Sheikh wa mkoa wa Mbeya asema wanaombeza Magufuli walaaniwe

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
2,995
2,000
pic+sheikh.png

Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mwansansu amesema anayezibeza juhudi za Rais John Magufuli anapaswa kulaaniwa.

Sheikh Mwansasu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu) usiku alipokuwa akisoma dua ya kumuombea Rais Magufuli kwenye kusanyiko la waumini wa Kiislamu wa mikoa ya Mbeya na Songwe.

Dua hiyo ilienda sambamba na futari iliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust, kwa waumini wa dini ya Kiislam na kufanyikia katika Ukumbi wa Royal Tughimbe jijini hapa.

“Lazima kwa umoja wetu tuendelee kuungana na Rais wetu katika kupambana na wezi na mafisadi wa rasilimali zetu, na nitamshangaa mtu mwenye akili timamu anapinga juhudi hizi kwa sababu ya itikadi za chama chake au mtu yeyote ni lazima aangamie mara moja,” amesema.

Amesema anachokifanya Rais Magufuli ni kwa ajili ya masilahi ya Watanzania wote na siyo familia yake wala chama chake hivyo Watanzania kwa umoja wao wanapaswa kuungana kwa pamoja katika kumuunga mkono ikiwa ni pamoja na kumuombea kwa Mungu kwani ndiye mlinzi mkuu.

Kuhusu futari hiyo amesema alichokifanya Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson kupitia taasisi yake ni jambo la thawabu hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati yeye ni Mkristo.

“Huu ni mfano mkubwa, Tulia kuwapa chakula Waislamu hivyo na sisi waislamu tuweze kufanya hivi kwa kuwaita jamii isiyo ya kiislamu na kukaa nayo pamoja zungumza na kufuturu pamoja,”amesema.

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Songwe, Hussein Issah Batuzi, amesema uislamu ni kuitisha jamii tofauti tofauti kukaa pamoja na kuzungumza na kuleta amani na utulivu badala ya kuleta shida, vurugu na patashika kwa jamii nyingine jambo ambalo mwenyezi Mungu anakataa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya (CCM) Wilson Nkhambaku, ametoa rai kwa viongozi hao wa dini ya kiislamu na Watanzania wote bila kujali tofaui za kiitikadi kuendelea kuwaombea viongozi wa Serikali kwa kazi ngumu wanayofanya ya kupambana na mafisadi wa rasilimali za Taifa.

“Naomba muendelee kuwaombea vingozi wetu ili Mungu aweze kuwapa ujasiri mkubwa na upendo kwa manufaa ya Taifa letu na waendelee kusimamia uchumi wa nchi yetu kwani kufanya hayo kunahitaji ujasiri na ulinzi wa mwenyezi Mungu.”amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Graph

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
2,742
2,000
Alaaniwe na nani? upuuzi mtupu, anatafuta kiki
Hawa viongozi wa dini tumewaingiza sana kwenye siasa sasa kila kitu imekua mungu mungu, hii nchi si tujiite tu non-secular kwa style hii. Serikali inabidi ikae mbali na dini mapema sana, siku moja patakuja kuchafuka tugeuke libya.
 
nkese

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
2,913
2,000
View attachment 527486

Sheikh wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Mwansansu amesema anayezibeza juhudi za Rais John Magufuli anapaswa kulaaniwa.

Sheikh Mwansasu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu) usiku alipokuwa akisoma dua ya kumuombea Rais Magufuli kwenye kusanyiko la waumini wa Kiislamu wa mikoa ya Mbeya na Songwe.

Dua hiyo ilienda sambamba na futari iliyoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust, kwa waumini wa dini ya Kiislam na kufanyikia katika Ukumbi wa Royal Tughimbe jijini hapa.

“Lazima kwa umoja wetu tuendelee kuungana na Rais wetu katika kupambana na wezi na mafisadi wa rasilimali zetu, na nitamshangaa mtu mwenye akili timamu anapinga juhudi hizi kwa sababu ya itikadi za chama chake au mtu yeyote ni lazima aangamie mara moja,” amesema.

Amesema anachokifanya Rais Magufuli ni kwa ajili ya masilahi ya Watanzania wote na siyo familia yake wala chama chake hivyo Watanzania kwa umoja wao wanapaswa kuungana kwa pamoja katika kumuunga mkono ikiwa ni pamoja na kumuombea kwa Mungu kwani ndiye mlinzi mkuu.

Kuhusu futari hiyo amesema alichokifanya Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson kupitia taasisi yake ni jambo la thawabu hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wakati yeye ni Mkristo.

“Huu ni mfano mkubwa, Tulia kuwapa chakula Waislamu hivyo na sisi waislamu tuweze kufanya hivi kwa kuwaita jamii isiyo ya kiislamu na kukaa nayo pamoja zungumza na kufuturu pamoja,”amesema.

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Songwe, Hussein Issah Batuzi, amesema uislamu ni kuitisha jamii tofauti tofauti kukaa pamoja na kuzungumza na kuleta amani na utulivu badala ya kuleta shida, vurugu na patashika kwa jamii nyingine jambo ambalo mwenyezi Mungu anakataa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya (CCM) Wilson Nkhambaku, ametoa rai kwa viongozi hao wa dini ya kiislamu na Watanzania wote bila kujali tofaui za kiitikadi kuendelea kuwaombea viongozi wa Serikali kwa kazi ngumu wanayofanya ya kupambana na mafisadi wa rasilimali za Taifa.

“Naomba muendelee kuwaombea vingozi wetu ili Mungu aweze kuwapa ujasiri mkubwa na upendo kwa manufaa ya Taifa letu na waendelee kusimamia uchumi wa nchi yetu kwani kufanya hayo kunahitaji ujasiri na ulinzi wa mwenyezi Mungu.”amesema.

Chanzo: Mwananchi
Yeye ana hakika kuwa hajalaaniwa tayari?
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,895
2,000
Sheikh ubwabwa huyo,wakati anaongea hayo taswira iliyopo kichwani mwake ni masahani ya ubwabwa na pilau.
 
london1

JF-Expert Member
Aug 16, 2011
354
1,000
Naomba wajuzi na wabobevu mnisaidie katika hili: Hivi inaswihi kumuombea dua mtu asiyekuwa muislamu?
Inaruhusiwa,sharti ni kuwa awe yupo hai,Mungu ni wa wote.ushahidi ni kuwa;prophet of islam(Neema za Mungu zimuendee n Amani)alikuwa akimuombea babu yake(ndio alimsaidia sana na kumlea) hakuwahi kuukubali uislamu mpaka yule babu alipokufa ndipo alipoacha, sababu ukifa,safari nyingine sasa.i hope this helps! Cioa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom