Sheikh yahaya angatuka rasmi jana;serikali nyingi kuangushwa zisizotimiza ahadi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Romana Mallya
25th February 2011

Mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein

Mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, ametabiri kuwa serikali ambazo hazitatimiza ahadi kwa wananchi zitaangushwa na kwamba siri nyingi za serikali zitavuja.
Kadhalika, amesema ndani ya miaka saba kuanzia Machi 13, mwaka huu, kutatokea machafuko, maandamano, uasi, maasi na kupinduliwa kwa serikali mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.
Katika taarifa iliyosomwa jana jijini Dar es Salaam na mtoto wake, Hassan Yahya Hussein kwa niaba yake, ilisema mambo hayo yatatokea kuanzia mwezi huo na yataendelea ndani ya kipindi cha miaka saba.

Sheikh Yahya alisema mambo hayo yatatokea baada ya kuja kwa sayari ya Uranus ambayo itaingia katika nyota ya Punda (Aries).

Alisema sayari hiyo huzizunguka nyota zote kwa miaka 84 na hukaa ndani ya nyota hiyo kwa kipindi cha miaka saba.
Alitaja mambo mengine yatakayojitokeza baada ya kuja kwa sayari hiyo kuwa ni mabadiliko ya ghafla ya kisiasa na kijamii, kuwepo kwa msukumo wa ghafla wa kufanya jambo, kuzinduka kwa watu kifikra na kutaka kujua ukweli na uwazi wa mambo yaliyojificha.

Mengine ni watu kudai haki zao kwa nguvu ambapo wataungana pamoja kupinga serikali na taasisi kubwa ambazo zitakuwa zinawatungia sheria na kanuni na kuwawekea vikwazo.
Alisema hilo litasambaa katika siasa na kwenye midahalo mbalimbali
.
Pia alisema kuanzia Julai, mwaka huu kutatokea mapinduzi ambapo polisi watafumaniwa kwenye maboma yao.
Alisema kutokana na ujio wa sayari hiyo ametabiri mwaka huu kutakuwa na mafanikio katika ugunduzi wa mambo ya afya ambapo wataalamu watavumbua dawa mpya ya kutibu magonjwa mengi.

Alisema wanasayansi watafanikiwa kugundua mbinu mpya za kutibu magonjwa yasiyokuwa na tiba kama Ukimwi na kansa.

Sheikh Yahya alisema kuanzia Januari 23, mwaka huu sayari ya Jupiter imeingia katika nyota ya Punda ambapo utabiri wake unaonyesha kuwa kutasikika habari nyingi kuhusiana na masuala ya michezo na wanamichezo.

Alisema wakati utabiri wake ukimuonyesha kuwa watu hao watapata mafanikio na umaarufu, kutasikika habari za vifo vya wanamichezo, wasanii na waandishi wa habari maarufu hapa nchini.
Alisema sayari ya Jupiter itaingia katika nyota ya ng'ombe Juni 4, mwaka huu ambapo itakaa huko hadi mwishoni mwa mwaka.

Alisema utabiri wake unaonyesha kutakuwa na mafanikio makubwa kwa watu wanaofanya biashara ya kujenga majumba na kuyauza au kuyapangisha kutokana na soko lao kuongezeka.
Sheikh Yahya alisema Aprili 4, mwaka huu sayari ya Neptune itaingia katika nyota ya Samaki ambapo utabiri wake unaonyesha kuwa kutakuwa na mabadiliko mengi ya hali ya hewa sehemu mbalimbali duniani.

Alisema kwa upande wa Tanzania wananchi wategemee kusikia habari za ukame na ukosefu wa maji kuanzia mwezi Aprili hadi Agosti mwaka huu.
 
hahahaa sasa anatabiri mambo ambayo yalishatokea??? ooh my!!!

Si mbaya lakini kutoa maoni yake kama raia wa tz.
 
Amejichokea mzee wa watu nawashauri hata waandishi wasiende kumsikiliza. Umeona sasa ameona wanasiasa wa africa wanawaachia kazi watoto wao naye anamwachia kazi kijana wake
 
Hassan Yahya Hussein kwa niaba yake

MMH JAMANI HUYU SIO KAWKAB??KAMA NI YEYE NDIE ANAMWACHIA LOH!!!!KAZI WANAYO
 
Romana Mallya
25th February 2011

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

Sheikh%20Yahya%20Hussein,(7).jpg

Mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein

Mnajimu maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, ametabiri kuwa serikali ambazo hazitatimiza ahadi kwa wananchi zitaangushwa na kwamba siri nyingi za serikali zitavuja.
Kadhalika, amesema ndani ya miaka saba kuanzia Machi 13, mwaka huu, kutatokea machafuko, maandamano, uasi, maasi na kupinduliwa kwa serikali mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania.
Katika taarifa iliyosomwa jana jijini Dar es Salaam na mtoto wake, Hassan Yahya Hussein kwa niaba yake, ilisema mambo hayo yatatokea kuanzia mwezi huo na yataendelea ndani ya kipindi cha miaka saba.
Sheikh Yahya alisema mambo hayo yatatokea baada ya kuja kwa sayari ya Uranus ambayo itaingia katika nyota ya Punda (Aries).
Alisema sayari hiyo huzizunguka nyota zote kwa miaka 84 na hukaa ndani ya nyota hiyo kwa kipindi cha miaka saba.
Alitaja mambo mengine yatakayojitokeza baada ya kuja kwa sayari hiyo kuwa ni mabadiliko ya ghafla ya kisiasa na kijamii, kuwepo kwa msukumo wa ghafla wa kufanya jambo, kuzinduka kwa watu kifikra na kutaka kujua ukweli na uwazi wa mambo yaliyojificha.
Mengine ni watu kudai haki zao kwa nguvu ambapo wataungana pamoja kupinga serikali na taasisi kubwa ambazo zitakuwa zinawatungia sheria na kanuni na kuwawekea vikwazo.
Alisema hilo litasambaa katika siasa na kwenye midahalo mbalimbali.
Pia alisema kuanzia Julai, mwaka huu kutatokea mapinduzi ambapo polisi watafumaniwa kwenye maboma yao.
Alisema kutokana na ujio wa sayari hiyo ametabiri mwaka huu kutakuwa na mafanikio katika ugunduzi wa mambo ya afya ambapo wataalamu watavumbua dawa mpya ya kutibu magonjwa mengi.
Alisema wanasayansi watafanikiwa kugundua mbinu mpya za kutibu magonjwa yasiyokuwa na tiba kama Ukimwi na kansa.
Sheikh Yahya alisema kuanzia Januari 23, mwaka huu sayari ya Jupiter imeingia katika nyota ya Punda ambapo utabiri wake unaonyesha kuwa kutasikika habari nyingi kuhusiana na masuala ya michezo na wanamichezo.
Alisema wakati utabiri wake ukimuonyesha kuwa watu hao watapata mafanikio na umaarufu, kutasikika habari za vifo vya wanamichezo, wasanii na waandishi wa habari maarufu hapa nchini.
Alisema sayari ya Jupiter itaingia katika nyota ya ng'ombe Juni 4, mwaka huu ambapo itakaa huko hadi mwishoni mwa mwaka.
Alisema utabiri wake unaonyesha kutakuwa na mafanikio makubwa kwa watu wanaofanya biashara ya kujenga majumba na kuyauza au kuyapangisha kutokana na soko lao kuongezeka.
Sheikh Yahya alisema Aprili 4, mwaka huu sayari ya Neptune itaingia katika nyota ya Samaki ambapo utabiri wake unaonyesha kuwa kutakuwa na mabadiliko mengi ya hali ya hewa sehemu mbalimbali duniani.
Alisema kwa upande wa Tanzania wananchi wategemee kusikia habari za ukame na ukosefu wa maji kuanzia mwezi Aprili hadi Agosti mwaka huu.

Sasa hapo utabiri uko wapi?aache ku2piga fix hata mimi ungekuja kwangu ningekuambia hivyohivyo hali halisi si inajionesha! hakuna utabiri ktk hili angeanza kusema toka mwaka jana sio timbwili lishatokea na yy anajifanya kutoka kimtindo
 
Amejichokea mzee wa watu nawashauri hata waandishi wasiende kumsikiliza. Umeona sasa ameona wanasiasa wa africa wanawaachia kazi watoto wao naye anamwachia kazi kijana wake

Waandishi hawa hawa ambao wakitishiwa kutopiga picha mwekezaji, wanaufyata au wale wa MwH?
 
anataka wateja huyo.... Lazima jk akamwulize mustakbali wake

jaaana katangaza rasmi ameachana na hii kazi amemwachia mwanae..lakini gafla akasema kuna kijana anaitwa hassan ataeleza zaidi ..aijulikani ndio kashika mikoba ama ....
 
All forms of horoscopes, Tarot cards, psychics, palm readings, fortune telling, crystal balls, Ouija boards, astrology, worshipping or contacting the dead (necromancy) and sorcery are of the Devil.

Astrology is of the Devil and is practiced by occultists in secret societies, as well as by the general public. Astrology is not the same as astronomy, which is simply the study of the universe.

Astrology is the worship of the stars, i.e., seeking spiritual wisdom and guidance from the universe, as if it were a life's force in itself (which it is not). God is the only deity Whom we ought to worship (Exodus 20:1-2; Isaiah 42:8). Astrology is idolatry!
 
Back
Top Bottom