Sheikh Seleiman Takadir

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,055
3,238
[HASHTAG]#HISTORIA[/HASHTAG] DONDOO MUHIMU KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU WA TANGANYIKA

SHEIKH SULEIMAN TAKADIR SHUJAA "ALIYETOSWA"

Sheikh Suleiman Takadir alikuwa mwanaharakati mzalendo na mwanazuoni wa Kiislamu kutoka nchini Tanganyika. Vilevile alikuwa mmoja kati ya watu wa awali walioshirikiana na Nyerere katika harakati za kudai Uhuru wa Tanganyika. Pamoja na yote hayo jina la Sheikh Suleiman Takadir halijapatwa kutajwa popote katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika wala katika historia ya TANU.

Hatajwi na hakupata kutajwa baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 na wala haidhaniwi hata kama atakuja kutajwa au kukumbukwa na hawa viongozi walio katika madaraka hivi sasa. Sheikh Suleiman Takadir hutajwa kila linapotokea jambo ambalo Waislam huonekana wanadhulumiwa na serikali kwani ilikuwa Sheikh Suleiman Takadir ndiye aliyeweka agenda ya hali ya baadae ya Waislam na Uislam katika Tanganyika huru mwaka 1958.

Jambo hili alipolileta lilitishia kuigawa TANU katika misingi ya dini katika wakati amabo umoja wa Waafrika ulikuwa unahitajika sana. Mwaka wa 1958 TANU ilikuwa imeenea nchi nzima na tayari iko katika barabara ya kuelekea kuchukua madaraka ya ndani na kisha Tanganyika kupata uhuru wake kamili.

HISTORIA YAKE KATIKA SIASA NA TANU

Sheikh Suleiman Takadir kwanza alikuwa "mwanazuoni" kisha alikuwa Mwenyekiti muasisi wa Baraza la Wazee wa TANU kuanzia TANU ilipoundwa mwaka 1954 hadi "alipotoswa" mwaka 1958 kwa kosa la "kuchanganya dini na siasa. Sheikh Takadiri alishiriki vilivyo ndani ya Baraza la Wazee wa TANU katika kutayarisha safari ya Nyerere kwenda UNO mwaka 1955. Wapenzi wake katika harakati za kupigania uhuru walimpachika jina la utani wakimwita "Makarios," wakimlinganisha na Askofu Makarios wa Cyprus na Ugiriki aliyekuwa anapambana na ukoloni wa Waingereza wakati yeye alipokuwa anapambana na Waingereza katika ardhi ya Tanganyika. Sasa kwa kuwa Suleiman Takadir alikuwa sheikh na mpambanaji ndipo walimpa jina hilo la "Makarios" na kwa hakika jina hili lilimkaa, likamwenea vyema na yeye akalipenda.

Mikutano ya mwanzo ya TANU ilikuwa ikifanyika Mnazi Mmoja mbele baadaye ilipojengwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima. Wakati ule pale palikuwa hakuna jengo lolote, palikuwa na kiwanja kitupu na ardhi ile ilikuwa mali ya Mzee John Rupia Makamu wa Rais wa TANU. Kiwanja hiki baaadaye Mzee Rupia aliwapa TANU na TANU wakaanzisha Chuo Kikuu pale mara baada ya uhuru. Mikutano ya kwanza ya TANU ikifanyika pale Mnazi Mmoja na kabla Nyerere hajapanda juu kwenye jukwaa kuzungumza na wananchi alikuwa kwanza anatangulia Sheikh Suleiman Takadir kusawazisha uwanja na kuwaweka wananchi tayari kumsikiliza kiongozi wao.

Kama alivyokuwa Nyerere, Sheikh Suleiman Takadiri alikuwa na kipaji cha kuongea. Leo hii huenda baadhi ya wasomaji wangu wasiamini lakini ukweli ni kuwa Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kabla hajazungumza lolote alikuwa akipiga "fat-ha," wananchi wakaitika na kwa umoja wao wakasoma, "Surat Fat-ha," sura ya ufunguzi katika Qurani Tukufu, kisha Sheikh Takadir akaomba dua na wananchi wakawa wanaitika kwa pamoja, "Amin," Amin," "Amin." Baada ya hapo ndipo atapanda Nyerere na kuanza kuhutubia. (Picha za mwanzo za mikutano hii zipo na zilipigwa na Mzee Shebe ambae katika miaka ile ya 1950 alikuwa na studio yake Mtaa wa Livingstone na Kipata. Vilevile Inaaminika ya kwamba Mzee Shebe ndiye mpiga picha wa kwanza wa TANU na Nyerere).

Sheikh Suleiman Takadir na huyu ndiye Nyerere kama alivyokuja kutambulishwa kwa watu wa Dar es Salaam na Sheikh Suleiman Takadir kwa mara ya kwanza mwaka wa 1954. Kabla ya hapo Nyerere alikuwa akijulikana na watu wachache katika TAA. Sheikh Takadir alimpenda sana Nyerere kiasi kuwa mwaka 1957 katika hotuba aliyotoa katika tafrija moja ya taarab Mtaa wa Mvita, alimwita Nyerere, "Mtume wa Afrika," aliyetumwa na Mungu kuwaokoa Waafrika. Maneno yale ya Sheikh Suleiman Takadir alikuwa kama anamtabiria Nyerere makubwa katika mustakabali wa Afrika, kwani miaka mingi baadaye Nyerere alikuja kusimama mstari wa mbele katika kuikomboa Afrika kutoka makucha ya wakoloni.

Nyerere akawa hapungui nyumbani kwa Sheikh Takadir Mtaa wa Swahili. Nyumba hii iko jirani na kilabu ya mpira ya Pan Africa. Kutembelewa na Nyerere pale nyumbani kwake ikapelekea baba mwenye nyumba, Jumbe bin Jumaa wa Digosi amuhamishe nyumba Sheikh Takadir asije kumponza kwa kwani Nyerere alijulikana kama adui mkubwa wa Waingereza.

Pichani Kutoka kushoto: Sheikh Suleiman Takadir, Mbutta Milando, John Rupia na Julius Nyerere. Hao Waliowazunguka na silaha za jadi ni Bantu Group kundi la vijana wa TANU lililokuwa linatoa ulinzi kwa viongozi wa TANU. Picha Hii Ilipigwa Mwaka wa 1955.

Itaendelea...
f08abb1dbc2d0eeed57813e1f459b561.jpg
 
Mungu awarehemu wapigania Uhuru wa nchi kuanzia kizazi cha awali cha wakina chifu Mkwawa,Kibasila,Isike,Milambo,Kinjeketile,Abushiri na wenzao mpaka kizazi cha kina Kawawa,Takadir,Sykes,Bibi Titit,Rupia,Nyerere na wenzake.
 
Sawa tumekuelewa, Ongera kwa kutujuza ila usije ukaanza kuingiza Dini katika uzi wako huu mzuri, muelezee mtu tu kwa ushujaa wake bila kuleta maudhui ya dini ili isije ukapoteza ladha ya huu uzi mtamu
 
Mimi ngoja nisubiri maelezo kutoka kwa Mohamed Saidi kama hili la Sheikh Takadir analifahamu!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom