Kuombwa talaka gerezani

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,881
5,183
Maisha ya mapenzi na ndoa yana changamoto sana. Ila matatizo ndio kipimo cha uvumilivu. Hiki kisa cha masheikh hawa, kimenikumbusha kisa cha Ayoub kuugua hadi kubaki ulimi tu na mkewe alisimama naye.

==============
Unguja.

Masheikh wa Uamsho, wameendelea kufunguka kuhusu machungu waliyopitia, huku baadhi wakieleza namna wake zao walivyowaomba talaka wakiwa gerezani

Taarifa kutoka miongoni mwao zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa masheikh wanne kati ya 36 waliombwa talaka, huku mmoja aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina akisema baada ya kutoka amebaini aliyekuwa mkewe ameolewa na ana mtoto mmoja.

Masheikh hao waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka 14 walioachiliwa huru kuanzia Juni 15 mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwaka

Sheikh huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema: “Ilikuwa mwaka jana mke mkubwa alinifuata gerezani, nia ni kuniambia maisha magumu afanyaje? Nilikuwa mpole na kumjibu sina la kusema kwa sababu sijui hatima yangu huku gerezani.”

“Aliniomba ushauri aende wapi nikamwambia sina la kusema pia, basi akaniambia nimpe talaka na nilimpa kwa sababu aliniambia maisha magumu na hajui mimi nitatoka lini gerezani. Juzi nimerudi nikaambiwa ameshaolewa na ana mtoto mmoja.”

Alisema huyo alikuwa mkewe mkubwa ambaye alibahatika kuzaa naye mtoto mmoja, lakini kwa sasa amebaki na mke mmoja ambaye ni mdogo mwenye watoto wawili, huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru mke huyo kwa uvumilivu

“ Namsihi aendelee kunivumilia maana ndio kwanza nimerudi kutoka gerezani. Miaka minane haikuwa mepesi kwa sababu nimerudi nyumba baadhi ya mali zangu nilizokuwa nazitumia kibiashara zote zimeharibika,” alisema.

Mbali na hilo, alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa ushirikiano wao uliosaidia kesi yao kuharakishwa kusikilizwa na hatimaye kuachiliwa huru.

Jana aliyekuwa kiongozi wa Uamsho, Sheikh Mselem Ali Mselem aliswali katika msikiti wa Swahaba Mtoni Kidatu, Mjini Unguja huku waumini waliojitokeza katika ibada hiyo wakionyesha furaha yao kwa sheikh huyo.

Source: Mwananchi
 
sheikhpic

Summary

  • Masheikh wa Uamsho, wameendelea kufunguka kuhusu machungu waliyopitia, huku baadhi wakieleza namna wake zao walivyowaomba talaka wakiwa gerezani

Unguja. Masheikh wa Uamsho, wameendelea kufunguka kuhusu machungu waliyopitia, huku baadhi wakieleza namna wake zao walivyowaomba talaka wakiwa gerezani

Taarifa kutoka miongoni mwao zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa masheikh wanne kati ya 36 waliombwa talaka, huku mmoja aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina akisema baada ya kutoka amebaini aliyekuwa mkewe ameolewa na ana mtoto mmoja.

Masheikh hao waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka 14 walioachiliwa huru kuanzia Juni 15 mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwaka

Sheikh huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema: “Ilikuwa mwaka jana mke mkubwa alinifuata gerezani, nia ni kuniambia maisha magumu afanyaje? Nilikuwa mpole na kumjibu sina la kusema kwa sababu sijui hatima yangu huku gerezani.”

“Aliniomba ushauri aende wapi nikamwambia sina la kusema pia, basi akaniambia nimpe talaka na nilimpa kwa sababu aliniambia maisha magumu na hajui mimi nitatoka lini gerezani. Juzi nimerudi nikaambiwa ameshaolewa na ana mtoto mmoja.”

Alisema huyo alikuwa mkewe mkubwa ambaye alibahatika kuzaa naye mtoto mmoja, lakini kwa sasa amebaki na mke mmoja ambaye ni mdogo mwenye watoto wawili, huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru mke huyo kwa uvumilivu.

“ Namsihi aendelee kunivumilia maana ndio kwanza nimerudi kutoka gerezani. Miaka minane haikuwa mepesi kwa sababu nimerudi nyumba baadhi ya mali zangu nilizokuwa nazitumia kibiashara zote zimeharibika,” alisema.

Mbali na hilo, alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa ushirikiano wao uliosaidia kesi yao kuharakishwa kusikilizwa na hatimaye kuachiliwa huru.

Jana aliyekuwa kiongozi wa Uamsho, Sheikh Mselem Ali Mselem aliswali katika msikiti wa Swahaba Mtoni Kidatu, Mjini Unguja huku waumini waliojitokeza katika ibada hiyo wakionyesha furaha yao kwa sheikh huyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Sijui kilichopelekea hao Mashekh wa Uamsho kutuhumiwa wao na si watu wengine!

Cha msingi tupendane na kuwa watu wenye subra na kusameheana wenyewe kwa wemyewe kwa sababu hakuna mkamilifu.Hasa yale matamshi ambayo yanaweza leta hisia ngumu kwa wengine.Nadhani Viongozi wetu wa dini kwa ujumla wao kuna la kujifunza hapo.
 
Back
Top Bottom