliza na kufuatilia mambo ya kichawi anayoyafanya eti kulisaidia Taifa. Hana ubavu huo.
 
Huyu sheikh ni mganag njaa tu; kwani amekwisha tabiri kuwa hakutakuwa na uchaguzi October 31!!
 
Huyu mzee bwana. Tutaomba Mungu ikibidi hata kwa kufunga Dr slaa hatupatwa na hiyo mauti sababu slaa analidwa na nguvu za Mungu aliyejuu. wasiwasi wangu ni kwa huyo anayelindwa na majini maana yakishindwa kumdhuru Dr. yatarudi na hasira na kumdhuru mteja wa shehe. du niagieni jamani
 
anaye anguka anguka ndiyo huyo anaweza kuanguka mara kuanguka mara kaangukaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hizo ni habari njema sana kwa waTanzania kwa kuwa ukipima tu kwa macho kati ya Dr Slaa na JK unaona kuwa afya ya JK ni mbovu ukilinganisha na Slaa, na of course JK ashadondoka hadharani mara kibao. Kwa hiyo kama ni kufuata nguvu za Mungu huo utabiri wa uongo utamkuta JK zaidi so tusihofu. Tuzitunze shahada zetu kwa ajili ya kumpa kura Dr Slaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom