Uchaguzi 2020 Sheikh Ponda: Zanzibar itakuwa ni mlango wa kuvunjika amani uchaguzi mkuu 2020

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,853
141,781
Katibu Mkuu wa Jumuiya za Kiislamu Tanzania sheikh Issa Ponda amedai kuwa kuna wazanzibar wengi hawajaandikishwa kwenye daftari la wapiga kura kinyume cha utaratibu.

Ponda amesema kwa Siasa zinazoendelea Zanzibar kwa sasa ni wazi kabisa kama amani itavunjika wakati wa uchaguzi basi mlango wake utakuwa ni huko Zanzibar.

Sheikh Ponda amesema hayo katika mahojiano yaliyorushwa mubashara na Star tv katika kipindi cha Tuongee Asubuhi mada ikiwa Amani wakati wa Uchaguzi.

Maendeleo hayana vyama!
 
johnthebaptist, Watu makini ni wale wenye kuweza kuona kwa jicho la tatu. CCM hawajali kwa sababu ya kubebwa kwa mbeleko ya vyombo vya dola. Lakini hawajui kuwa dhuluma huwa ina mwisho, na hapo ndipo mbeleko huchanika.

Waliichezea vibaya fursa muhimu sana ya kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa kwa ulafi, uchoyo na tamaa za madaraka, huku wakipoka kwa makusudi ushindi wa wananchi. Sasa ni kazi kwao, kusuka ama kunyoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SHEHE Ponda sio mzanzibarI akamatwe UPESI akaungane na mashehe wenzie ndani. Zanzibar ni nchi kamili na huru.Hawezi fanya Tanzania bara eneo lake la kuishambulia nchi ya zanzibar .AKAMATWE UPESI


Akamatwe kwa kosa gani?
 
Back
Top Bottom